Jinsi ambavyo ghafla Marekani imembadilikia Ukraine na kutafuta suluhu na Russia hii inatukumbusha matukio matatu makubwa jinsi Marekani anavyoweza kubadilika kama kinyonga na kutokuunga mkono.
Kabla ya WW2 Marekani ilikuwa ikiunga mkono Ujerumani.
Wakati wa WW2, Marekani iliunga mkono USSR dhidi ya Ujerumani (NAZI)
Baada ya WW2 Marekani iliwaunga mkono NAZI (Ujerumani) dhidi ya USSR wakati wa Cold War.
Nobody does switcheroo better than USA!
Wakati wa mkutano wa wanachama wa NATO uliofanyika Brussels, Belgium, waziri wa ulinzi wa Marekani aliwaacha kwenye mataa Ukraine na mataifa ya Ulaya.
Alisema kuwa Marekani haitatoa msaada kwa Ukraine na kutaka NATO isipeleke misaada bali taifa mojamoja la Ulaya likiamua kuisaidia Ukraine sawa tena kwa gharama ya taifa hilo husika.
Kwa kifupi hapa Marekani aliwasaliti wenzake ukiangalia kwa miaka 3 alikuwa nao sambamba tena yeye akiwa mstari wa mbele.
Wakati wanamalizia mkutano huo waziri huyo wa ulinzi alisema sasa wanafocus Indo-Pacific ili kuzuia ushawishi wa China.
"Pia tunakabiliwa na mshindani China anayeweza kutishia Marekani na maslahi ya Marekani katika eneo la Indo-Pacific. Marekani imekuwa ikibadilisha vipaumbele vyake vya kijeshi kwa kulinda nchi yake na kuizuia China."
– Pete Hegseth (Waziri wa ulinzi wa Marekani)
Na kama tujuavyo lazima Marekani itayatumia mataifa kama Japan, India, S.K, Australia, Philippines n.k
Ikiwa dhumuni hilo litashindwa na uhakika ni lazima litashindwa usishangae Marekani ikawa Pro-China.
Hii historia ya kabla, wakati na baada ya WW2 na hili la Ukraine ni mifano michache kati ya mingi ya kutolitumaini taifa la Marekani kama mshirika.
Atakuwa nawe kwa sasa kwa interest zake akishakutumia anakutema kama chewing gum au fundo la muwa lililoisha utamu wake.
Hii inapaswa iwe funzo kwa mataifa mengine duniani au yale yatakayotumika na Marekani dhidi ya China eneo la Indo-Pacific.
Kwa kifupi:
"America has no permanent friends or enemies, only interests.”
– Henry Kissinger (Former U.S Secretary of State)