Kuna taarifa za uhakika wa jambo hili. Na nilikuwa Bukoba nikatembelea Kijiji kimoja katika wilaya ya Misenyi nikapewa taarifa na uongozi wa Kijiji kuhusu kuwepo kwa mafunzo haya na vijana walikuwa wakisajiliwa katika vyuo hivi bubu. haikujulikana bado malengo hasa ni nini. Bahati mbaya sana Usalama wa taifa nao umegawanyika, hili si jambo la aja bu au la kupingwa. Ni utawala peke yake utakaoamua kama mambo haya ambayo yanaweza kuchukuliwa kisiasa, lakini yakaleta madhara, kwani katika umri mdogo, na kutokuwa na taarifa za uhakika kama ni karate tu au kuna itikadi nyingine mfano za "extremism na fanatic" zikiendelezwa, na pale ambapo vita ya dunia ya sasa inayotia hofu ni ile ya kushawishi baadhi ya waislamu kuwa wanaonewa, na njia peke yake ni kulipiza kisasi na kujitoa muhanga kufa kwa ajili ya dini, badala ya kuwapa nafasi zaidi za kielimu na kiuchumi na ujuzi ili washindane katika soko la ulimwengu linalozingatia ujuzi zaidi badala ya ushabiki na mtizamo. Si waislamu wote wanaoamini hayo, ila vijana wakiandaliwa kuamini hili basi kizazi kinachokuja cha vijana wa kiislamu kinaweza kuwa na idadi kubwa ya watu wanaokuwa na itikadi ya kufikirika kuonewa na jamii au kundi lingine na ajira yao ikawa ni udhalimu, ugaidi na kuharibu katika jina la kupigania haki ya kuonewa. Bila shaka wengi mtakubaliana na mimi, waislamu wa kweli wa sasa ni wale ambao wanaongeza juhudi katika misikiti kuwapa vijana wao fursa za kujiinuaa kielimu dunia, ujuzi mbalimbali na kuunganisha imani ya Kiislamu ambayo nguzo yake ni upendo na amani na wote, kama Mtume Muhamad (SAW) alivyokuwa akifanya. Bahati mbaya aya zinazozungumzia matendomema ya Mtume (SAW) ambaye aliweza hata kupatanisha makundi hasimu kipindi fulani katika jamii yake miaka hiyo, makundi ambayo hakuna mtu yeyote aliwahi kufanikiwa kuyapatanisha, hazizungumziwi, kwani hazikidhi maslahi dhalimu ya baadhi ya makundi ya watu wasiokuwa na nia njema. Asiposimama kiongozi na kuzungumza hili na kulipuuzia, basi tuna hatari kubwa ya huko baadae.