Ushahidi: Delila hakumnyoa Samsoni bali alisingiziwa

Delila afungue mashtaka kwa kusingiziwa, dunia mzima tunajua yeye ndo Gaidi kama Mbowe.
Akifungua mashitaka ya kusingiziwa nae watamfungulia maana anakabiliwa na kesi nyingi sana.
 
Bado Delila ni mtuhumiwa namba 1.

Mashtaka ya Delila:
1.Kula njama za kumnyoa Samson
2.Kumlewesha Samson kwa nia ovu ya kumnyoa nywele zake.
3.Kushiriki kumnyoa samson.
4.Kutakatisha pesa(pesa alizolipwa baada kutekeleza huu uhalifu)
5.Uhujumu uchumi
Hapo kweli Delila anakabiliwa na mashtaka mengi sana ila nae atawashitaki kwa kumsingizia kuwa alimunyoa Samsoni.
 
Mkuu namba 4 hakuna uhakika kama alifanya hivyo.
Alifanya hivyo rejea hapa;

Waamuzi 16:5,18
[5]Nao wakuu wa Wafilisti wakamwendea, wakamwambia, Mbembeleze, upate kujua asili ya nguvu zake nyingi, na jinsi tutakavyoweza kumshinda, tupate kumfunga na kumtesa; nasi tutakupa kila mtu fedha elfu na mia moja.
[18]Delila alipoona ya kuwa amemwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akatuma mtu akawaita wakuu wa Wafilisti, akisema, Njoni huku mara hii tu, maana ameniambia yote aliyo nayo moyoni mwake. Ndipo wakuu wa Wafilisti wakamwendea wakachukua ile fedha mikononi mwao.
 
Akawaambia akinyolewa nywele nguvu zote zitakwisha (anashiriki hapo). Delila atabaki kuwa mtuhumiwa namba moja ksbb pekee ndie alieuza siri ya nguvu za Samson kuwa kwenye nywele. Akamlewesha na kilevi ili alale na anyolewe (dhamira ovu ya Delila ikatimia)
Delila anakabiliwa na mashtaka mengi sana ila sema dunia imeaminishwa uongo kuwa Delila alimunyoa Samsoni kitu ambacho si kweli ila Delila alishiliki kumnyoa.
 
Hii Stori ukiangalia kwa umakini ni kuwapa Onyo wanaume WA Israel wasioe makabila mengine... Ni pure Ubaguzi.
Kweli kabisa hapa wanatuaminisha kutowaamini watu wa upande mwingine.
 
sawa ila kuna mazingira ya kumuuza samson.
Delila hana kosa kabisa. Yeye alikuwa AFISA MPELELEZI AKA AFISA KIPENYO WA WAFILISTI. KUMBUKA WAFILISTI WALIKUWA WANAPIGANA NA HAO WATOTO WA ISRAEL KITAMBO SO ZILIKUWA JAMII ADUI. SO DELILA ALITUMWA YEYE KAMA JASUSI ALIYEKAMILIKA KUMALIZA KAZI ILIYOWASHINDA WENGI. Kosa ni la Samson kumuamini Beibe wa upande wa adui eti akupende mazima. Hawa wa hapa bongo tu wote wa tz na kabila moja na wanatutenda sembuse huyo adui wa kifilisti. Muacheni Delila na ntafungua kesi mahakamani kwa wote waliomzalilisha
 
Bado Delila ni mtuhumiwa namba 1.

Mashtaka ya Delila:
1.Kula njama za kumnyoa Samson
2.Kumlewesha Samson kwa nia ovu ya kumnyoa nywele zake.
3.Kushiriki kumnyoa samson.
4.Kutakatisha pesa(pesa alizolipwa baada kutekeleza huu uhalifu)
5.Uhujumu uchumi
Delila hawezi kuwa mtuhumiwa wakati alikua kazini,, kazi ya kachero yeyote kunasa magaidi, samson alikua gaidi mmoja hatari sana, akiua watu ovyo ovyo tu,
Delila alikuwa undercover agent wa serikali ya wafilisti,, kipindi hicho waisrael hawakuwa na taifa lao, na waliishi katika nchi ya caanan, chini ya utawala wa wafilisti,,
Samsoni alikuwa kafanya ugaidi wa kuchoma moto mashamba ya watu, pamoja na kufanya mauaji mengi ili ajipatie magovi kwa ajili ya kulipia mahari au betting kama sikosei
 
Delila hana kosa kabisa. Yeye alikuwa AFISA MPELELEZI AKA AFISA KIPENYO WA WAFILISTI. KUMBUKA WAFILISTI WALIKUWA WANAPIGANA NA HAO WATOTO WA ISRAEL KITAMBO SO ZILIKUWA JAMII ADUI. SO DELILA ALITUMWA YEYE KAMA JASUSI ALIYEKAMILIKA KUMALIZA KAZI ILIYOWASHINDA WENGI. Kosa ni la Samson kumuamini Beibe wa upande wa adui eti akupende mazima. Hawa wa hapa bongo tu wote wa tz na kabila moja na wanatutenda sembuse huyo adui wa kifilisti. Muacheni Delila na ntafungua kesi mahakamani kwa wote waliomzalilisha
Ila pia na yeye alipokea rushwa hapo atabaki kuwa na makosa.

Waamuzi 16:5,18
[5]Nao wakuu wa Wafilisti wakamwendea, wakamwambia, Mbembeleze, upate kujua asili ya nguvu zake nyingi, na jinsi tutakavyoweza kumshinda, tupate kumfunga na kumtesa; nasi tutakupa kila mtu fedha elfu na mia moja.
[18]Delila alipoona ya kuwa amemwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akatuma mtu akawaita wakuu wa Wafilisti, akisema, Njoni huku mara hii tu, maana ameniambia yote aliyo nayo moyoni mwake. Ndipo wakuu wa Wafilisti wakamwendea wakachukua ile fedha mikononi mwao.
 
Hao woye unaowataja hawakupata kuishi hapa duniani. Ni hadithi za kutungwa tuu kama kina madenge na sokomoko wa gazeti la sani.
Ngoja tufanye tafiti ila kuna watafiti huleta ushahidi kuwa hivyo vitu vilitokea.
 
Lakini sio ilikuwa mipango ya Mungu itokee vile ili samson akawashikishe adabu wafirisiti.
Unaamini ya kuwa alicho panga Mungu binadamu hawezi kupangua.
 
Delila hawezi kuwa mtuhumiwa wakati alikua kazini,, kazi ya kachero yeyote kunasa magaidi, samson alikua gaidi mmoja hatari sana, akiua watu ovyo ovyo tu,
Delila alikuwa undercover agent wa serikali ya wafilisti,, kipindi hicho waisrael hawakuwa na taifa lao, na waliishi katika nchi ya caanan, chini ya utawala wa wafilisti,,
Samsoni alikuwa kafanya ugaidi wa kuchoma moto mashamba ya watu, pamoja na kufanya mauaji mengi ili ajipatie magovi kwa ajili ya kulipia mahari au betting kama sikosei
Kwa nini Delila alipokea rushwa ili kuifanya kazi hiyo?
 
Samsoni aliingia mtegoni zaidi ya mara 3 Delila akiwa anamuandalia mazingira ya kumuweza vyema.
Mwisho wa Siku Samsoni akaisema siri yake na Delila kufanya yake.
Bila shaka hii siri samsoni aliitoa wakiwa kitandani
 
Back
Top Bottom