Pre GE2025 Ushahidi wa Jinsi Katibu Mkuu wa CCM Emmanuel Nchimbi alivyotapeliwa na kudanganywa huko Itilima huu hapa

Pre GE2025 Ushahidi wa Jinsi Katibu Mkuu wa CCM Emmanuel Nchimbi alivyotapeliwa na kudanganywa huko Itilima huu hapa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ina maana jamaa hawa (ma - CCM) kupitia katibu mkuu wao Emmanuel Nchimbi yanatembea nchi nzima just kuibomoa CHADEMA tu na sio kushughulika na kero za wananchi...?

Ndiyo maana baada ya miaka mitano, serikali imeamua kukwangua kwa magreda barabara za vumbi za mitaa ktk miji yote....

Yaani barabara zimekaa hovyo hovyo miaka yote hii leo CCM kwa kuwa mwezi ujao ni uchaguzi wa serikali za mitaa, eti ndio wanajidai wanawapenda sana wananchi na hivyo wanawakwangulia barabara za vumbi za mitaa yao....

Na tunaposema CCM haipo kwa ajili ya wananchi bali ni kwa ajili yao wenyewe na matumbo yao muwe mnaelewa. Ushahidi ndiyo huo sasa....

UKWELI NI KUWA: Wananchi tumeshaelewa janja yenu, hatudanganyiki na hamuwezi kuendelea kutufanya wajinga na mazwazwa tena. CCM KURA HAITAPATA NG'O labda waibe uchaguzi wote kama 2019 na 2020...

Na safari hii CCM tunawatahadharisha mapema kabisa, kuwa, mkifanya ujinga na upumbavu wa mwaka 2019 na 2020 kutunyang'anya haki yetu ya kuchagua viongozi tunaowataka kutoka vyama tunavyotaka, hakika mtakoma na kujuta nyie nyote na familia zenu...!!
 
Wanasiasa wazuri uwekeza kwenye tangible things/maendeleo ya watu,haki na amani yao.
Ni kweli viongozi ni lazima waanzie ngazi za chini,lakini hawakumbukwi hadi nyakati za uchaguzi.
Hili ni funzo kwa wanasiasa wote kuwekeza rasilimali watu wenye uwezo wa kusimamia manifesto ya vyama vyao kwa muda wote.
 
Tumerudia mara kadhaa humu tukionyesha namna baadhi ya viongozi matapeli wa ccm huko mikoani wakiwafanya viongozi wao wa Kitaifa Mabwege , kwa kuwakusanyia watu duni na wasela na kutangaza kwamba eti ni wanachama wa Chadema wanaohamia ccm, Lakini tumeonekana ni waongo.

Sasa angalia mwenyewe uone Nchimbi alivyopigwa hela kizembe sana

Soma Pia: Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi azifunga Ofisi za CHADEMA Itilima Mkoani Simiyu mbele ya Maelfu ya Wananchi

View attachment 3119104View attachment 3119106View attachment 3119107

Ni Aibu sana kwa kiongozi wa Juu wa CCM kudanganywa na watu wajinga kama hao viongozi wa Itilima.

Naamini baada ya Uzi huu viongozi wote wa CCM wa Itilima watafukuzwa.
What a shame 😂
 
Mdau amekuuliza swali lenye HOJA nzito kuwa,

Sheria zile zile kandamizi na Sasa mlizolalamikia kuwanyanganya ushindi 2020 hakuna hata Moja iliyorekebishwa,

Badala ya kupambania kudai Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote, tunawaambia wananchi wajiandikishe,

Sasa mkihujumiwa kwenye uchaguzi mliouingia Kwa Ishara ya kukubaliana na matokeo, mnawezaje kurudi kulalamikia hujuma endapo zitatokea?
 
Mdau amekuuliza swali lenye HOJA nzito kuwa,

Sheria zile zile kandamizi na Sasa mlizolalamikia kuwanyanganya ushindi 2020 hakuna hata Moja iliyorekebishwa,

Badala ya kupambania kudai Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote, tunawaambia wananchi wajiandikishe,

Sasa mkihujumiwa kwenye uchaguzi mliouingia Kwa Ishara ya kukubaliana na matokeo, mnawezaje kurudi kulalamikia hujuma endapo zitatokea?
Haya
 
Tunawaomba wale Mamluki wa ccm wa humu JF wapitie uzi huu
Hata sielewi ni kwa nini, lakini kazi iliyokuwa ni ya kama "kumsukumiza mlevi" (CCM) shimoni kadri siku zinavyo zidi kusogea; inakuwa kama mlevi huyo huyo kang'ang'ania mikono ya msukumaji (CHADEMA), ambaye inaelekea yeye ndiye atasukumizwa huko huko shimoni na huyu mlevi!

Inashangaza sana na kusikitisha.
 
Mimi sio mwanasiasa wala mwanachama wa chama chochote cha kisiasa, na wala sio social scientist bali nipo kwenye natural sciences. Kwa mujibu wa research nazofanya mojawapo ni qualitative ambayo haihitaji empirical data, tunapata conclusions kwa human perceptions, feelings, thoughts, says, mitazamo, mazungumzo, reactions, nk nk.

Kwa ujumla utafiti wangu usio rasmi qualitatively, naona Chadema ni lidude moja kubwa mno na linalotisha sana kwa kutazama namna reactions, na qualitative data zilizopo humu JF, radioni, social media zingine, TV, blogs, Polisi, jeshini, mitaani, magengeni, chats, groups za chawas etc. hamna siku chadema haijatajwa mara 10 hadi 20! Kuanzia mama yao/yetu akilala, akiamka, akiongea, akiwaza, chadema inazunguka kichwani kwake, makondeko kule kwa landrover kila akiamka, makalai kwenye mizunguko yake ya perdiem, joni nchambi, mcheza kiduku wa daslam, hapi, mkumbwa, cc yote ya ccm, machawa wazoefu na wapya kote mitandaoni, mwashamba, talalalah, choicevariable, yohana mbatizaji, na wengine lukuki. Polisi ndio wakisikia kuanzia kaka yao mkubwa anayevaa official dress na buti hata kwenye sherehe ikulu kama yupo vitani ndio wanapagawa kabisa na kuitana nchi nzima, na kuwasha mazimamoto yao ya kipigaji. Hili dude linawatisha sana kisaikolijia.

My conclusion kwa haya naona chadema sasa niifananishe na maji kwa kweli, yani ni lazima uyatumie tu ili uishi, kuna watu kwa kuitajataja tu wamepata uwaziri, ukuu wa wilaya, ukuu wa mikoa, ubunge, uchawa rasmi, ukatibu-kata na uenezi wa ccm, wengine wakapigwa na pesa, wengine ubalozi, wengine ucovid-19 sasa hii si sawa na maji tu wandugu??

Yani utake usitake utayanywa, usipoyanywa utayaoga, usipoyaoga utafulia, usipoyafulia utapikia, usipopikia utaoshea hata tongotongo. Ili tumbo lako lisitirike kwa sasa we andika, taja, waza, ongea kuhusu chadema, ukiongelea mwengine unafutika tu kama upepo. Relavance yako itakuja kwa kusema chademaaaaa, chademaaaa hata kama huna logic km mwashamba.

Yani kuna watu wasipotaja chadema wanapotea so ili wawe relevant lazima kila siku waje na uzi kuhusu chadema tu, gosh!! Wengine hata spelling hawajui lkn chadema ipo midomoni mwao kutwa kucha.

No offence hii ni perception ya jamii ya watanzania kuanzia mama yetu shuka chini hadi kwa machawa wa level za chini kbs kama hapa nilipo cholesamvula. 😀😎😕
 
Back
Top Bottom