Habari wana MMU, natumai muwazima ndani ya jukwaa letu pendwa.
Mimi ni kijana wa makamo niliye ndani ya ndoa sasa yapata mwaka wa tatu,na tatizo linalonikabili ndani ya ndoa yangu,nilikutana na binti mrembo ambaye kusema ukweli nilipenda sana na kuvutiwa naye hadi kufanya maamuzi ya kufunga ndoa ya kanisani,mwanzoni mwa uchumba binti huyu ambaye ni mke wangu kwa sasa alitumia sindano za kuzuia mimba kwa muda wa miezi sita mana wakati huo alikua yupo masomoni chuoni. Nilipogundua nilipiga marufuku asiendelee kuchoma sindano hizo,aliacha na tukaendelea na mahusiano hadi ndoa.
Baada yakumaliza tu tukafunga ndoa,,sasa yapata miaka mitatu mke wangu hasiki mimba ana unene uliopitliza,anaweza kaa hata miezi mitano hajaingia hedhi,anakiingia inaweza kaa hadi mwezi inatoka na inatoka mabonge mabonge,mwaka jana alishika mimba nayo ilitoka ndani ya mwezi mmoja,hadi sasa bado natafuta mtoto naye ila bado changamoto zake hazijakaa sawa.
Tumejaribu kwenda hospitali mbalimbali kubwa hapa mjini DSM tuaambiwa kuwa ni hormonal imbalance kwa sababau ya matumizi ya sindano za kupanga uzazi hivyo tukapewa dawa COC za miezi mitatu na kuambiwa tuendelea kuvumulia atatengamaa ila mpaka sasa bado.
Mimi wakati wa Ujana nilifanikiwa kupata mtoto,ambaye nikili wazi ndio faraja yangu kubwa kasasa,ingawa bado nahitaji sana watoto ndani ya ndoa yangu ukizingatia huyu mwanamke tumetoka naye mbali sana na nampenda,ila likija suala la uzao najihisi kukata tamaa na kuwaza kutafuta mwanamke mwengine anitafutiue uzao,naombeni ushauri nifanyeje na pia msaada ili kuweza tibu tatizo la mke wangu,nitashukuru sana.[emoji120]
Maamuzi nayotaka kuchukua ni either kumuacha kabisa na kuoa mwanamke mwingine au kuendelea naye huku nikitafuta mtoto kwingine,mana umri unaenda na mimi siwezi kuendelea kuvumilia.
N.B:mabinti kama mnampango wa kujenga familia na kuzaa watoto msitumie madawa ya panga uzazi kilio mnakileta kwenye ndoa.