makedonia
JF-Expert Member
- Nov 17, 2014
- 4,171
- 3,461
YesSamsoni hakunyolewa na Delila bali Delila amekaa kusingiziwaView attachment 2040992
Imekuwa ikienea kuwa mwanamke kwa jina la Delila ndiye alimunyoa Samsoni kitu ambacho si kweli. Wengi hufikiri kuwa Samsoni alinyolewa na Delila.
Ushahidi unaonyesha katika biblia takatifu Delila yeye alihusika katika kumdanganya Samsoni na kujua siri zilizo zificha katika Nywele zake na Delila yeye alihusika pia wakati Samsoni ananyolewa lakini Delila binafsi yeye hakumunyoa Samsoni kitu ambacho Delila amekaa kusingiziwa.
Ushahidi katika biblia ukisoma Waamuzi 16:19
Imeandikwa "Waamuzi 16:19
[19]Naye akamlaza usingizi magotini pake. Kisha akamwita mtu akavinyoa vile vishungi saba vya nywele za kichwa chake; akaanza kumsumbua, nguvu zake zikamtoka.
Hivyo ukirejea ushahidi wa biblia Samsoni alinyolewa na mtu mwingine ambaye hakutajwa na wakati huo Samsoni alikuwa magotini mwa Delila.
Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app