Usaliti wanaopitia Ukraine na Ulaya kutoka kwa Marekani, kihistoria ni kawaida ya Marekani. Sio taifa la kuliamini kwa 100% Tujikumbushe kidogo

Xi Jinping

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2023
Posts
3,651
Reaction score
11,548
Jinsi ambavyo ghafla Marekani imembadilikia Ukraine na kutafuta suluhu na Russia hii inatukumbusha matukio matatu makubwa jinsi Marekani anavyoweza kubadilika kama kinyonga na kutokuunga mkono.
  • Kabla ya WW2 Marekani ilikuwa ikiunga mkono Ujerumani.​
  • Wakati wa WW2, Marekani iliunga mkono USSR dhidi ya Ujerumani (NAZI)​
  • Baada ya WW2 Marekani iliwaunga mkono NAZI (Ujerumani) dhidi ya USSR wakati wa Cold War.​

Nobody does switcheroo better than USA!

Wakati wa mkutano wa wanachama wa NATO uliofanyika Brussels, Belgium, waziri wa ulinzi wa Marekani aliwaacha kwenye mataa Ukraine na mataifa ya Ulaya.

Alisema kuwa Marekani haitatoa msaada kwa Ukraine na kutaka NATO isipeleke misaada bali taifa mojamoja la Ulaya likiamua kuisaidia Ukraine sawa tena kwa gharama ya taifa hilo husika.

Kwa kifupi hapa Marekani aliwasaliti wenzake ukiangalia kwa miaka 3 alikuwa nao sambamba tena yeye akiwa mstari wa mbele.

Wakati wanamalizia mkutano huo waziri huyo wa ulinzi alisema sasa wanafocus Indo-Pacific ili kuzuia ushawishi wa China.

"Pia tunakabiliwa na mshindani China anayeweza kutishia Marekani na maslahi ya Marekani katika eneo la Indo-Pacific. Marekani imekuwa ikibadilisha vipaumbele vyake vya kijeshi kwa kulinda nchi yake na kuizuia China."
– Pete Hegseth (Waziri wa ulinzi wa Marekani)​

Na kama tujuavyo lazima Marekani itayatumia mataifa kama Japan, India, S.K, Australia, Philippines n.k

Ikiwa dhumuni hilo litashindwa na uhakika ni lazima litashindwa usishangae Marekani ikawa Pro-China.

Hii historia ya kabla, wakati na baada ya WW2 na hili la Ukraine ni mifano michache kati ya mingi ya kutolitumaini taifa la Marekani kama mshirika.

Atakuwa nawe kwa sasa kwa interest zake akishakutumia anakutema kama chewing gum au fundo la muwa lililoisha utamu wake.

Hii inapaswa iwe funzo kwa mataifa mengine duniani au yale yatakayotumika na Marekani dhidi ya China eneo la Indo-Pacific.

Kwa kifupi:

"America has no permanent friends or enemies, only interests.”
Henry Kissinger (Former U.S Secretary of State)
 
Inaonyesha kwamba marais wa marekani wana nguvu kuliko mipango ya muda mrefu ya nchi au dira ya nchi. Kwamba kila rais anaweza kubadili gea angani au kubadilisha dira ya nchi kulingana na misimamo yake au sera zake binafsi. Hii inafanana kabisa na magufuli style ya uongozi
 
Wakati wa mkutano wa wanachama wa NATO uliofanyika Ujerumani, waziri wa ulinzi wa Marekani aliwaacha kwenye mataa Ukraine na mataifa ya Ulaya.

Alisema kuwa Marekani haitatoa msaada kwa Ukraine na kutaka NATO isipeleke misaada bali taifa mojamoja la Ulaya likiamua kuisaidia Ukraine sawa tena kwa gharama ya taifa hilo husika.

Kwa kifupi hapa Marekani aliwasaliti wenzake ukiangalia kwa miaka 3 alikuwa nao sambamba tena yeye akiwa mstari wa mbele.

Wakati wanamalizia mkutano huo waziri huyo wa ulinzi alisema sasa wanafocus Indo-Pacific ili kuzuia ushawishi wa China.

"Pia tunakabiliwa na mshindani China anayeweza kutishia Marekani na maslahi ya Marekani katika eneo la Indo-Pacific. Marekani imekuwa ikibadilisha vipaumbele vyake vya kijeshi kwa kulinda nchi yake na kuizuia China."
– Pete Hegseth (Waziri wa ulinzi wa Marekani)​

Na kama tujuavyo lazima Marekani itayatumia mataifa kama Japan, India, S.K, Australia, Philippines n.k

Ikiwa dhumuni hilo litashindwa na uhakika ni lazima litashindwa usishangae Marekani ikawa Pro-China.

Hii historia ya kabla, wakati na baada ya WW2 na hili la Ukraine ni mifano michache kati ya mingi ya kutolitumaini taifa la Marekani kama mshirika.

Atakuwa nawe kwa sasa kwa interest zake akishakutumia anakutema kama chewing gum au fundo la muwa lililoisha utamu wake.

Hii inapaswa iwe funzo kwa mataifa mengine duniani au yale yatakayotumika na Marekani dhidi ya China eneo la Indo-Pacific.

Kwa kifupi:

"America has no permanent friends or enemies, only interests.”
Henry Kissinger (Former U.S Secretary of State)
Bwanamdogo elewa sera ya Marekani, "hawana adui wa kudumu wala rafiki wa kudumu" wenzako wana akili siyo hizi blablaah zako
 
Inaonyesha kwamba marais wa marekani wana nguvu kuliko mipango ya muda mrefu ya nchi au dira ya nchi. Kwamba kila rais anaweza kubadili gea angani au kubadilisha dira ya nchi kulingana na misimamo yake au sera zake binafsi. Hii inafanana kabisa na magufuli style ya uongozi
Huku bongo huwa wanaimba kuwa usa eti ana mifumo imara .. il kiukweli rais wa usa ana nguvu na ni kama mungu mtu .. sehem ambayo huwa hawapagusi ni pale israel maana ni kama hekalu lao
 
Madikteta wakubwa wa dunia hao lakini wanajifanya wanahimiza demokrasia uchwara kwa nchi nyingine za duniani kwa maslahi yao binafsi
 
Inaonyesha kwamba marais wa marekani wana nguvu kuliko mipango ya muda mrefu ya nchi au dira ya nchi. Kwamba kila rais anaweza kubadili gea angani au kubadilisha dira ya nchi kulingana na misimamo yake au sera zake binafsi. Hii inafanana kabisa na magufuli style ya uongozi
Ndani ya Marekani mabadiliko huja hasa ikiwa chama kilichotoka madarakani ni tofauti na kinachoingia madarakani

Pili kimataifa wanabadilika ikitegemea interests ya taifa lao kwa wakati huo ikitegemea sera ya chama tawala

Kimataifa iwe ni Dems au Reps wote sera ya taifa ni kulinda U.S global hegemony ila wanatofautiana tu kwenye approaches
 
Inaonyesha kwamba marais wa marekani wana nguvu kuliko mipango ya muda mrefu ya nchi au dira ya nchi. Kwamba kila rais anaweza kubadili gea angani au kubadilisha dira ya nchi kulingana na misimamo yake au sera zake binafsi. Hii inafanana kabisa na magufuli style ya uongozi
Lkn uzuri wa USA,chama chochote kikishika madaraka sera yao ni moja (USA kwanza), wanatofautiana tu namna yautekelezaji wa hizo sera, mfano mmoja atatumia diplomasia,lkn mwingine aweza tumia diplomasia kidogo na nguvu zaidi.
 
Madikteta wakubwa wa dunia hao lakini wanajifanya wanahimiza demokrasia uchwara kwa nchi nyingine za duniani kwa maslahi yao binafsi
Uko sahihi

Baada ya kuona harakati za CIA za kufanya mapinduzi zinajulikana wakaanzisha taasisi zao zikijifanya zinatetea democracy.

Bajeti zao zinapewa support na The Fed kupita bunge la Marekani

  • NED (National Endowment for Democracy)
  • IRI (International Republican Institute)
  • NDI (National Democratic Institute)
  • CIPE (Center for International Private Enterprise)
  • USAID

Hizi taasisi zinafanya kazi bega kwa bega na CIA

Kama NED imechangia sana mapinduzi ya kiutawala katika mataifa mbalimbali kwa kusambaza propaganda dhidi ya tawala ambazo Marekani hawazitaki, wanajifanya kuwatrain vijana kumbe wanawaandaa kwa mapinduzi ambayo Marekani anataka kuweka vibaraka wake.

Mfano wa karibuni walipofaulu ni Bangladesh, ila Venezuela walichemka

Hizi taasisi na kazi wanazofanya kwa niaba ya CIA na Marekani kwa siri

Mataifa yanayojielewa waliyafukuza hayo mashirika kitambo sana kwenye mataifa yao
 
Madikteta wakubwa wa dunia hao lakini wanajifanya wanahimiza demokrasia uchwara kwa nchi nyingine za duniani kwa maslahi yao binafsi
Ukikuta sehem anahimiza demokrasia basi aliekalia kiti kwenye hio nchi anaminya maslahi yao,,,....ila hata akikaa dikteta ila anasimamia maslahi yao hutaona wanapiga kelele za demokrasia kwenye hio nchi
 
Ukiangalia walivyopigana na Vietnam na kuua watu wengi huku wakitumia sumu iitwayo 'agent orange ' kuharibu misitu na mazingira yake, leo aaongoza kwa uwekezaji nchini humo.
Japan ilitandikwa na Marekani mabomu ya atomic mwishoni mwa WW2 katika miji ya Nagasaki na Hiroshima

Leo hii Japan ni taifa ambalo linaongoza kuwa na American troops na U.S military bases duniani. Japan military command yao inategemea Marekani hii ni aibu kubwa

Miaka ya 1980 wakati Japan inapanda kwa kasi kuchumi na kiteknolojia kutaka kuizidi Marekani, ikapigwa na Marekani mkataba ulioitwa Plaza Accord na bidhaa za Japan zikazuiwa kuingia Marekani. Japan ikashushwa!

Cha ajabu leo Japan trade partner wake mkubwa ni Marekani

Marekani inapenda sana mataifa kama Japan ambayo yanakubali kuburuzwa na Marekani
 
Na sisi chawa wa Marekani na Europa tunalo la kujifunza
Moja ya chawa aliyeanza kujifunza ni huyu mpambanaji anayejiita HIMARS

Screenshot_20250224-134729.jpg
 
Sawa. Tuwaamini urusi na china walioshindwa kumtetea kibaraka wao Assad pale Syria
 
Japan ilitandikwa na Marekani mabomu ya atomic mwishoni mwa WW2 katika miji ya Nagasaki na Hiroshima

Leo hii Japan ni taifa ambalo linaongoza kuwa na American troops na U.S military bases duniani. Japan military command yao inategeme Marekani hii ni aibu kubwa

Miaka ya 1980 wakati Japan inapanda kwa kasi kuchumi na kiteknolojia kutaka kuizidi Marekani, ikapigwa na Marekani mkataba ulioitwa Plaza Accord na bidhaa za Japan zikazuiwa kuingia Marekani ikashushwa!

Cha ajabu leo Japan trade partner wake mkubwa ni Marekani

Marekani inapenda sana mataifa kama Japan ambayo yanakubali kuburuzwa na Marekani
Japan is an occupied state
 
Jinsi ambavyo ghafla Marekani imembadilikia Ukraine na kutafuta suluhu na Russia hii inatukumbusha matukio matatu makubwa jinsi Marekani anavyoweza kubadilika kama kinyonga na kutokuunga mkono.
  • Kabla ya WW2 Marekani ilikuwa ikiunga mkono Ujerumani.​
  • Wakati wa WW2, Marekani iliunga mkono USSR dhidi ya Ujerumani (NAZI)​
  • Baada ya WW2 Marekani iliwaunga mkono NAZI (Ujerumani) dhidi ya USSR wakati wa Cold War.​

Nobody does switcheroo better than USA!

Wakati wa mkutano wa wanachama wa NATO uliofanyika Brussels, Belgium, waziri wa ulinzi wa Marekani aliwaacha kwenye mataa Ukraine na mataifa ya Ulaya.

Alisema kuwa Marekani haitatoa msaada kwa Ukraine na kutaka NATO isipeleke misaada bali taifa mojamoja la Ulaya likiamua kuisaidia Ukraine sawa tena kwa gharama ya taifa hilo husika.

Kwa kifupi hapa Marekani aliwasaliti wenzake ukiangalia kwa miaka 3 alikuwa nao sambamba tena yeye akiwa mstari wa mbele.

Wakati wanamalizia mkutano huo waziri huyo wa ulinzi alisema sasa wanafocus Indo-Pacific ili kuzuia ushawishi wa China.

"Pia tunakabiliwa na mshindani China anayeweza kutishia Marekani na maslahi ya Marekani katika eneo la Indo-Pacific. Marekani imekuwa ikibadilisha vipaumbele vyake vya kijeshi kwa kulinda nchi yake na kuizuia China."
– Pete Hegseth (Waziri wa ulinzi wa Marekani)​

Na kama tujuavyo lazima Marekani itayatumia mataifa kama Japan, India, S.K, Australia, Philippines n.k

Ikiwa dhumuni hilo litashindwa na uhakika ni lazima litashindwa usishangae Marekani ikawa Pro-China.

Hii historia ya kabla, wakati na baada ya WW2 na hili la Ukraine ni mifano michache kati ya mingi ya kutolitumaini taifa la Marekani kama mshirika.

Atakuwa nawe kwa sasa kwa interest zake akishakutumia anakutema kama chewing gum au fundo la muwa lililoisha utamu wake.

Hii inapaswa iwe funzo kwa mataifa mengine duniani au yale yatakayotumika na Marekani dhidi ya China eneo la Indo-Pacific.

Kwa kifupi:

"America has no permanent friends or enemies, only interests.”
Henry Kissinger (Former U.S Secretary of State)
Seems like USA know snitching code better than anyone
 
Back
Top Bottom