Usaliti ulivyogharimu maisha ya watu niliowapenda

Usaliti ulivyogharimu maisha ya watu niliowapenda

Inaendelea, No 2

Nilivyorudi home nikawa na mixed feelings, niliumia kumsaliti mpenzi wangu lakini pia nilienjoy show ya mtoto Lily nikawaza mbona hafananii? alionekana ni binti mpole sana asiye na hatia lakini kitandani kiboko, anyway nikamcall na kumwambia kilichotokea kiishe kisijirudie tena, akaitikia kinyonge sana na maisha yakaendelea, mawasiliano yalikuwepo ila nilikua namkwepa sana tusionane,
Siku moja ofisini kwetu kukawa na event Znz, tulialika watu na yeye nikamualika so akawa ni mgeni wangu, tulivyofika Zenji tukafikia hotel ila wageni walipewa pesa cash wajichagulie wao pakulala kama mtu ana ndugu ruksa au kama watashea room ni wao tu, basi Lily akaniomba ashee room na mimi ili asave pesa yake, nilijiwazia sana ila nikaona fresh huyu ni mwanafunzi acha asave pesa itamsaidia, usiku ulikua mrefu sana kwetu uvumilivu ulinishinda nikasaliti tena mahusiano yetu, tulikaa Znz for 3 days tuliienjoy each other, tulivyorudi Dar penzi likaiva, likawa shata shata,

About my babe, yeye alikua nje ya nchi kikazi, ndani ya Mwaka tulionana mwezi mmoja au mitatu, inategemea na likizo, ni kazi ambayo kwa pamoja tuliiridhia ili tufanikishe malengo yetu, ila hii sijaiweka kama kutetea usaliti wangu, bado nilikosea, mahusiano yetu yatafikisha miaka 10 huu mwaka,

Kupeleka story mbele, baada ya mwaka mmoja wa mahusiano yetu na Lily,
Mwaka 2021 September, babe wangu alikuja for my birthday katika vitu hawezi kumiss ni birthday yangu, so tukasafiri nje ya Dar, just kuenjoy pamoja, nikampanga Lily kua babe wangu amekuja na tunasafiri asinitafute mpaka nitakaporudi hapo ndio niliamsha a monster inside her, hakuweza kuvumilia kukaa bila mawasiliano, alipiga simu na kutuma meseji nonstop, kiufupi alichanganyikiwa alisema kila giza likiingia anawaza kuna mtu mwingine ananigusa basi anapata ukichaa, usumbufu ulikua mkubwa ikabidi nimblock kila sehemu, babe wangu nilimpanga ni simu za kazi anaelewa pia aliniamini sana,
Lily alipogundua nimemblock akatumia namba nyingine kupokea alikua ni yeye analia sana, niliumia hua sipendi kuona mtu analia hata awe nani, nikamtuliza akatulia nikapanga nikirudi Dar inabidi nimmwage haraka bila hivyo ataniharibia mahusiano yangu maana hakuweza kula na kipofu....

Itaendelea
 
Back
Top Bottom