Kuna mama mmoja kijijini kwetu aliugua kwa kipindi kifupi akafariki, ni miaka karibia 20 sasa, huyu mama baada ya kufa kwa kipindi hicho hakukuwa na utaratibu wa kuhifadhi mwili mochwari, mwili wake ulihifadhiwa chumbani kwa siku 2-3 kusubiri ndugu na jama, siku ya pili baadhi ya ndugu walikuwa wamefika na taratibu za mazishi zikawa zinaendelea ili azikwe siku inayofuata ambayo ni siku ya 3, jioni kuele siku ya tatu alipiga chafya, wamama waliokuwa chumbani wakilinda mwili walitahamaki, bibi mmoja nae yupo mpaka leo akawaambia yeyote asikimbie wala kusema neno, mama aliekuwa amefariki akainuka na kukaa kisha akaomba maji ya kunywa, yule bibi akakataza asipewe kwanza, baada ya kuwa ktk hali fulani ndipo akapewa maji kidogo, baada ya kunywa na kutulia ndipo wakamhoji, akasema alijikuta ameelekea nyumba moja iliojengwa kwa asili ya zamani ya wachaga (msonge) nyumba ya duara iliyoezekwa kwa majani ya migomba, hapo aliwakuta wenyeji wake ambao ni watu anaowafahamu na walishakufa muda mrefu mwanaume na wanawake, wakwanza kumkuta alikuwa mwanamke aliemsimamia pindi alipofanyiwa tohara, alimkuta anafagia uwanja (mazingira ya nyumba) alipobisha hodi alimwitikia na kumuuliza amefuata nini, akamwambia nina njaa sana nipeni kwanza chakula ndipo nitawaambia nilipotoka, watu waliokuwa ndani wakitoka na vyakula, pombe ya mbege, viazi vilivyochemshwa na maziwa mgando wakawa wanampa lakini yule mama aliemsimamia wakati wa tohara akawa anakataa wasimpe hata wakataka kugombana, anaekatazwa kula anamlalamikia kwanini anakataa asipewe chakula ilhali ana njaa na wale wenye vyakula wanapambana kumpa, alipofanikiwa kumzuia kula chochote akamwambia rudi na njia uliokujanayo na usipitie popote, anasema aliondoka kwa hasira ya njaa na akatembea kwa muda mrefu ndipo akajipata yupo pale chumbani amezungukwa na wamama. Hapo ndipo akaambiwa ulikuwa umekufa na ndugu zako wote wameshafika kesho ulikuwa uzimwe. Ni kweli kila kitu kilikuwa kimekamilika kwaajili ya mazishi. Huyu mama yupo na bibi aliekataza watu pale chumbani wasikimbie pia yupo. Sasa huu uzi na hichi nilichokieleza vinanichanganya. Tuwaze pamoja.