Ushahidi wa wazi kuwa Ali kiba anahujumiwa kwenye tuzo

SectionTwenty

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2013
Posts
675
Reaction score
611
Kwanza niseme mapeeeema mi sio team kibakuli wala team domondo...
Ok nikija kwenye point ni hivi wote tunajua kuwa mwaka huu tuzo za kili hazitakuwepo ila tuzo pekee zitazofanyika kwa hapa bongo ni EATV AWARDS zinazoandaliwa na Eatv au Channel 5.

Wadhamini wakuu wa hizi tuzo ni Vodacom na Coca Cola.. Sasa tujiulize kidogo, kuna mtu asiyejua mkataba wa diamond na Voda!?

Kila mtu anajua... Na je diamond na cocacola!?

Inajulikana wazi kuwa coca na vodacom mtu wao wanayemtumia kwa matangazo ni diamond..

Sasa hapa ali kiba atapataje tuzo mbele ya diamond..!!?

Yaani makampuni haya yadhamini tuzo halafu mtu anayetangaza brand zao wamnyime wampe mpinzani wake!!!?

Haiwezekani,yaani hapa kiba asitegemee tuzo hata moja, lazima ziende tu kwa diamond..

Kama kuna mtu asubiri hizo tuzo zifanyike halafu aone matokeo yatakuaje..
Nmeongea mapeema kabla ya tuzo ila watu wasije wakasema ni maneno ya mkosaji...

Japo mi sio team kibakuli ila kwa tuzo za style hii kiba atasubiri sana kupata tuzo...
 
 
TEAM KIBA hamnaga jipya kila saa mnawaza upuuzi tu mbona mnamtetea sana huyo jamaa na kumkandamiza platnumz ebhana mbajshtukia sana tumewachoka pumba pumba pumba!
 
Kama wewe siyo team Kibakuli basi we ndo Kibakuli mwenyewe hujatoa ushahidi bali umetoa hisia, na umeanza kulaum watu wakati hata tuzo hazijafanyika, sasa unaogopa nini!!? Au unajua kuwa hana ubavu wa kushinda!!?
Hizo lawama zenu hazimfikishi popote Kiba akae chini apige kazi
 
Upuuzi huu unavumiliwa sana siku hizi humu jamii forum,Ingekuwa zamani heshima ingekuwepo.
 
HAYA HEBU TUAMBIE IKIWA ATACHUKUA YEYE UTASEMAJE .......(bila shaka ulivyo zuzu utasema ANASTAHILI)
 
Naza mtv ni vodacom na Coca-Cola nani kwa nn hayo makampuni yasimtumie kiba au diamond ni mmiliki wa makqmpuni hayo mnajikaangiq sumu wenyewe
 
Kwani Kiba na Diamond wanafanana kwa kipi? huwezi kulinganisha maharage na nyama!
 
Tukusaidie nini sasa?kawaambie sony nao wadhamini hizo tuzo kuliko kupiga kelele huku ambako hakuna msaada
 
Mbona mnapenda kulialia kila siku? hizo tuzo hulazimishwi kushiriki bali ni wewe mwenyewe unajipendekeze...
Sasa nimeanza kuamini Kiba na mashabiki wake mmeanza kuugua vichwa...nani alikwambia Voda na Coca wanachagua mshindi? Yani mmekuwa kama watu walio changanyikiwa na mkikaribia kushindwa mnaanza kutengeneza mazingira ya kuhalalisha kushindwa kwenu.
Huu uoga mlionao juu ya Diamond hauna tofauti na mtu anaye taka kujiua..
Hivi kwani ni Lazima mshinde kila tunzo?
Mnakera sana tena sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…