Usalama wa taifa kazi yao nini? Watuambie Panya road ni akina nani?

Usalama wa taifa kazi yao nini? Watuambie Panya road ni akina nani?

Usalama wa Taifa ni Idara iliyo chini ya Ofisi ya Rais, Utawala Bora.

Usalama wa Taifa siyo Mamlaka (Authority), kwa hiyo haina mamlaka ya kutoa taarifa wala kufanyia kazi taarifa, bali kazi yao ni kukusanya taarifa na kuzipeleka taasisi husika ili zifanyiwe kazi kulingana na majukumu ya taasisi iliyopelekewa taarifa hizo
 
Ni kwanini hadi leo hawajatupa namba za NIDA za panya road wote Tz? Why?!
 
Usalama wa Taifa ni Idara iliyo chini ya Ofisi ya Rais, Utawala Bora.

Usalama wa Taifa siyo Mamlaka (Authority), kwa hiyo haina mamlaka ya kutoa taarifa wala kufanyia kazi taarifa, bali kazi yao ni kukusanya taarifa na kuzipeleka taasisi husika ili zifanyiwe kazi kulingana na majukumu ya taasisi iliyopelekewa taarifa hizo
Duh
 
Si walimshindwa kigogo watawaweza hao wengine?
 
So simple tu

Waambieni wananchi HUKO MITAANI WAPIGE KURA ZA SIRI

30 min mnao panya road KIGANJANI

Wakisikia KURA ZA SIRI ZINAPIGWA...Mitaani watakimbia hiyo mitaandao yao
Good idea, hili lifanyike
 
Ni kwanini hadi leo tunasumbuliwa na Panya road? Kazi ya Usalama wa taifa ni nini?
Kazi za usalama wa taifa ni kulinda usalama wa rais na viongozi wa juu wa nchi. Kazi nyingine ni kufuatilia nyendo za watu mbalimbali wanaoweza kuathiri uelekeo wa nchi, mfano viongozi wa majeshi, wabunge, baadhi ya watumishi wa umma, mawaziri, wakuu wa vitengo serikalini, wakuu wa mashirika, waasiasa, viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa makanisa, watu wenye utajiri mkubwa, watu maarufu nk.

Kazi nyingine ni kudhibiti hali ya mambo pale ambpo nchi inaingia kwenye uchaguzi mkuu. Kufanya udukuzi na kuingilia harakati za vyama vya siasa, kufanya hujuma kwa maelekezo ya waliopo madarakani, kufuatilia na kuvuruga mikakati ya wapinzani, kushawishi baadhi ya sera, mpaka kuiba uchaguzi pale inapobidi ili kutimiza malengo maalum yaliyoamuliwa na baadhi ya watu waliojipa jina la deep state.

Hao panya road hawana uwezo wowote wa kubadili uelekeo wa nchi. Panya road wanawaibia wananchi wanaoishi maeneo ya kimaskini tu. Panya road ni sehemu ya uholela wa makazi duni. Wengi wamekulia huko huko wanakotamba. Huko hata polisi hawahangaiki kuweka ulinzi. Panya road hawawezi kwenda maeneo ya wenye kipato cha juu kamwe.

Mpambane nao tu nyie wananchi wanyonge mkisaidiwa na polisi wachache. Hao ni watoto wenu mliokua nao huko uswazi, mkawapa malezi duni, elimu duni na maadili duni. Msilazimishe usalama wa taifa waje waangalie familia za watu wasio na maadili. Siyo kazi yao.
 
Kazi za usalama wa taifa ni kulinda usalama wa rais na viongozi wa juu wa nchi. Kazi nyingine ni kufuatilia nyendo za watu mbalimbali wanaoweza kuathiri uelekeo wa nchi, mfano wabunge, baadhi ya watumishi wa umma, mawaziri, wakuu wa vitengo serikalini, wakuu wa mashirika, waasiasa, viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa makanisa, watu maarufu nk.

Bila kusahau kudhibiti hali ya mambo pale ambpo nchi inaingia kwenye uchaguzi mkuu. Kufanya udukuzi na kuingilia harakati za vyama, vya siasa, kufanya hujuma kwa maelekezo ya waliopo madarakani, mpaka kuiba uchaguzi pale inapobidi.

Hao panya road hawana uwezo wa kubadili uelekeo wa nchi. Mpambane nao tu nyie wananchi mkisaidiwa na polisi wachache tu. Mnawaweza.
Hahahahh, u r not serious
 
Subiri 2025 ndo utajua kazi ya hizo KIMA..
 
Usalama wa Taifa ni Idara iliyo chini ya Ofisi ya Rais, Utawala Bora.

Usalama wa Taifa siyo Mamlaka (Authority), kwa hiyo haina mamlaka ya kutoa taarifa wala kufanyia kazi taarifa, bali kazi yao ni kukusanya taarifa na kuzipeleka taasisi husika ili zifanyiwe kazi kulingana na majukumu ya taasisi iliyopelekewa taarifa hizo

Sawa lakini Hawa huripoti kila kitu hata mvua ikinyesha wanaripoti,kwanini hawajaripoti suala la panya road?
 
Back
Top Bottom