Ushahidi: Jinsi CCM "walivyoshinda uchaguzi" kwa kishindo cha 98%

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,843
Reaction score
29,350
Mbinu zilizotumika kwenye "uchaguzi" wa mwaka 2020 ndizo walizopanga kuzitumia pia mwaka 2025. Lakini safari hii liliwakuta jambo ikabidi wabadili gea angani.

Mwaka 2020 wasimamizi wa vituo waliletewa matokeo ya bandia na ARO Kata wakati upigaji wa kura halali ukiendelea. Hizo kura za mchongo ndizo ambazo wasimamizi walielekezwa kuziingiza kwenye karatasi ya mwisho ya matokeo ambayo hubandikwa kwenye kituo cha kupigia kura. Haijalishi kama kura hizo zitatofautiana na kura halali zilizopigwa kwa kiasi gani. Cha muhimu tu hizo kura zisizidi idadi ya wapigakura waliojiandikisha.

Swali: je, mgombea wa chama cha upinzani akiamua kwenda mahakamani kudai kura zilizotangazwa sio halali itakuwaje? Jibu ni kwamba baada ya zoezi la kupiga kura kutamatika, Mkurugenzi wa halmashauri, ambaye ni kada maarufu wa CCM, huwakusanya makada wa CCM na mamluki wengine na kuwafungia mahali ambapo huwapigisha kura ili kufikisha idadi ya kura zilizochakachuliwa. Kwa mfano, kama kwenye kituo A kura halali zilizopigwa ni 23 lakini zilichakachuliwa na kuandikwa 400, basi watu hao watapewa makaratasi ya kura na kutiki kura 377 na kisha kuziingiza kwenye masanduku. Ile rakili iliyofungwa siku ya kupiga kura hukatwa na kufungwa rakili mpya. Hapa hata mtu ukienda mahakamani, kura zikahesabiwa upya bado huwezi kufua dafu. Hii ilikuwa drama ya mwaka 2020.

Sasa tugeukie wizi wa 2025. Wizi wa safari hii ulikuwa tofauti kwa sababu ya tishio la maandamano na kususia upigaji kura. Msimamizi mmoja wa kituo cha uchaguzi aliniambia kuwa idadi ya watu waliopiga kura kwa kila kituo haikuzidi 50. Kwa mfano, katika kituo alichosimamia, chenye idadi ya wapiga kura 500 waliojiandikisha, ni watu 98 (19.6%) tu waliofika kupiga kura. Lakini kwenye karatasi ya kuingiza matokeo ya jumla ambayo aliiwasilisha kwa mkurugenzi (RO) aliongeza namba 4 mwanzoni na kupelekea matokeo kusoma 498 (99.66%). Hivi ndivyo kura zilivyokuzwa safari hii baada ya kuwa mbinu iliyotumika mwaka 2020 imegunduliwa na viongozi wa upinzani. Ile haikutumika tena safari hii. Na haya maelekezo ya kuandika namba nyuma ya matokeo halali ili kuongeza kura na idadi ya waliopiga kura, yalitolewa siku chache kabla ya siku ya uchaguzi. Tukumbuke wasimamizi hawa ni watumishi wa halmashauri na mkurugenzi ndiye bosi wao. Hivyo, hawawezi kukataa kutii maelekezo ya bosi.

Ukweli ni kwamba baada ya wapinzani wa kweli (CHADEMA) kujitoa kwenye kinyang'anyiro hiki, ilikuwa lazima CCM washinde hata bila kuchakachua kura kwa sababu hata mgombea akiamua kuchukua ukoo wake wa watu 30 wakaenda kumpigia kura, lazima tu ataibuka mshindi. Kwa utaratibu wa uchaguzi wa Tanzania, anayepata kura nyingi ndiye mshindi. Haijalishi umepigiwa kura na watu wangapi.

Kwa bahati mbaya, CCM kwa kutaka sifa pamoja na kuwakomoa wasusiaji, wakaamua kuwaelekeza wasimamizi wa vituo kukuza kura ili kuuhadaa umma wa kimataifa na pia kujihadaa wao wenyewe kwamba wapigakura walijitokeza kwa wingi kwenye vituo vya kupigia kura na kuonyesha kuwa mama anaupiga mwingi.

Nchi ya ovyo kabisa. Wapinzani wa kweli wamekuwaachieni ulingo upigane na wewe mwenyewe lakini bado unakuza matokeo! Hii ni aibu kubwa sana kwa Samia na genge lake. Ipo siku Mungu atawahukumu sawasawa na matendo yao maovu.
​
 
Mbinu zilizotumika kwenye "uchaguzi" wa mwaka 2020 ndizo walizopanga kuzitumia pia mwaka 2025. Lakini safari hii liliwakuta jambo ikabidi wabadili gea angani.

Mwaka 2020 wasimamizi wa vituo waliletewa matokeo ya bandia na ARO Kata wakati upigaji wa kura halali ukiendelea. Hizo kura za mchongo ndizo wasimamizi walipaswa kuziingiza kwenye karatasi ya mwisho ya matokeo ambayo hubandikwa kwenye kituo cha kupigia kura. Haijalishi kama kura hizo zitatofautiana na kura halali zilizopigwa kwa kiasi gani. Cha muhimu tu hizo kura zisizidi idadi ya wapigakura waliojiandikisha.

Swali: je, mgombea wa chama cha upinzani akiamua kwenda mahakamani kudai kura zilizotangazwa sio halali itakuwaje? Jibu ni kwamba baada ya zoezi la kupiga kura kutamatika, Mkurugenzi wa halmashauri, ambaye ni kada maarufu wa CCM, huwakusanya makada wa CCM na mamluki wengine na kuwafungia mahali ambapo huwapigisha kura ili kufikisha idadi ya kura zilizochakachuliwa. Kwa mfano, kama kwenye kituo A kura halali zilizopigwa ni 23 lakini zilichakachuliwa na kuandikwa 400, basi watu hao watapewa makaratasi ya kura na kutiki kura 377 na kisha kuziingiza kwenye masanduku. Ile rakili iliyofungwa siku ya kupiga kura hukatwa na kufungwa rakili mpya. Hapa hata mtu ukienda mahakamani, kura zikahesabiwa upya bado huwezi kufua dafu. Hii ilikuwa drama ya mwaka 2020.

Sasa tugeukie wizi wa 2025. Wizi wa safari hii ulikuwa tofauti kwa sababu ya tishio la maandamano na kususia upigaji kura. Msimamizi mmoja wa kituo cha uchaguzi aliniambia kuwa idadi ya watu waliopiga kura kwa kila kituo haikuzidi 50. Kwa mfano, katika kituo alichosimamia, chenye idadi ya wapiga kura 500 waliojiandikisha, ni watu 98 (19.6%) tu waliofika kupiga kura. Lakini kwenye karatasi ya kuingiza matokeo ya jumla ambayo aliiwasilisha kwa mkurugenzi (RO) aliongeza namba 4 mwanzoni na kupelekea matokeo kusoma 498 (99.66%). Hivi ndivyo kura zilivyokuzwa safari hii baada ya kuwa mbinu iliyotumika mwaka 2020 imegunduliwa na viongozi wa upinzani. Ile haikutumika tena safari hii. Na haya maelekezo ya kuandika namba nyuma ya matokeo halali ili kuongeza kura na idadi ya waliopiga kura, yalitolewa siku chache kabla ya siku ya uchaguzi. Tukumbuke wasimamizi hawa ni watumishi wa halmashauri na mkurugenzi ndiye bosi wao. Hivyo, hawawezi kukataa kutii maelekezo ya bosi.

Ukweli ni kwamba baada ya wapinzani wa kweli (CHADEMA) kujitoa kwenye kinyang'anyiro hiki, ilikuwa lazima CCM washinde hata bila kuchakachua kura kwa sababu hata mgombea akiamua kuchukua ukoo wake watu 30 wakaenda kumpigia kura, lazima tu ataibuka mshindi. Kwa utaratibu wa uchaguzi wa Tanzania, anayepata kura nyingi ndiye mshindi. Haijalishi watu waliojiandikisha ni wangapi.

Kwa bahati mbaya, CCM kwa kutaka sifa pamoja na kuwakomoa wasusiaji, wakaamua kuwaelekeza wasimamizi wa vituo kukuza kura ili kuuhadaa umma wa kimataifa na pia kujihadaa wao wenyewe kwamba wapigakura walijitokeza kwa wingi kwenye vituo vya kupigia kura na kuonyesha kuwa mama anaupiga mwingi.

Nchi ya ovyo kabisa. Wapinzani wa kweli wamekuwaachieni ulingo upigane na wewe mwenyewe lakini unakuza matokeo! Hii aibu kubwa sana kwa Samia na genge lake. Ipo siku Mungu atawahukumu sawasawa na matendo yao maovu.
​

Hiyo siyo mbinu na hakuna mbinu yeyote wanayoitumia kushinda. Kinachofanyika ni kujitangazia matokeo kwa namna wanavyotska na baadaye kukaa vhini na kutengeneza hayo matokeo.
 
Kwa, utawala,huu wa, ccm, genz imewathibitishia kuwa wanaweza kupoteza madaraka, sasa, watafanya kila kitu kulishika jeshi, ikishindikana uchavuzi, ujao wataua, watu wengi, na hapo jeshi, litachukua nchi, jeshi, likikamatwa, na lenyewe likawa, kama idara, ya, ccm, basi, nchi itakuwa, imefika kwenye kiwango cha utawala wa, Rais wa, zamani wa, Raanda, Habyarimana, au Milton Obote wa, Uganda, nchi walizitawala kidiketa, wakisadiwa, na, jeshi, ilibidi watu waingie msituni kuwatoa,
Kipindi hicho, Ma gen Z Kagame, mseven, kiiza besigye,Kayumba nyamwasa, Patric kalegeya, winne byanyima,waliingia msituni na kuendesha Vita
 
Hiki ndicho kitakachofuata ikiwa CCM wataendelea kuziba masikio. Kusikia kwa mamba hadi damu masikioni. Roho za watu waliowaua na kuwachoma moto kwenye tanuru wengine wakiwa hai, haziwezi kwenda bure.
 
Inategemea na eneo mkuu. Kwenye maeneo ya mijini waliogopa kutumia mbinu ya zamani wakaamua kutumia hii mbinu mpya.
Hapo juu umeandika Mungu atawahukumu! Sasa ya nini kuandika hapa? Si ungeeacha tu Mungu afanye kazi yake?

Hujaowasoma G -Z wao hawakungojea Mungu, na ndiyo huo ukweli, hata Samia na genge lake lote nao wanaamini Mungu.
 
Tunawapiga kotekote mkuu. Tinawapiga kwa kutumia Gen Z na kwa kutumia Mungu. Mashambulizi yote ni sahihi.
 
Ccm ni loser
95887660-375c-4207-abb3-d87bb061f54d.jpeg
 
Mbinu zilizotumika kwenye "uchaguzi" wa mwaka 2020 ndizo walizopanga kuzitumia pia mwaka 2025. Lakini safari hii liliwakuta jambo ikabidi wabadili gea angani.

Mwaka 2020 wasimamizi wa vituo waliletewa matokeo ya bandia na ARO Kata wakati upigaji wa kura halali ukiendelea. Hizo kura za mchongo ndizo wasimamizi walipaswa kuziingiza kwenye karatasi ya mwisho ya matokeo ambayo hubandikwa kwenye kituo cha kupigia kura. Haijalishi kama kura hizo zitatofautiana na kura halali zilizopigwa kwa kiasi gani. Cha muhimu tu hizo kura zisizidi idadi ya wapigakura waliojiandikisha.

Swali: je, mgombea wa chama cha upinzani akiamua kwenda mahakamani kudai kura zilizotangazwa sio halali itakuwaje? Jibu ni kwamba baada ya zoezi la kupiga kura kutamatika, Mkurugenzi wa halmashauri, ambaye ni kada maarufu wa CCM, huwakusanya makada wa CCM na mamluki wengine na kuwafungia mahali ambapo huwapigisha kura ili kufikisha idadi ya kura zilizochakachuliwa. Kwa mfano, kama kwenye kituo A kura halali zilizopigwa ni 23 lakini zilichakachuliwa na kuandikwa 400, basi watu hao watapewa makaratasi ya kura na kutiki kura 377 na kisha kuziingiza kwenye masanduku. Ile rakili iliyofungwa siku ya kupiga kura hukatwa na kufungwa rakili mpya. Hapa hata mtu ukienda mahakamani, kura zikahesabiwa upya bado huwezi kufua dafu. Hii ilikuwa drama ya mwaka 2020.

Sasa tugeukie wizi wa 2025. Wizi wa safari hii ulikuwa tofauti kwa sababu ya tishio la maandamano na kususia upigaji kura. Msimamizi mmoja wa kituo cha uchaguzi aliniambia kuwa idadi ya watu waliopiga kura kwa kila kituo haikuzidi 50. Kwa mfano, katika kituo alichosimamia, chenye idadi ya wapiga kura 500 waliojiandikisha, ni watu 98 (19.6%) tu waliofika kupiga kura. Lakini kwenye karatasi ya kuingiza matokeo ya jumla ambayo aliiwasilisha kwa mkurugenzi (RO) aliongeza namba 4 mwanzoni na kupelekea matokeo kusoma 498 (99.66%). Hivi ndivyo kura zilivyokuzwa safari hii baada ya kuwa mbinu iliyotumika mwaka 2020 imegunduliwa na viongozi wa upinzani. Ile haikutumika tena safari hii. Na haya maelekezo ya kuandika namba nyuma ya matokeo halali ili kuongeza kura na idadi ya waliopiga kura, yalitolewa siku chache kabla ya siku ya uchaguzi. Tukumbuke wasimamizi hawa ni watumishi wa halmashauri na mkurugenzi ndiye bosi wao. Hivyo, hawawezi kukataa kutii maelekezo ya bosi.

Ukweli ni kwamba baada ya wapinzani wa kweli (CHADEMA) kujitoa kwenye kinyang'anyiro hiki, ilikuwa lazima CCM washinde hata bila kuchakachua kura kwa sababu hata mgombea akiamua kuchukua ukoo wake watu 30 wakaenda kumpigia kura, lazima tu ataibuka mshindi. Kwa utaratibu wa uchaguzi wa Tanzania, anayepata kura nyingi ndiye mshindi. Haijalishi watu waliojiandikisha ni wangapi.

Kwa bahati mbaya, CCM kwa kutaka sifa pamoja na kuwakomoa wasusiaji, wakaamua kuwaelekeza wasimamizi wa vituo kukuza kura ili kuuhadaa umma wa kimataifa na pia kujihadaa wao wenyewe kwamba wapigakura walijitokeza kwa wingi kwenye vituo vya kupigia kura na kuonyesha kuwa mama anaupiga mwingi.

Nchi ya ovyo kabisa. Wapinzani wa kweli wamekuwaachieni ulingo upigane na wewe mwenyewe lakini unakuza matokeo! Hii aibu kubwa sana kwa Samia na genge lake. Ipo siku Mungu atawahukumu sawasawa na matendo yao maovu.
​
Jakaya Mrisho Kikwete aliwahi kusema kuwa CCM wana mbinu zaidi ya 100 za kuiba kura ili kushinda uchaguzi hivyo hadi sasa wametumia mbinu 4 tu za wizi wa kura bado wanazo mbinu 96 kibindoni, hawa watu ni washenzi sana.
 
Hiyo siyo mbinu na hakuna mbinu yeyote wanayoitumia kushinda. Kinachofanyika ni kujitangazia matokeo kwa namna wanavyotska na baadaye kukaa vhini na kutengeneza hayo matokeo.
We hujui choçhote. Nakumbuka Nape aliwahi kusema CCM wana mbinu 1000 za ushindi> likiwemo bao la mkono.
 
Jakaya Mrisho Kikwete aliwahi kusema kuwa CCM wana mbinu zaidi ya 100 za kuiba kura ili kushinda uchaguzi hivyo hadi sasa wametumia mbinu 4 tu za wizi wa kura bado wanazo mbinu 96 kibindoni, hawa watu ni washenzi sana.
Hawa watu ni zaidi ya ibilisi
 
Umenena vyema. Umesema kweli kabisa hicho ndicho kilichofanyika hata hapa kata ya Nyabubinza wilaya ya Maswa Mkoa wa Simiyu.
 
Back
Top Bottom