Usaliti ulivyogharimu maisha ya watu niliowapenda

Usaliti ulivyogharimu maisha ya watu niliowapenda

Acha maigizo. Astaghafulilah ya nini wakati upo bampa to bampa na story.

Lengo la mleta mada ni kuifanya jamii ivutiwe na upande aliopo, na ndio maana anajaribu kunomalize vitu
Naunga mkono hoja yako
 
Inaendelea No 3,
Nilirudi Dar na babe wangu aliondoka kurudi kazini, ndio nikapata nafasi ya kumpigia simu Lily na kumwambia tukutane kwenye mgahawa flani upo town, alifurahi sana akasema kwanini nisiende kwake amenimiss and stuff nikamwambia nope, tunahitaji kuonana pale basi jioni kweli tukakutana, alionekana mchangamfu kupita maelezo hadi nilimshangaa nikajiuliza kanywa pombe lakini hapana hua hanywi pombe basi nikajisemea labda alinimiss sana, ilikua ngumu sana kumwambia kua nataka kukatisha usaliti wangu nilizunguka sana hatimae nikampasulia ukweli, alitulia tuliiii, aliniangalia usoni kama dakika 2 hivi akacheka kidogo kisha akasema niende nyumbani atanitafuta baada ya siku 5, akaongeza kua sio akili yangu ni hiyo vacation imenichengua akili, ila nitarudi kua normal after sometimes kisha akaondoka haraka nikama hakutaka nimuone akilia, niliganda pale nikimtafakari nikaona isiwe shida nikamblock tena nikarudi home, alipiga akakuta block lakini mimi naona kua alinitafuta,
Baada ya siku 5 nikapokea simu kwenye namba ngeni akajitambulisha ni yeye na angependa twende Bagamoyo amesha arrange kila kitu, nikamjibu politely kabisa nimetingwa na kazi hadi wakati mwingine, akasema basi walau nimuone hata dakika 5 nikamwambia sina muda nikakata simu, baada ya muda mlango ukagongwa kutoka nje ni kijana anayetufanyia usafi anasema kuna mgeni wangu getini mmh nikapata wasiwasi kidogo sababu kwanza hua sileti mtu nyumbani kwangu akiwemo Lily hakuwahi kupajua kwangu, pili kwa wanaopajua hawawezi kuja bila kunipigia simu, nikamwambia kijana anisindikize, nafika nje namkuta Lily amebadilika sana, nywele zake ndefu na nzuri kazinyoa sijui kiduku sijui kijogoo, yule msichana mrembo mwenye uso usio na hatia alibadilika na kua kwenye muonekano wa kiume, alichora tattoo kubwa mkononi yenye jina langu, nilishangaa hadi nilitaka kudondoka, akavunja ukimya wa mshangao wangu kwa kunisalimia na kunitaka radhi kwa kuja bila taarifa, hapo ndio aliponizindua na kumuuliza amefikaje pale, akasema alikua anapajua maana alinifatilia siku nyingi kujua ninapoishi na mara kadhaa alifika pale bila kuniambia, kiufupi mchepuko alikua ananispy kama nachepuka dah😄
Nikamwambia aondoke haraka na asinisumbue nina kazi nyingi, wakati nataka kuondoka akanishika mkono kwa nguvu niliona moto mkali kwenye macho yake yaliyojaa hasira, nikasema kwa nguvu NIACHEEEE yule kijana akaingilia kati na kumtaka aondoke mara moja, mimi nikakimbilia ndani na kuwaacha nje, akasema nitakusubiri hapa hapa hadi utakapoamua kuondoka na mimi, geti lilifungwa na yeye alibaki nje.....

Itaendelea
Bora nimekujua leo maana kila siku maswali ya kujiuliza mwenyewe yalikuwa hayaishi, na urembo wote huu boss na huna bwana! Kumbe ndio iko hivi.
Ni mimi mlinzi wako.
 
Inaendelea No 7,

Kipenzi changu akaniuliza kwa upole kabisa, "babe, naomba ufafanuzi juu ya zile voice please" nilikua naangalia chini sikuweza kumuangalia usoni, nikawa nawaza naanzia juu au katikati?

Naomba niwape dondoo chache kuhusu mpenzi wangu, kwanza ni mpole sanaaa, mstaarabu, ana heshima kwa kila mtu, ni mtu fulani anapenda amani muda wote, hua anakasirika sometimes ila hua haweki hasira kwa muda mrefu, mimi ikitokea nimemuudhi hua haongei sana adhabu yangu naikuta kitandani 🙈,
Niseme ukweli wakati tunaanzana mwaka 2015 mimi nilikua bado barobaro yaani ujana mwingi kila sketi nataka niifunue nione yaliyomo yamoooo!? halafu sikai sana yaani tukidate mwezi mmoja wewe umekaa sana,🤫
Wakati nakutana nae yeye hakua na mambo mengi yaan exs zake walikua wawili tu, kiukweli alipambana sana kunituliza, amenizidi miaka mitano siku zote alikua ananiona mtoto ipo siku nitakua na nitaacha (na kweli nimeacha na tunalea mtoto) anavuna matunda ya uvumilivu,

Kipindi chote nipo na yeye sijawahi kuona wala kuhisi kua ananisaliti, katika vitu ambavyo ninamkubali hicho ni kimoja wapo, pia mwenzangu huyu ni mtu yupo focused sana na maisha, mpambanaji asiyekubali kushindwa kwa umri wake wa miaka 35 amefanikisha vingi ambavyo kijana yoyote angetamani kua navyo,
That's my baby sichoki kumuelezea, niko nae proud sana😘🥰

Haya turudi kwenye kikao chetu sasa, nikamfungukia japo sio story nzima nilimwambia tu nilikutana nae kwenye event ya Znz akaniomba tushee room nikamkubalia usiku ndio vile ila kulivyokucha kila mtu aliendelea na mambo yake ajabu kaniganda hadi leo wakati ilikua a one night stand, akaniuliza kwenye voice ulisema "sometimes i miss US" ulimaanisha mlichofanya kiliwakolea, hapo nikaruka nikamwambia "no babe kwanza hata sikumbuki, nilimwambia vile tu kumfanya ajisikie vizuri na sio kingine" nikaongeza "shauri lake lipo polisi alishaitwa akaonywa na sasa nataka nimpeleke tena" akashtuka kusikia habari za polisi akaniuliza ilikuaje nikaeleza matusi na vitisho alivyokua anatuma, alivyokua anaweka nguo za damu getini, alivyomtrick cuzo kupata namba yako, aisee alikasirika sana akasema sasa mimi nitadeal nae tulia, yeye atachagua aende jela au milembe hospital, akanambia nijiandae twende polisi uzuri alishawahi kukiri kwa maandishi kukaa mbali na mimi na sasa anarudia na meseji zipo, safari ya polisi ikawadia, tulisikilizwa wakasema huyu safari hii tukimuita haji, huyu ni kwenda kumkamata tu, ishu ikawa atakua wapi basi nikaambiwa nimpigie nijifanye kama nataka tuonane haraka nina shida, nilipiga sana bila kupokelewa akatuma meseji yupo darasani, nikamjibu akitoka anicheki nimechanganyikiwa nahitaji msaada wake, nahisi pindi lilikua halipandi kwani baada ya dakika 15 akanicall na kuniuliza nini mbaya, nikamwambia mambo ya kazini kuna mahesabu hayaendi sawa nikajifanya kama nalia, akaniuliza nilipo nikamuelekeza akasema anakuja chap, tukapewa askari mmoja na mgambo tukaenda hadi sehemu husika kumsubiri kweli akaja alionekana yupo so worried hapo hapo wakamkamata, nakumbuka alivyokua anapiga kelele za niacheni niacheni, alivyokua anaita jina langu na kuniuliza kwanini namfanyia vile, nilijisikia vibaya sana, nilimuomba atulie hao ni askari anaenda kituoni tu, aliendelea kupiga kelele huku akisema ananichukia, ataniua, sikuweza kupanda gari lile mimi nilichukua bajaji nakuwafata kituoni, nilikuta ameshawekwa selo lakini alikua anaongea na kupiga kelele, alikua anamtukana babe wangu, nakumbuka askari mmoja wa kike alienda akamzaba makofi na kumuamuru anyamaze ni kama alichochea moto ndio alizidi kupiga kelele, aliruka ruka alisema akitoka hapo wote atawaua na yeye atajiua, polisi walitaka familia yake ijue kua yupo pale, akaombwa namba ya mtu wake wa karibu akawa hataki kutoa anaongea vitu havieleweki, nikakumbuka kuna namba iliwahi kunicheki whatsapp huyo mtu alijitambulisha kama rafiki yake, nikaikuta na kuipiga, uzuri iliita na akapokea nikajitambulisha kwake na kumwambia Lily amekamatwa awasiliane na familia yake kituo flani waje wamtoe hayupo sawa, baada ya muda simu zikaanza kuita kwangu, alikua ni dada ake akanihoji hoji nikamwambia sina maelezo zaidi njoeni mumtoe humo na mumpeleke hospital kitengo cha magonjwa ya akili, akasema wanakuja.....

Itaendelea

Leejay49 , Lamomy , Joannah ,
ephen_ , Dejane , Demi , realMamy

Na wengine wooooooooooote
Huyu hakuwa mtu wa kawaida huyu
 
Inaendelea No 8,
Baada ya nusu saa ya kelele na matusi hatimae Lily akatulia, tukaitwa ofisi ya askari, katika maongezi akasema huyu dawa za kulevya zimemuathiri aende sober house, nikamwambia inawezekana maana anavuta sana bangi na stress na bangi haviendani, akasema kumuweka hapa ni kumuongezea tatizo anahitaji msaada wa akili, nikamwambia familia yake inakuja tafadhali waelezee hayo maana kwa alipofikia anaweza kweli akaua mtu au akajiua yeye, hata babe wangu kwa hali aliyoiona alikubaliana na sisi hakua na pingamizi,
Askari akaamuru Lily atolewe selo akaletwa kwenye ofisi tuliyokuwepo, alipotuona alituangalia kwa jicho la chuki na hasira kali akakaa na kuanza kuhojiwa akawa hajibu kitu analia tu, baadae tukajulishwa familia yake imekuja, wakaingizwa ofisini alikua dada ake mkubwa na mume wake, dada ake waliofatana kuzaliwa na shangazi yao, dada zake wakaanza kulia kumbe walikua hawajamuona siku nyingi yaan Lily tangu abadilike tabia na muonekano wake alikaa mbali na familia yake walikua wanawasiliana nae kwa simu tu, alikua amekonda, amepoteza nuru, na ile style ya nywele, zile tattoos alionekana wazi anapitia kipindi kigumu,

Askari akawaeleza kinachoendelea na akatoa wazo lake la kupelekwa sober house na mimi nikasema au hospital kitengo cha akili, Lily alikurupuka "mimi sio chiziiii, niacheni niondoke mimi sio kichaa" kila mtu akaona hapa kazi ipo,
Familia yake wakajitahidi sana kumtuliza hadi akatulia, wakamalizana na mambo ya polisi si unajua kuingia bure kutoka na cash,😀
Wakampandisha kwenye gari na kuondoka, na sie tukawashukuru maafande pale, ofcourse mkono mtupu haulambwi 😊 tukaondoka,
Ilikua ni siku ndefu na ngumu tukaimalizia beach,

Tukiwa beach nikamuomba msamaha mpenzi wangu kwa ujinga nilioufanya nilimuahidi kutulia na yaliyotokea hayatajirudia tena, akanisamehe kwa moyo mkunjufu kabisa akanambia tuangalie yajayo, tukagonga cheers 🥂

Mara nikapokea simu kutoka hospital, vipimo viko tayari niende tu donor kwa ajili ya process zinazofata, tulifurahi sana ilikua a night to remember (wakubwa mshaelewa 😋)

Itaendelea
🍷 aisee kastori katamu kanasahaulisha madeni ya vikoba 😅😅😅😝
 
Nilijua ni ke😳
Kwani hamna ke wanaotamani kufunua sketi za wenzao hasa wawe wazurii watapata taabu haswa!

Mdogo wangu mmoja wa kufikia kaja dar kwa kazi zake tuu hapa na pale.....

Mimi ni mtu mmoja mtulivu sana na mkimya hasa ninaookuwa na watu wengi ama wageni wageni.....

Yule binti akanisoma naye ndo tabia kama zangu japo jinsia tofaut

Tulivyo zoeana akaniuliza siku moja ety Tomboy ndo nn ? Mimi nilicheka sana nikamuuliza umekutana na nni? Akawa kama kapanic

Nikamtuliza then nikamjibu ni mwanamke mwenye swaga za kiume nni oyaah oyaah kma zote!

Ndo akaniambia Jana Kuna mdada wakati yupo restaurant kamfata ..... anamwambia ni mzurii, kamwelewa sjui hivi mara vile....

Nikamwambia kaa mbali naye..... Huyo atakuwa lesb nikampa darasa maake dogo hata style zetu za chuma mboga ukiongea anaona msamiati mpya

Japo katoka bush she's cute aseeh,, white, tall medium, ana hips flani... Hivo mzee
 
Izi ishu za kusagana sio jambo geni kabisa huku kitaa especially kwa hawa dada zetu wa kaskazini ni kitu cha kawaida sana na sasaiv idadi yao ni kubwa sana.

%kubwa ya wadada wanaoitana "Babe" "my other half" sweet nininini sijui kwenye simu au wanaolala kitanda kimoja hususan hostel au huku mtaani ni wanasagana💯 na ni kitu ambacho nishafanyia utafiti na nikahitimisha way long ago.

Leta maneno Dr. Mariposa
 
Back
Top Bottom