Usalama wa Taifa (TISS) kaeni kando na CCM, mnachafuka

Usalama wa Taifa (TISS) kaeni kando na CCM, mnachafuka

DOMBWELA

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2014
Posts
757
Reaction score
843
Wana JamiiForums "msema kweli ni mpenzi ni mpenzi wa Mungu", hapo awali kabla sijawa karibu na Taasisi hii TISS nilijua na kuamini kuwa TISS ni washauri wa mambo ya kitaifa kwa maslahi ya Taifa na sio kwa maslahi ya CCM au kikundi cha watu fulani.

Niseme ukweli, nimeumia kujua kuwa wamekuwa wakijua uovu unaofanywa na CCM na kundi lake lakini hawachukui hatua kwa maslahi ya Taifa lao, jamii yao, ndugu zao na vizazi vyao wakiwa wamekwisha tangulia mbele ya haki.

Hivi ni kweli bado mpo kwa maslahi ya Taifa, kama ni kweli bado mpo kwa maslahi ya Taifa inakuwaje haya yanayopoteza mwelekeo wa Taifa letu yanafanyika mkijua, hamshauri au kuzuia yasifanyike kwa maslahi ya Taifa letu?

Nimeangilia mwenendo wa baadhi ya watumishi wetu katika ushiriki wa chaguzi zilizopita za Serikali za Mitaa, kweli nimeanza kuamini kuwa mpo sasa hivi kwa maslahi ya CCM na sio maslahi ya Taifa letu?

Naomba kuuliza tena, hivi vyama vya upinzani na wapinzani wapo kwa maslahi ya Taifa letu?, na kama wapo kwa maslahi ya Taifa letu kwa nini wanafanyiwa haya maovu na CCM lakini hamuwashauri nini cha kufanya kuondokana na changamoto zinazo wakuta kwa maslahi ya Taifa letu kama mnavyofanya kwa CCM?

Au ni lini mmewahi kushauri au saidia vyama vya upinzani kama mnavyo shauri na kusaidia CCM? Nasema hayo kwasababu ninajua na nimeona mlivyosaidia CCM kuanzia uandikishaji, vetting ya wagombea wa CCM na zoezi la uchaguzi, nk.

Nashauri tuachaneni au tuvunjeni ndoa na CCM vinginevyo tutaendelea kupoteza heshima ya Taasisi yetu tuliyojijengea ndani na nje ya Taifa letu, lakini ndoto zetu kama Taifa tutachelewa kuzifikia.

Hebu tuige kwa Taasisi kama zetu za Marekani, Izrael wanavyo handle issue za kitaifa maana wao hawafungamani na chama cha siasa au kikundi chochote, wao wanaangalia maslahi ya Taifa lao tu.

Nimtazamo wangu tu kwa issue za kitaifa, naomba mnivumilie sijui mitazamo yenu juu ya Taasisi yetu ya TISS kwa masuala ya Kitaifa.
 
Hawa wakusanya taatifa wetu wamepotoka kabisa na kupoteza muelekeo!

Kwa sasa wao taifa ni CCM na Magufuli!!

Yaani unakuta mtu wa taasisi hii anajiapiza kabisa kuitumikia CCM unamuangaliaa....unaishia kukubaluana na watu wanaosema TZ hawa watu wanachaguliwa kwa kuangalia watu wenye upeo mdogo ili wasihoji mambo kwa akili!
 
Yaani haujui boss wa TISS anateuliwa na nani
Aisee hata kama anateuliwa na Rais bado sijaamini kwa haya yanayoendelea!. Ila inawezekana unachokisema kuwa yaweza ikawa tatizo maana hata Mhe Kabwe Zitto aliwahi kushauri kuwa Taasisi yetu hii ifanyiwe reform lakini tumechelewa kumuelewa kama Taifa alichomaanisha!.
 
Acha upotoshaji chombo hiki ni huru na hakina maslahi yoyote na CCM umejipachika kwenye chombo ili tuamini andiko lako la kuwa na wewe ni mmoja wa wana chombo kiacheni kifanye kazi sake kwa maslahi mapama ya Taifa hili
 
Mwanzo mwisho ni kulalamika tu. Sema wazi ni kipi kimefanywa na hao unaowaita TISS? Acha kulalama hovyo kama mjusi aliebanwa na mlango
 
Unataka TISS wawe upande wa wapinzani ambao ni wasaliti wa nchi yetu hasa Chadema wanaoshirikiana na maadui zetu wa nje? Unaona wanavyofurahia kukamatwa kwa ndege zetu huko nje? Uliona walivyokuwa wanashangilia magaidi waliokuwa wanauwa wananchi wa Kibiti? Wapinzani ni maadui wa TZ hivyo TISS hawawezi kuwa upande wao. Washauri kwanza hao wapinzani waache usaliti kwanza kwa nchi yao!
Kama wewe haufurahii kukamatwa kwa ndege basi ni mjinga, mtu makini anayependa haki hufurahi anapoona anayedaiwa analazimishwa kulipa deni, yule mkulima ni kiumbe na kila siku inavyokwenda anazeeka na mwisho atafariki na akifariki serikali itashangilia kwa kutokuwepo mtu wa kumlipa kwa uzembe wa mdai kufariki wakati mikakati ya kulipa imekamilika! Mswahili hakosi neno.
 
hio kazi uweled uliishia kwa mwinyi .kwanza walikuwa hawatambuliki. sasa .sasa hivi kwenye kundi la watu rahisi kuwatambu wao
 
Back
Top Bottom