Youngblood
JF-Expert Member
- Aug 1, 2014
- 19,433
- 56,810
SanaP Funk alikuwa mbele ya muda sana.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
SanaP Funk alikuwa mbele ya muda sana.
Utasikia Mahaba niueHuu wimbo uliachiliwa Mwaka 2001, katika albam yake ya Machozi, Jasho na Damu.
Nitachambua na kuunganisha na Matukio ya sasa ambayo enzi hizo yalikuwepo ila baadhi ya watu wanayafanya kama ni mambo mapya... na uzuri huyu PROFESA Alichimba ndani sana..
1- Ushoga
2- Umalaya na Kuuza Miili
3- Tabia za watanzania za kuponda starehe pale akipata vihela
na Mambo mengine mengi..
Twende nami..
" Subiri kichapo chake pale mbongo anapozipata
Mwendo wa kiti kirefu jirani na nyama choma
Na toto mbili tatu za geti au za kona"
Huu utaratibu bado tunaendelea nao mpaka hii leo watu wanaenda ktk maeneo ya starehe huku wamezungukwa na wachumba kwenye meza wakitusua manyama na unywaji wa pombe za kutosha..
neno Toto mbili tatu za geti au za KONA... nafkiri biahsara ya uuzaji Utamu maeneo ya Sinza pale Kona Bar ni wa muda mrefu miaka 22+
"Pitia pitia night kali mitaa ya Kinondoni
Kina dada poa nusu uchi fegi mdomoni
Na kama una gari watajazana madirishani wee
Mpaka ukose hewa wote wanataka hisani"
Hapa tunaona Biashara ya uuzaji miili ndani ya DSM ni ya kitambo, hivyo yale malalamiko ya mara kwa mara humu kanakwamba ni jambo jipyaa mie nafkiri baadhi ya watu (Wakuja/Wamikoani) hivi vitu kwao ni vipya.
"Mpaka bibi vizee sasa wanafanya ukahaba"
Mnajionea wenyewe PROFESA anazidi kutuhabarisha ndani ya mwaka huo 2001 mabibi pia walikuwa wanauza miili...
"Vijana wamejibana wapate mtaji wa biashara
Nawaita machinga ingawa sio wote kutoka Mtwara
Mbaya kuliko vyote mnapovunja vibanda vyao
Wengine walikuwa wezi, je warudie zama zao?"
Hapa aligusa jamii.. hasa ya wafanya biashara kuhusu vita yao na serikali.. hi vita ni ya miaka nenda rudi.
"Wabongo wanapenda sana starehe kuliko kazi
Wanatamani wangezaliwa Blue Nay wamwage radhi"
Nyuzi nyingi hata humu JF zinahusiana na Mapenzi na Ngono pamoja na starehe zingine hii inasadiki na ni tabia ya WABONGO mpaka hii leo huu utaratibu wa kupenda starehe upo.
"Mablaza majina yao ya asili hawayataki
Bitoz Nyangema anataka aitwe Tupac!"
Wacha tufanye utafiti wa Majina ya members humu jee wana majina ya Asili? hii ni tabia ya kitambo sana tunaona hapo baadae kizazi hiki kinachokuja hakitakuwa na majina ya Asili tena.
"Funga mkanda, fungua mabano unavyotaka"
anayejua maana ya hii vesi anijulishe........!
"Sinza ya leo, kila baada ya nyumba bar
Na zote zinajaa, hapo ndipo utakaposhangaa
Na kwenye night club ni lundo la kaka poa
Huwezi ukaamini jinsi walivyojipodoa"
Kama mnavyoona hapo ishu ya USHOGA ipo na ilikuwepo ingawa sahivi watu wanaipa sana airtime kama vile ni jambo jipya ktk jamii.. kuna nyuzi za kuigusia SINZA za hivi karibuni watu wanaijadili Sinza kama ni sehemu iliyoharibika hivi karibuni.. kumbe ndio sehemu iliyochachuka miaka na miaka.... ni ASILI ya hilo eneo.
"Na watu wana magari mpaka ya milioni 200"
Hapa watu wanashangaa Mhe MSUKUMA kuvuta chuma cha mil 400+ hali ya kuwa mwaka 2001 huko watu walimiliki vyuma vya mil 200.. unaweza kufikiri ni jinsi gani watu walikuwa na hela ukizingatia mfumo wa ujamaa ulikuwa bado una vimizizi kipindi hicho.
Huyu Jamaa PROF JAY ni kichwa.. na ni msanii mbunifu na mwenye uwezo mkubwa wa uandishi na kupangilia ngoma ambazo zitaishi miaka mingi. huu wimbo ni kama umetoka mwaka jana.
JIONI NJEMA....
Ilikuwa album ya machozi jasho na damuHata beat lake kali sijui alitengeneza nani
una akili nukta.Kawaida sana
Halafu sasa vipindi vya hip hop watu wanacheza Ngoma za Wakazi upuuzi mtupubIlikuwa album ya machozi jasho na damu
Ilikuwa album kali sana ikibeba wimbo kama.
1. Jina langu hii ngoma pia kali sana.
2.Ndio mzee.
Jay wa mitulinga.. anabalaa lake.Hakuna msanii nchi hii mwenye kumfikia Prof katika utunzi japo wasanii wa zamani walikuwa wanajua sana kutunga nyimbo zinazoishi.
1. Bongo Dar es Salaam
2. Niamini
3. Joseph
4. Elimu mitaani Dknob
5. Mtazamo
6. Starehe
Hizi nyimbo ni hit songs mpaka leo
Serious... ni nyimbo chache sana za wasanii wanaotunga vitu vikaendelea kuishi.Hii ngoma inaenda na uhalisia naiona hata miaka 10 ijayo wakati imeimbwa mm nipo shule ya msingi mpk leo nina miaka Zaidi ya thelathini duu hili jamaa ni genious hakuna msanii anaemfikia kwa kutunga mashairi yalikyokuwa mbele ya muda 😁 😁
Ndio Mzee kali sana nakumbuka ilitoka remix ya Sio MzeeIlikuwa album ya machozi jasho na damu
Ilikuwa album kali sana ikibeba wimbo kama.
1. Jina langu hii ngoma pia kali sana.
2.Ndio mzee.
Mnooo.. Jamaa anajuakiukweli sina la kusema kuhusu profesa jay yaani huyu jamaa ni zaidi ya msanii akili kubwa sana
Mnooo... ila nyimbo bado ipo hot..Ni zaman sana
Na mambo ni yale yale bado yapo ujumbe unaishi 💯Mnooo... ila nyimbo bado ipo hot..
Mie ni kijana nafkir hii nyimbo inatoka nilikuwa chini ya miaka 5.
- Prof. Jay!! The Living Legend! Je huyu mwamba anaendeleaje?
- Natamani kusikia anahojiwa hewani. Nimeacha kusikia redio za FM kwa wanaongea 'm.avi'
- Dah! Kila zama na zama zake.
- Tuliokuwa vijana zama hizo, kwa sasa hata sijui mnaowaita wasanii wanachoimba. Mbaya zaidi nyimbo za rika letu hazipo
hapa nasikiliza nipoze moyo mama daah huyu jamaa ni mwishoTuwaambie Vijana kutoka Mikoani wakija Mjini DSM wakae kwa kutulia
Kula chuma hicho.hapa nasikiliza nipoze moyo mama daah huyu jamaa ni mwisho
SaluteLYRICS
Yoh, yoh, yoh
Ndani ya Bongo mambo super hapana ubongo
Ingawa sometime Bongo chungu kama sifongo
Nafanya makaratee kama machinga mtaa wa Congo
Kimtindo mtindo nakata ngebe vimtima nyongo
Hapana matata kitu roho inapenda mtapata
Bongo Dar Es Salaama ni mpeto wa kutakata
Nenda viwanja vikali vya Bongo ustaajabu
Na pita Sleepway, Blue Pam au Mambo Club
Kama hujazoea unaweza ukavunja shingo
Mambo Isidingo watu mkononi Nokia bingo
Huwezi kujua yupi mtoto wa geti, yupi changu
Wote wanameremeta kama mamtoni mwanangu
Hizi zinapoyeyuka wabongo tunalia ukata
Subiri kichapo chake pale mbongo anapozipata
Mwendo wa kiti kirefu jirani na nyama choma
Na toto mbili tatu za geti au za kona
Hii watu wa Bongo tunasema napoteza mawazo
Lakini mara nyingi hutokea wakati unazo
Wakati wa dumba kali saa moja shuka utosini
Na kujifanya unawaza mambo mengi ya ofisini
Pitia pitia night kali mitaa ya Kinondoni
Kina dada poa nusu uchi fegi mdomoni
Na kama una gari watajazana madirishani wee
Mpaka ukose hewa wote wanataka hisani
Kwenye madaladala kuibiwa ni kawaida
Vaa cheni shingoni, saa mkononi utoe faida
Wacha dirisha wazi kisha ukatize Manzese
Ili uwape mateja mtaji waende chimbo wakatese
Rudi Mwananyamala oh! Mateja kibao
Katiza saa moja moja uone roba za mbao
Utaona kama mtoa roho yuko karibu yako
Ni kheri utoe chochote ili uokoe nafsi yako
Bongo eh
Bongo Dares Salaam
Utalia lia lia lia
Bongo Dares Salaam
Kaa chonjo eh
Ndani ya Dares Salaam
Utalia lia lia lia
Ndani ya Dares Salaam
Bongo ya sasa sio ya mwaka 47
Mpaka bibi vizee sasa wanafanya ukahaba
Sijui niseme nini ili muweze kunielewa
Na sijui nifanye nini nisaidie wanaoonewa
Hakuna heshima, ni vurugu mechi kwenye jamii
Hakuna utii wala mafunzo ya manabii
Na wezi wa mfukoni wanachomwa moto kinyama
Mwingine hajaiba kapewa kesi kwa uhasama
Nani atakae jua na sheria ipo mikononi?!
Watu wa Bongo mbona hamna utu moyoni
Vijana wamejibana wapate mtaji wa biashara
Nawaita machinga ingawa sio wote kutoka Mtwara
Mbaya kuliko vyote mnapovunja vibanda vyao
Wengine walikuwa wezi, je warudie zama zao?
Ni mshike mshike sometime ni vita na mapolisi
Wao na sisi, rungu na pingu kama ibilisi
Huku kwetu uswahilini ni mambo ya kila siku
Na ni kama kuibiwa cheni kwenye ngoma za mchiriku
Wabongo wanapenda sana starehe kuliko kazi
Wanatamani wangezaliwa Blue Nay wamwage radhi
Masista duu wa Bongo wanazidi kupanda chati
Huwezi kujua yupi wa Kigogo, yupi wa Masaki
Mablaza majina yao ya asili hawayataki
Bitoz Nyangema anataka aitwe Tupac!
Ni burudani tosha, hivyo ni vijimambo tu
Wabongo tuna title kubwa lakini hatuna kitu
Unaujua mstakabari wa ma-superstar wa Bongo?
Lazma ufunzwe chuo kikuu cha mbwembwe za uongo
City center, ofisi ni mtu aliposimama
Hata muhuri wa ikulu unapata haina gharama
Ngoma inakuwa nzito mnapokutana matapeli
Akili kumkito ukilemaa umeachwa ferry
Aliyeuziwa cheni katoa hela bandia
Aliyepokea hela nae kauza cheni ya bandia
Tuliozoea jiji tunasema ngoma droo
Na una-set mambo mengine yaende kwenye mtandao
Bongo eh
Bongo Dares Salaam
Utalia lia lia lia
Bongo Dares Salaam
Kaa chonjo eh
Ndani ya Dares Salaam
Utalia lia lia lia
Ndani ya Dares Salaam
Katikati ya jiji hata usikiri dili haziji
Na ukitaka ku-win Bongo cheza dili na wale magwiji
Naona vijana wa Bongo wanapenda safari kafiri
Hata mkoba wanategua kitendawili
Safari bado ni ngumu jamani msiende kwa nguvu ya ndumba
Ujinga sumu acha Mwenyezi awahukumu
Changa uchange uende kiwanja unachotaka
Funga mkanda, fungua mabano unavyotaka
Maskani Kimara, watu kila siku magoni
Jonas Kiwia wasalimie Washington
Ukiweza pita Texas mpe hi Chief Son
Na mkumbushe uzushi wa Bongo Dar es Salaam
Sinza ya leo, kila baada ya nyumba bar
Na zote zinajaa, hapo ndipo utakaposhangaa
Na kwenye night club ni lundo la kaka poa
Huwezi ukaamini jinsi walivyojipodoa
Upinzani wa jadi Bongo haupo Simba na Yanga
Matonya na Makamba, na Sitte na wamachinga
Na kali kuliko zote upinzani konda na denti
Wanaposhika mashati tu denti anapoketi
Hakuna mnyonge, wala anayekubali kushindwa
Ngoma ngoroigwa na wote wanataka ubingwa
Na watu wana magari mpaka ya milioni 200
Kwa mbongo wa kawaida baiskeli kitendawili
Wasioamini ni wale wenzangu na mimi
Mlio na imani iliyopo juu mngoje chini
Mtangoja milele, na mtakufa bila kelele
Kama walivyokufa wafuasi wa Kibwetele
Ndani ya Bongo!
Bongo eh
Bongo Dares Salaam
Utalia lia lia lia
Bongo Dares Salaam
Kaa chonjo eh
Ndani ya Dares Salaam
Utalia lia lia lia
Ndani ya Dares Salaam
Bongo eh
Bongo Dares Salaam
Utalia lia lia lia
Bongo Dares Salaam
Kaa chonjo eh
Ndani ya Dares Salaam
Utalia lia lia lia
Ndani ya Dares Salaam