papaayenga
JF-Expert Member
- Dec 21, 2013
- 765
- 503
I think unakubaliana na mtazamo kuwa viumbe vinafanya mageuzi. Lakini unakataa mtazamo kuwa Species mpya haziwezi kuwepo. Bali mageuzi yaliyopo ni kama yana kikomo. Hayawezi kupelekea uwepo wa species mpya. Na ushahidi unaopatikana kwa fossils, archaeological data na DNA unaona kuwa ndizo zinazokosea na kupelekea wanadamu kutazama kuwa ni species mpya kumbe ni zile zile. So, unakubali evolution (mabadiliko ya viumbe), lakini sio kupelekea kwa uwepo wa viumbe vipya.
Ni mojawapo ya changamoto kwangu katika kuelewa mtazamo huo. Kwa sababu, ushahidi wa DNA na fossils unaonyesha dhahiri kuwa viumbe vinaweza kubadilika na kupelekea kutokea kwa species mpya.
Nakupa ushahidi mzuri sana kuhusiana na kiumbe species ambayo imekuja kuwa kiumbe cha aina yake kutokana na mabadiliko ya kuadapt mazingira mapya.
NYANGUMI: Umeshawahi kujiuliza ni kwanini nyangumi ananyonyesha? Hana mapafu? Anazaa? Ana mikono sawa kama mmalia, na ana manyoya bila magamba kama samaki? Katika mtazamo wa kidini ambao ndio unaoamini ni sahihi unaamini aliumbwa hivyo hivyo kama alivyo na muumba. Lakini sio mtazamo sahihi kwa sababu nyangumi alikuwa ni mnyama aliyependelea kufanya mawindo yake katika kingo za bahari. Katika addaptation hiyo akazoea kukaa kwenye maji kwa muda mrefu na kutokana na uchache wa samaki katika pwani akazoea kwenda mbali na pwani na kuwinda na katika mazoea ya miaka zaidi ya milions of years amekuwa na adaptation ya kuishi kwenye bahari. Sio mfano wa viumbe vilivyokuwa nchi kavu na kuzoea kuishi majini, kuna viumbe kama chura, penguins, sea lions na kobe ambao wote hao ni kutokana na adaptation tofauti na mazoea tofauti na kupelekea hali tofauti walizonazo. Ni mabadiliko ya species mpya. Leo hii kasa hawezi kuzaliana na kobe wa nchi kavu hata kama wote ni kobe, na ndio sababu tunaita ni species. Tunaangalia classification ya species kwa kuangalia pia na uwezo wa kuzaliana (yaani kufanya mating) na sio kuangalia muonekano tu. Kubadilika kwa muonekano ni ishara ya kutofautiana katika adaptation tofauti (mfano mtu mweusi na mtu mweupe ni kutokana na adaptation tofauti na mazingira tofauti ya makazi), na huwa hali hii ya utofauti ikiendelea kwa kipindi kirefu hupelekea species mpya. Tukisema kipindi kirefu tunamaanisha kipindi kirefu sana sio cha miaka ya 1000 au 10,000 bali ni miaka mamilioni.
Hizi sio assumption bali ni mitazamo ambayo inapewa suport kuwa katika mabaki ya fossils na kipimo cha structure ya DNA kwa kila kiumbe
Mawazo yangu ni kuwa katika maisha tuwe tunapenda kuchunguza. Mtu unaposema uislam unasema hivi ni kwamba unajishusha na kuona uislam au dini fulani ndio inajibu kila kitu katika maisha na mitazamo mengine umeshai-exlude. Ni vyema mtu kuchunguza na wewe binafsi, JE NI KWELI, Je mitazamo mingine inasema nini na ushahidi wake ni nini. Fahamu kwa kina zaidi na kisha angalia kipi kina logical na ushahidi mzuri.
Sipingi mitazamo ya uislam juu ya mabadiliko ya viumbe bali naheshimu mitazamo ya kila mtu. Nami pia hapo kabla nilisoma uislam vyema na mitazamo yake. Kinachonipa ugumu, mimi napenda kujifunza na kufahamu kwa ushahidi bila kuwa na imani tu.
Unaweza kuendelea kuamini unavyoweza kuamini. It's free to understand this world as we wish.
I think I am done katika mjadala huu mkuu, asante sana kwa mawazo yako na ushahidi wako.
Thanks.
My Sources
Ten Species That Are Evolving Due to the Changing Climate | Science | Smithsonian
Nami nashukuru, sana hata mimi hapo awali nilikua na mawazo kama hayo yako lakini nilipoanza kusoma upande huu wa dini ndipo nilipogundua kuna aya nyingi ndani ya qur'an zina elezea kua as long as the climate change also species must be change accordingly even human beings we were changed in physical body strength, skin hair, and hight.ect. amazing enough that was tought in a dark age way back 610 AD
Lakini katu hakutotokea kiumbe MPYA
Pamoja na kuwepo mabaki ya fossils na DNA structures ya kila kiumbe bado itabaki ni assumptions za kuja viumbe wapya why? Because species must be created, not formed by a certain conditions, kwa mujibu was Qur'an.
Hebu tumtazame nyangumi katka quran Hawa wanyama wamegawanyika sehemu mbili,sehemu ya kwanza wanaitwa Daabatul bary (wanyama wa nchi kavu) na sehemu ya pili wanaitwa Daabatul bahry ( wanyama wa majini) na Mtume(saw) akasema mnyam wa majini hawezi kuishi nchi kavu akimaanisha kua mnyama ambaye mazalio yake na maisha yake ni majini hawezi akavuta hewa ya nchi kavu kwamuda mrefu, acha wale wanaozalia nchikavu na kuweza kuvuta hewa ya nchi kavu, halafu wanaingia majini hao si wanyama wa majini,
Swali je Nyangumi anaweza kuishi nchi kavu kama anavyo weza kuishi sea lion, penguins, kasa n,k?
Nakama anaweza kuishi nchi kavu basi ni dhahiri hapo mwanzo nyangumi aliishi nchi kavu pamoja na kua hana mapafu na aka adapt mazingira ya majini akawa mnyama wa majini.
Nakama hawezi basi mfumo wa upuaji wa nyangumi ni mfumo wa viumbe wa majini katu hawezi kuishi nchi kavu na fikra za kua aliishi nchi kavu hizo ni assumptions.
Ahsante sana nimefurahi sana mkuu kwa ustaarabu ulioonyesha ktk kubadilishana mawazo na kupeana elimu natarajia ikosiku utaoona ukweli.
THANKS