Ushahidi: Delila hakumnyoa Samsoni bali alisingiziwa

Ushahidi: Delila hakumnyoa Samsoni bali alisingiziwa

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
Samsoni hakunyolewa na Delila bali Delila amekaa kusingiziwa
FB_IMG_16392581377299843.jpg

Imekuwa ikienea kuwa mwanamke kwa jina la Delila ndiye alimunyoa Samsoni kitu ambacho si kweli. Wengi hufikiri kuwa Samsoni alinyolewa na Delila.

Ushahidi unaonyesha katika biblia takatifu Delila yeye alihusika katika kumdanganya Samsoni na kujua siri zilizo zificha katika Nywele zake na Delila yeye alihusika pia wakati Samsoni ananyolewa lakini Delila binafsi yeye hakumunyoa Samsoni kitu ambacho Delila amekaa kusingiziwa.

Ushahidi katika biblia ukisoma Waamuzi 16:19
Imeandikwa "Waamuzi 16:19
[19]Naye akamlaza usingizi magotini pake. Kisha akamwita mtu akavinyoa vile vishungi saba vya nywele za kichwa chake; akaanza kumsumbua, nguvu zake zikamtoka.


Hivyo ukirejea ushahidi wa biblia Samsoni alinyolewa na mtu mwingine ambaye hakutajwa na wakati huo Samsoni alikuwa magotini mwa Delila.
 
Bado Delila ni mtuhumiwa namba 1.

Mashtaka ya Delila:
1.Kula njama za kumnyoa Samson
2.Kumlewesha Samson kwa nia ovu ya kumnyoa nywele zake.
3.Kushiriki kumnyoa samson.
4.Kutakatisha pesa(pesa alizolipwa baada kutekeleza huu uhalifu)
5.Uhujumu uchumi
6.Ukahaba
 
Mkuu namba 4 hakuna uhakika kama alifanya hivyo.
Bado Delila ni mtuhumiwa namba 1.

Mashtaka ya Delila:
1.Kula njama za kumnyoa Samson
2.Kumlewesha Samson kwa nia ovu ya kumnyoa nywele zake.
3.Kushiriki kumnyoa samson.
4.Kutakatisha pesa(pesa alizolipwa baada kutekeleza huu uhalifu)
 
Akawaambia akinyolewa nywele nguvu zote zitakwisha (anashiriki hapo). Delila atabaki kuwa mtuhumiwa namba moja ksbb pekee ndie alieuza siri ya nguvu za Samson kuwa kwenye nywele. Akamlewesha na kilevi ili alale na anyolewe (dhamira ovu ya Delila ikatimia)
 
katika kesi hii naomba nikutane na kibatala,yeye akae kwa delila namgaragaza robo saa baada ya shauri kuanza kusikilizwa.View attachment 2040235
Waendesha mashitaka:Wkt wa Operation ukuta mshitakiwa alisema watashikisha ukuta police mwaka huu.

Mahakama:Ni Kweli mshitakiwa ulisema?

Mshitakiwa:Ni Kweli nilisema.

Wakili wa mshitakiwa:Mh. Hakimu naomba police atusaidie kushika ukuta hapa mahakamani tuone Kama Ni vibaya.

Police akashika ukuta.

Hakimu😛olice ameshika ukuta na hakuna Baya limetokea, mshitakiwa Yuko huru.
 
Hao woye unaowataja hawakupata kuishi hapa duniani. Ni hadithi za kutungwa tuu kama kina madenge na sokomoko wa gazeti la sani.
 
honey pot kwa majajusi wanaelewa hii kitu, hata viongozi na maboss wa miaka hii wanakutana nayo
 
Penzi kitovu cha uzembe.

Mwamba alilala usingizi wa namna gani, alitudhalilisha sana.
Samsoni aliingia mtegoni zaidi ya mara 3 Delila akiwa anamuandalia mazingira ya kumuweza vyema.
Mwisho wa Siku Samsoni akaisema siri yake na Delila kufanya yake.
 
Back
Top Bottom