Ushahidi: Jinsi CCM "walivyoshinda uchaguzi" kwa kishindo cha 98%

Huo Uhuni kwako ni mbinu...!!?
Kwa CCM kila kitu kinawezekana. Kama wamewachukua majeruhi hospitali na kwenda kuwachoma moto kwenye tanuru la Wazo Hill wakiwa hai, hawashindwi kitu.
 
Mbinu zilizotumika kwenye "uchaguzi" wa mwaka 2020 ndizo walizopanga kuzitumia pia mwaka 2025. Lakini safari hii liliwakuta jambo ikabidi wabadili gea angani.

Mwaka 2020 wasimamizi wa vituo waliletewa matokeo ya bandia na ARO Kata wakati upigaji wa kura halali ukiendelea. Hizo kura za mchongo ndizo ambazo wasimamizi walielekezwa kuziingiza kwenye karatasi ya mwisho ya matokeo ambayo hubandikwa kwenye kituo cha kupigia kura. Haijalishi kama kura hizo zitatofautiana na kura halali zilizopigwa kwa kiasi gani. Cha muhimu tu hizo kura zisizidi idadi ya wapigakura waliojiandikisha.

Swali: je, mgombea wa chama cha upinzani akiamua kwenda mahakamani kudai kura zilizotangazwa sio halali itakuwaje? Jibu ni kwamba baada ya zoezi la kupiga kura kutamatika, Mkurugenzi wa halmashauri, ambaye ni kada maarufu wa CCM, huwakusanya makada wa CCM na mamluki wengine na kuwafungia mahali ambapo huwapigisha kura ili kufikisha idadi ya kura zilizochakachuliwa. Kwa mfano, kama kwenye kituo A kura halali zilizopigwa ni 23 lakini zilichakachuliwa na kuandikwa 400, basi watu hao watapewa makaratasi ya kura na kutiki kura 377 na kisha kuziingiza kwenye masanduku. Ile rakili iliyofungwa siku ya kupiga kura hukatwa na kufungwa rakili mpya. Hapa hata mtu ukienda mahakamani, kura zikahesabiwa upya bado huwezi kufua dafu. Hii ilikuwa drama ya mwaka 2020.

Sasa tugeukie wizi wa 2025. Wizi wa safari hii ulikuwa tofauti kwa sababu ya tishio la maandamano na kususia upigaji kura. Msimamizi mmoja wa kituo cha uchaguzi aliniambia kuwa idadi ya watu waliopiga kura kwa kila kituo haikuzidi 50. Kwa mfano, katika kituo alichosimamia, chenye idadi ya wapiga kura 500 waliojiandikisha, ni watu 98 (19.6%) tu waliofika kupiga kura. Lakini kwenye karatasi ya kuingiza matokeo ya jumla ambayo aliiwasilisha kwa mkurugenzi (RO) aliongeza namba 4 mwanzoni na kupelekea matokeo kusoma 498 (99.66%). Hivi ndivyo kura zilivyokuzwa safari hii baada ya kuwa mbinu iliyotumika mwaka 2020 imegunduliwa na viongozi wa upinzani. Ile haikutumika tena safari hii. Na haya maelekezo ya kuandika namba nyuma ya matokeo halali ili kuongeza kura na idadi ya waliopiga kura, yalitolewa siku chache kabla ya siku ya uchaguzi. Tukumbuke wasimamizi hawa ni watumishi wa halmashauri na mkurugenzi ndiye bosi wao. Hivyo, hawawezi kukataa kutii maelekezo ya bosi.

Ukweli ni kwamba baada ya wapinzani wa kweli (CHADEMA) kujitoa kwenye kinyang'anyiro hiki, ilikuwa lazima CCM washinde hata bila kuchakachua kura kwa sababu hata mgombea akiamua kuchukua ukoo wake wa watu 30 wakaenda kumpigia kura, lazima tu ataibuka mshindi. Kwa utaratibu wa uchaguzi wa Tanzania, anayepata kura nyingi ndiye mshindi. Haijalishi umepigiwa kura na watu wangapi.

Kwa bahati mbaya, CCM kwa kutaka sifa pamoja na kuwakomoa wasusiaji, wakaamua kuwaelekeza wasimamizi wa vituo kukuza kura ili kuuhadaa umma wa kimataifa na pia kujihadaa wao wenyewe kwamba wapigakura walijitokeza kwa wingi kwenye vituo vya kupigia kura na kuonyesha kuwa mama anaupiga mwingi.

Nchi ya ovyo kabisa. Wapinzani wa kweli wamekuwaachieni ulingo upigane na wewe mwenyewe lakini bado unakuza matokeo! Hii ni aibu kubwa sana kwa Samia na genge lake. Ipo siku Mungu atawahukumu sawasawa na matendo yao maovu.
​
Mr tpaul mwaka huu haikuwa hivyo

From the beginning, Tume ya Uchaguzi ilikuwa ijajua fika kuwa watu hawatakwenda kupiga kura

Kwa kujua hili, mchakato wa kuiba uchaguzi ukaanza toka ndani ya ofisi za Tume yenyewe na kila kituo kikapewa idadi ya kura zilizopigwa na Samia kupewa za kwake Ili tu isiwe under 98%..!

Na utaratibu wenyewe wa wizi mwaka huu 2025 ulikuwa hivi:

1. Ulianza kwenye uandikishaji wapiga kura wengi hewa hata registered voters wa Tanzania kufikia a record of 32,000,000. Kumbuka, watu walihoji uhalali wa takwimu hizi from the beginning, lakini Tume ya Uchaguzi haikutoa majibu yoyote ya kuridhisha zaidi ya blah blah. Lakini, the fact ni kuwa, ndo wizi wenyewe wa kumtafutia kura bandia Samia ulikuwa unapikwa!!

2. Pili, kupanga vituo vya kupigia kura vyote nchi nzima; kila Kijiji/mtaa, kila kata na kila Jimbo sambamba na kupanga idadi ya wapiga kura kwa kila kituo

3. Kwa kujua kuwa watu hawatakwenda kupiga kura na wakiwa wamedhamiria kumpitisha "mama yao kwa 98%" waliseti "target" ya kura anazotakiwa apate kitaifa bila kujali kama watu watakwenda kupiga kura ama la

4. Target ya idadi ya kura hizo ikavunjwa vunjwa (broken down) na kugawanywa kwenye majimbo kwa wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo

5. Wasimamizi wa majimbo nao Wakai - break down na kuishusha kwa wasimamizi wa kata (walioitwa ARO - Assistant Returning Officers). Kumbuka target ni kura zile zile milioni 32 sawa na 98%!!

6. Hawa ARO wa kata wakazi - distribute kura hizo (number) kwa kila kituo na zisomeke hivyo kwenye fomu za matokeo haijalishi watu wamepiga kura ama la. Mfano kama kituo kina wapiga kura 500, basi lazima fomu ya matokeo isomeke kuwa waliojitokeza kupiga kura ni 498 na Samia kapata 480 (98%) na wengine 18!!!

NOTE:
👉98% ya matokeo ktk kituo cha kupigia ni reflection halisi ya target ya kitaifa ya Tume ya Uchaguzi ambayo ndio hiyohiyo 98%. Hii reflection ya 98% ni lazima itambae hivyo kutoka kituo cha kupigia kura 98% ➖Katani 98% ➖Jimboni 98% na ➖Taifa 98%. Ndicho hicho tulichokiona..!!

👉Angalia wakati wa utangazaji wa matokeo ulivyokuwa. Ulikuwa very smooth kwa kuwa kila kitu kilishaandaliwa mapema. Hata hivyo, pamoja na kuwa hawakupata shida kutangaza matokeo yao ya kupika, lakini body language yao, nyuso zao zilikuwa zimejaa haya na hofu kuu kwa sbb waliokuwa wanatambua kuwa wanatangaza uongo na uchafu mtupu!!

👉Cha kushangaza ni kuwa hata maeneo yaliyoathiriwa vibaya na vurugu kukiwa na ushahidi kabisa kuwa watu hawakupiga kura, lakini Tume ya Uchaguzi imetangaza matokeo kwa mfumo uleule wa 98% na kwamba watu wote wamejitokeza kupiga kura bila shida kwa kiwango cha 98%😼😼😼!!

👉Wizi wa mwaka huu ulikuwa shahiri dhahiri bila kificho, bila haya wala soni na kwa mabavu makubwa. Na ni hakika kabisa, msimamizi wa kituo ulikuwa ukileta ubishi, wanakuua na kwenda kutupwa katikati ya waandamanaji Ili uonekane umekufa kwenye maandamano

👉 Uchaguzi huu, lilikuwa tukio baya, la aibu, kutia kinyaa na uchafu mtupu. Ni tukio linalotia hasira na fedheha kwa wahusika. Huu haukuwa uchaguzi bali tukio la kihuni lililopangwa na wahuni kwa maslahi yao binafsi na sio ya nchi na wananchi. Ndio maana litapingwa na kukataliwa kwa njia zozote zile mpaka kieleweke!!
 
Mbinu zilizotumika kwenye "uchaguzi" wa mwaka 2020 ndizo walizopanga kuzitumia pia mwaka 2025. Lakini safari hii liliwakuta jambo ikabidi wabadili gea angani.

Mwaka 2020 wasimamizi wa vituo waliletewa matokeo ya bandia na ARO Kata wakati upigaji wa kura halali ukiendelea. Hizo kura za mchongo ndizo ambazo wasimamizi walielekezwa kuziingiza kwenye karatasi ya mwisho ya matokeo ambayo hubandikwa kwenye kituo cha kupigia kura. Haijalishi kama kura hizo zitatofautiana na kura halali zilizopigwa kwa kiasi gani. Cha muhimu tu hizo kura zisizidi idadi ya wapigakura waliojiandikisha.

Swali: je, mgombea wa chama cha upinzani akiamua kwenda mahakamani kudai kura zilizotangazwa sio halali itakuwaje? Jibu ni kwamba baada ya zoezi la kupiga kura kutamatika, Mkurugenzi wa halmashauri, ambaye ni kada maarufu wa CCM, huwakusanya makada wa CCM na mamluki wengine na kuwafungia mahali ambapo huwapigisha kura ili kufikisha idadi ya kura zilizochakachuliwa. Kwa mfano, kama kwenye kituo A kura halali zilizopigwa ni 23 lakini zilichakachuliwa na kuandikwa 400, basi watu hao watapewa makaratasi ya kura na kutiki kura 377 na kisha kuziingiza kwenye masanduku. Ile rakili iliyofungwa siku ya kupiga kura hukatwa na kufungwa rakili mpya. Hapa hata mtu ukienda mahakamani, kura zikahesabiwa upya bado huwezi kufua dafu. Hii ilikuwa drama ya mwaka 2020.

Sasa tugeukie wizi wa 2025. Wizi wa safari hii ulikuwa tofauti kwa sababu ya tishio la maandamano na kususia upigaji kura. Msimamizi mmoja wa kituo cha uchaguzi aliniambia kuwa idadi ya watu waliopiga kura kwa kila kituo haikuzidi 50. Kwa mfano, katika kituo alichosimamia, chenye idadi ya wapiga kura 500 waliojiandikisha, ni watu 98 (19.6%) tu waliofika kupiga kura. Lakini kwenye karatasi ya kuingiza matokeo ya jumla ambayo aliiwasilisha kwa mkurugenzi (RO) aliongeza namba 4 mwanzoni na kupelekea matokeo kusoma 498 (99.66%). Hivi ndivyo kura zilivyokuzwa safari hii baada ya kuwa mbinu iliyotumika mwaka 2020 imegunduliwa na viongozi wa upinzani. Ile haikutumika tena safari hii. Na haya maelekezo ya kuandika namba nyuma ya matokeo halali ili kuongeza kura na idadi ya waliopiga kura, yalitolewa siku chache kabla ya siku ya uchaguzi. Tukumbuke wasimamizi hawa ni watumishi wa halmashauri na mkurugenzi ndiye bosi wao. Hivyo, hawawezi kukataa kutii maelekezo ya bosi.

Ukweli ni kwamba baada ya wapinzani wa kweli (CHADEMA) kujitoa kwenye kinyang'anyiro hiki, ilikuwa lazima CCM washinde hata bila kuchakachua kura kwa sababu hata mgombea akiamua kuchukua ukoo wake wa watu 30 wakaenda kumpigia kura, lazima tu ataibuka mshindi. Kwa utaratibu wa uchaguzi wa Tanzania, anayepata kura nyingi ndiye mshindi. Haijalishi umepigiwa kura na watu wangapi.

Kwa bahati mbaya, CCM kwa kutaka sifa pamoja na kuwakomoa wasusiaji, wakaamua kuwaelekeza wasimamizi wa vituo kukuza kura ili kuuhadaa umma wa kimataifa na pia kujihadaa wao wenyewe kwamba wapigakura walijitokeza kwa wingi kwenye vituo vya kupigia kura na kuonyesha kuwa mama anaupiga mwingi.

Nchi ya ovyo kabisa. Wapinzani wa kweli wamekuwaachieni ulingo upigane na wewe mwenyewe lakini bado unakuza matokeo! Hii ni aibu kubwa sana kwa Samia na genge lake. Ipo siku Mungu atawahukumu sawasawa na matendo yao maovu.
​

Hakukuwa na mbinu zozote bali ni uharamia na kulazimisha.
 
Attachments

  • 6223126-8be1d1a5066d282c809bb601c639198.mp4
    4 MB
Afu eti wapinzani uchwara wote hakuna aliyeenda hata kupinga matokeo mahakamani. Wamekubaliana kuwa wameshindwa kihalali.
 
Back
Top Bottom