Ushabiki wa timu oyaoya bila kadi unakera sana

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Ushindi wa timu yako unanoga na kufurahisha sana kama ukiwa mwanachama hai. Iko siku wanachama hai watapata gawio la fedha mbali na lile gawio la sasa la furaha viwanjani. Mpira ni pesa twendeni tukakate kadi za timu zetu ili nasi tuwe sehemu kamili ya uendeshaji wa timu zetu. Ukiwa mwanachama hai hata dua zako zitakubaliwa.

Ushabiki oyaoya tu kwenye luninga ni janga kwa timu yako.
 
Sijui kwanini huwa inaniwia vigumu kuchukua kadi ya uwanachama.

Nimejiwekea utaratibu wa kununua jezi mpya kila msimu na kila shindano, kwenda uwanjani mara nyingi kama njia ya kuisapoti timu yangu Yanga.
 
Waambieni hao viongozi waanzishe card za kidigital. Sio lazima inayoshikika. Watu wana smartphone siku hizi
 
Wanachama hai ndo mnachagua viongozi wa hovyo....viongozi wabishi Kama mishipa
Sijui kwanini huwa inaniwia vigumu kuchukua kadi ya uwanachama.

Nimejiwekea utaratibu wa kununua jezi mpya kila msimu na kila shindano, kwenda uwanjani mara nyingi kama njia ya kuisapoti timu yangu Yanga.
Hakutakuwa na gawio kwa wanachama kwa siku hizi za karibuni, Nadhani kwa sasa lazima kuwe na vivutio (incentives) vinavyotofautisha kati ya mwanachama na asiyekuwa mwanachama kwenye viingilio, ununuzi wa jezi, vifaa vya timu mbali na kushiriki kwenye chaguzi za viongozi. Kama jezi inauzwa 50,000 mwanachamahai aipate kwa 40,000 au 45,000.
 
Kama mwanachama hatakua na limit ya idadi ya jersey za kununua, anaweza kumnunulia huyu asie mwanachama.
 
Sijui kwanini huwa inaniwia vigumu kuchukua kadi ya uwanachama.

Nimejiwekea utaratibu wa kununua jezi mpya kila msimu na kila shindano, kwenda uwanjani mara nyingi kama njia ya kuisapoti timu yangu Yanga.
Jitahidi kuwa shabiki muwajibikaji sio mlalamikaji
Chikua kadi yako ya yanga mRemBo
 
Back
Top Bottom