tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 27,843
- 29,350
Awali ya yote napenda kuweka wazi kuwa sishabikii maandamano wala mauaji ya raia wasiokuwa na hatia. Niliyoshuhudia au kusimuliwa na watu kuhusu maauji ya baada ya uchaguzi wa Oktoba 2025 yanahuzunisha sana na yamenifanya niamini kuwa jeshi la polisi Tanzania linafanya kazi kitutusa sana.
Nimeanzisha uzi huu ili tupeane updates kuhusu kilochojiri kwenye maeneo yetu ili kuthibitisha ukiukwaji wa maadili uliofanywa na jeshi la polisi kwa raia wasiokuwa na hatia. Katika eneo nililopo watu wengi sana waliouliwa hawakuwa na hatia na wala hawakuhusika kwenye maandamano. Pamoja na kuzimwa kwa huduma ya internet na wananchi kuzuiliwa kufanya shughuli zao za kiuchumi, ni dhahairi wananchi mmeshuhudia mauaji holela katika maeneo yenu ambayo yangeweza kuepukika ikiwa polisi wangetumia busara na weledi.
Matukio ya kipuuzi na yasiyokuwa na chembe ya utu ambayo nimeshuhudia au kusimuliwa na wananchi wakati nikichukua takwimu za mauaji ni mengi lakini naomba niweke haya machache kwa kuwa mengi yanafanana na haya.
1. Polisi waliingia kwenye kituo cha watoto wanaojifunza mpira (football academy) wakati watoto hao wakijifunza kwa vitendo mambo ya mpira kwenye runinga, wakawaua watoto 7 kwa risasi papo hapo.
2. Katika tukio lingine, polisi waliokuwa wakirandaranda huku na huku walifika kwenye baa moja na kuwakuta watu wakinywa pombe. Wakamuita mzee mmoja akatoka nje kabla hajafika mbali wakampiga risasi kifuani akafia palepale.
3. Polisi waliwakuta vijana dukani wakiwa kwenye foleni ya kununua bidhaa, wakawaamrisha walale chini kifudifudi bila kujitikisha. Wakawapiga risasi za kisogoni wote kisha wakapakia maiti kwenye gari wakaondoka nazo.
4. Polisi walivamia genge la mama ntilie mmoja, wakawatawanya raia waliokuwa wakila chakula kwa kuwarushia risasi za moto. Risasi ikampata mama ntilie ikampasua kichwa akafia palepale.
5. Polisi walipita mtaani wakawakuta wanafamilia wameketi nje ya nyumba yao wanajipatia chakula cha jioni, wakwarushia risasi mfululizo na kufanikiwa kumuua baba wa familia na mtoto wake mmoja papo hapo.
Kwa mifano hiyo michache ni wazi kuwa polisi wa Tanzania hawana weledi kabisa wa kikazi. Hata kama walipewa maagizo ya kuua raia kwa risasi za moto, hakukuwa na haja ya kuwaua raia wasiokuwa na hatia kwa kuwapiga risasi ovyo. Kwa takwimu hizi za kusimuliwa na kushuhudia mwenyewe, ni dhahiri wananchi wengi waliouawa hawakuwa kwenye maandamano na wala walikuwa hawafanyi vurugu yoyote. Fikiria watu wako kwenye shughuli zao lakini wanauliwa bila sababu za msingi.
Tumekuwa tukishuhudia kwingineko duniani polisi wakituliza maandamano lakini siokwa staili hii ya polisi wa Tanzania. Inasikitisha sana. Hizi roho za wananchi wasiokuwa na hatia zilizozimwa na polisi haziwezi kupita bure.
Je, eneo ulilopo kuna tukio gani la mauaji ya ovyo uliloshuhudia? Tunataka tukusanye matukio ya kutosha ili watetea haki za binadamu na ICC wazitumie kama reference ya kuichukulia hatua serikali ya Tanzania kwa mauaji haya ya halaiki.