Usalama wa Taifa (TISS) kaeni kando na CCM, mnachafuka

Acha upotoshaji chombo hiki ni huru na hakina maslahi yoyote na CCM umejipachika kwenye chombo ili tuamini andiko lako la kuwa na wewe ni mmoja wa wana chombo kiacheni kifanye kazi sake kwa maslahi mapama ya Taifa hili
Kipofu wa kujitakia wewe!
 
Mwandishi wa taarifa hii ni mpotoshaji TISS ni taasisi yenye weledi na ina heshima kubwa duniani kwa utendaji wake uliotukuka na inaendesha shughuli zake pasipo kufungamana na upande wowote bali inatizama maslahi ya Taifa pekee.
 
Kwani lazima u comment?
 
CCM bado wanahodhi idara zote nyeti za umma kama mali yao, na ndiyo maana wanaweza kufanya lolote wakati wowote na hakuna raia wenye uwezo wa kuwahoji.
Ref; uchaguzi ala sorry uchafuzi serikali za mitaa majuzi.
 
Mtoa taarifa andiko lako limejaa hisia za uchama kuliko fact, hujaeleza wamesaidiaje na maeneo gani?
Nimekueleza mfano mdogo walivyosaidia katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuanzia uandikishaji, vetting ya wagombea wa CCM na wakati wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa!.
 
Ni ngumu tumefata mfumo Wa ujamaa chama ndo umiliki dola.Kazi ya tiss,polisi,nk ni kulinda chama.Mfumo wa magharibi dollar hailindi maslai ya chama bali dola ulinda nchi
Nadhani huu ndio ukweli wenyewe, lakini ninachojiuliza huo mfumo wanaotumia bado unasaidia Taifa letu kwa kipindi hiki au ulikuwa unasaidia sana kipindi kile cha ujamaa na mfumo wa chama kimoja?.
 
Mtoa taarifa andiko lako limejaa hisia za uchama kuliko fact, hujaeleza wamesaidiaje na maeneo gani?
We jamaa, hujaelewa wapi mbona umepewa mfano ijapo yanayofanyika ya kutia aibu ni mengi wanayoyafahamu lakini hawachukui hatua!.

Haya nikuongezee issue nyingine ya account ya escrow kama alivyo kili Mhe Ben Mkapa, fedha zile hawakujua kuwa zimechotwa?. Na zinachotwa si kwa maslahi ya Taifa na bali nikwaajili ya CCM na kundi dogo?.
 
Mwandishi wa taarifa hii ni mpotoshaji TISS ni taasisi yenye weledi na ina heshima kubwa duniani kwa utendaji wake uliotukuka na inaendesha shughuli zake pasipo kufungamana na upande wowote bali inatizama maslahi ya Taifa pekee.
Tueleze ilivyo saidia kuokoa bilions of money kwenye escrow account kama Ben Mkapa alivyokili?.

Acha ushabiki tu, tunahitaji TISS inayosimama na kushauri ili maslahi ya Taifa yasiharibiwe na Chama cha siasa chochote au kikundi cha watu wowote!.
 
Sawa ni mtizamo wako na tunaheshimu lakini kuna mahala katika andiko lako umeonyesha kama uko karibu na taasisi hii, sasaa kwanini hauwashauri na kuwapa mawazo yako mazuri huko? nami ni mtazamo wangu.
 
Dooooh... Watajuta kukushirikisha operation zao! By the way umewauliza sababu ya wao kuwabeba CCM? Labda wapinzani wana nia ovu na nchi kuliko CCM so huenda kuwabeba kwao ni kwa maslahi ya Taifa!
 
Inasikitisha sana pale vyombo vya kitaifa tena vizito vinapochagua kuwa kikundi ndani ya chama cha siasa
 
Hivi kama kweli kabisa unaakili timamu, huyu kiongozi anayetuongoza sasa sio adui kwa taifa letu kweli? matendo yake hayaliangamizi taifa?

Alifikaje hapo ilhali tunao hao UWT wanaojifanya wanaweza kuona adui kabla hajapewa madaraka?
 
hapo awali kabla sijawa karibu na Taasisi hii TISS nilijua na kuamini kuwa TISS ni washauri wa mambo ya kitaifa kwa maslahi ya Taifa na sio kwa maslahi ya CCM au kikundi cha watu fulani.
Wewe huwezi kuwa karibu na idara nyeti kama hii ukaja kuharisha humu
Sema upo karibu na msafisha vyoo alieajiriwa na ikulu nitakuelewa
 
Mwandishi wa taarifa hii ni mpotoshaji TISS ni taasisi yenye weledi na ina heshima kubwa duniani kwa utendaji wake uliotukuka na inaendesha shughuli zake pasipo kufungamana na upande wowote bali inatizama maslahi ya Taifa pekee.
Usitumie jina ililojijengea Zamani sasa hivi TISS mmmmh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…