Dr. Mariposa
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,264
- 10,535
Wakuu kwanza leo ndio nimejua kua nimetimiza miaka 10 jamii forum, mnipigie makofi tafadhaliiii🥳🥳🤣
Okay, nashare na ninyi hadithi hii ya kweli iliyonitokea mimi mwenyewe, hua naumia sana kila nikiwaza kwa ujinga wangu nilivyohatarisha mahusiano yangu na kuharibu maisha ya huyu binti,
Mwaka 2020, nilienda kwenye semina ya vijana juu ya uelewa wa Afya ya Akili, kulikua kuna taasisi nyingi zilialikwa ikiwemo na sisi, basi muda wa kupata chakula cha mchana nikamuona binti mmoja mrembo amekaa meza ya peke yake anakula taratiibu, akilini nikahisi anajitenga kwa hiyo nilibeba chakula changu na kuwaacha wenzangu wanaelekea kukaa meza nyingine nikaenda kukaa na yule binti, nilimsamlimia na kumuuliza kama ninaweza kukaa akanikaribisha kwa tabasamu zuri, basi tukaanza kupiga story za hapa na pale hadi tulipomaliza kula tukaagana na kila mmoja akarejea alipokaa awali, kiukweli mimi sikumtilia maanani tena,
Semina ilivyoisha wakati najiandaa kuondoka yule binti akaja mbio na kuniomba namba ya simu, nilisita kidogo akadai ana shida ya ushauri basi nikampa chap nikaondoka,
Nilivyofika home mida ya saa moja jioni sms ikaingia muhusika akajitambulisha anaitwa LILY (sio jina halisi) tulikutana kwenye semina hapo ndipo mawasiliano yalipoanza rasmi,
Nitajaribu kuifupisha maana sina kipaji cha uandishi,
Mimi na Lily tukawa marafiki sana, mimi nilimchukulia kama mdogo wangu (alikua chuo mwaka wa pili) huku yeye akitengeneza hisia za mapenzi kwangu licha ya kujua nipo kwenye mahusiano,
Siku moja akanipigia simu niende kwake alikua anaumwa sana, nakumbuka jioni baada ya kumaliza kazi nikanunua matunda na mazaga mengine nikaenda kumuona mdogo wangu mgonjwa, ilikua mara ya kwanza kufika kwake, alikua amepanga chumba master na jiko, alifurahi sana kuniona kila mara alisema hakuamini kama ningeenda, nakumbuka alivyoifakamia chocolate niliyomletea, anapenda sana chocolate, nilikaa kama masaa mawili nikaaga, akaniomba aoge kisha anisindikize japo nje tu, nikasema poa, alipotoka kuoga dah! hata sielewi ilikuaje nikajikuta namsaliti babe wangu 😭😭 pia nikanasa kwenye mtego mbaya sana ambao unanitesa hadi leo, just one mistake 🙌🏻.......
Mnisamehe siwezi kuandika yote hapa itakua ndefu sana itawaboa.
Itaendelea