Ushauri: Anataka kuacha kazi Serikalini sababu ya maslahi madogo

Ushauri: Anataka kuacha kazi Serikalini sababu ya maslahi madogo

The Lonnie

Member
Joined
Sep 3, 2024
Posts
12
Reaction score
26
Niulize nini faida ya kufanya kazi serikalini, kama ualimu na daktari?

Kuna mwana ni mwalimu ajira mpya mwaka jana anatamani kuacha kazi mazima ila pa kuanzia sasa ndo haelewi. Anaomba ushauri sababu haoni challenge yoyote ya maisha ikiwa hamna marupurupu na take home ni finyu kidogo.

Mazingira sio poa ni kijiji ndani huko, maduka mawili tu ya mpesa, benki mpaka utoe nauli ya elfu 6 ndio unafika.

Soma Pia: USHAURI: Niliacha kazi Serikalini kutokana na mazingira magumu ya kazi miaka miwili imepita, baada ya mambo yangu kutengemaa nataka kurudi
 
Niulize nini faida ya kufanya kazi serikalini, kama ualimu na daktari?

Kuna mwana ni mwalimu ajira mpya mwaka jana anatamani kuacha kazi mazima ila pa kuanzia sasa ndo haelewi. Anaomba ushauri cz haoni challenge yoyote ya maisha ikiwa hamna marupurupu na take home ni finyu kidogo.

Mazingira sio poa ni kijiji ndani huko, maduka mawili tu ya mpesa, benki mpaka utoe nauli ya 6k ndio unafika.
Ukiwa huna ajira utatamani nafasi ya huyu mwamba upewe wewe lakini kwa tuliotembea vijijini kuna maisha hata hiyo ajira haina maana yoyote.

Ifike wakati serikali iajili watu kutoka kwenye jamii husika wafanye kazi kwa moyo na mazingira ndio walikozaliwa hayawapi tabu
 
Mazingira sio poa ni kijiji ndani huko, maduka mawili tu ya mpesa, benki mpaka utoe nauli ya 6k ndio unafika.
Msomi ana mind set ya kuajiriwa, ameajiriwa anaona ni tofauti na expectations zake. Sehemu yenye maduka mawili ameshindwa kugeuza challenge kuwa fursa, hatutoacha kulalamika hadi hapo tutakapobadilika mind set!!
 
Huyo mwana bila shaka ndio wewe, sawa acha kazi uingie mtaani kuna marupurupu kibao.......
Huku ndio hapawezi kabisa ataishia kuamini watu ni freemason, ndinga kubwa matumizi million kama buku tu halafu huoni watu wanafanyakazi gani na wala siyo majambazi

Huku mtaani ndio kwenye matumizi ya akili winner to stay

Kuna dogo mmoja alikuwa na akili nzuri za darasani lakini sasa hivi asubuhi anaamkia visungura keshadata na degree yake kabatinim
 
First appointment nlikua(ga) bush huko, usiku nikilala ni fisi tu nasikia wanakimbia kimbia uwanjani huku wanajichekesha......
Mbaya zaidi unaweza kujikuta kwenye mahusiano na mtu siyo pigo zako kabisa.

Shem wangu mmoja aliishia kuzaa na dereva wa halmashauri halafu mume wa mtu, mpaka nikajiuliza degree mbili ndio zinakuja kuendup namna hii?
 
Ajira ya ualimu haina fedha mwanzoni. Mwambie avumilie mbele ni kutamu zaidi.
Ila mkumbushe hata akipata kazi ya ndoto yake na akalipwa mamilioni, fedha huwa haitoshi kutokana na matumizi yako lakini ukilipwa kidogo inaweza kutosha kutokana na matumizi yako pia.

"Aishi kwa malengo" zingatia Hili kuliko hayo ya juu.
 
Huku ndio hapawezi kabisa ataishia kuamini watu ni freemason, ndinga kubwa matumizi million kama buku tu halafu huoni watu wanafanyakazi gani na wala siyo majambazi

Huku mtaani ndio kwenye matumizi ya akili winner to stay

Kuna dogo mmoja alikuwa na akili nzuri za darasani lakini sasa hivi asubuhi anaamkia visungura keshadata na degree yake kabatinim
Bush mwanaume mwenye akili, ambae hana umjini mjini anaweza kufanya vitu vya maana.....kule kwanza hakuna hata matumizi ukikaa ndani na elf 50 mwezi unaisha na hela ipo, mazao bei rahisi anaweza kuwa ananunua na kuja kuuza mjini.

Kama shule ina mashamba walimu hugaiwa bure, ila ndio hadi uweze kuishi huko....ila mjini ni mjini tu jamani 😹
 
Niulize nini faida ya kufanya kazi serikalini, kama ualimu na daktari?

Kuna mwana ni mwalimu ajira mpya mwaka jana anatamani kuacha kazi mazima ila pa kuanzia sasa ndo haelewi. Anaomba ushauri cz haoni challenge yoyote ya maisha ikiwa hamna marupurupu na take home ni finyu kidogo.

Mazingira sio poa ni kijiji ndani huko, maduka mawili tu ya mpesa, benki mpaka utoe nauli ya 6k ndio unafika.
Watu wengi mpaka wanakua watu wazima hawajujui wenyewe wakati unatafuta kazi ya ualimu ulikua unatagemea nini? Kupata shule mwenge au Ubungo, alitegemea kulipwa 1m au 3m.......akili zetu bado sanaa kuchambua maisha hapo unawaza kuvuta mkopo na kukimbia ndo unataka ushauriwe ndo mwisho wa akili zenu.
 
Niulize nini faida ya kufanya kazi serikalini, kama ualimu na daktari?

Kuna mwana ni mwalimu ajira mpya mwaka jana anatamani kuacha kazi mazima ila pa kuanzia sasa ndo haelewi. Anaomba ushauri cz haoni challenge yoyote ya maisha ikiwa hamna marupurupu na take home ni finyu kidogo.

Mazingira sio poa ni kijiji ndani huko, maduka mawili tu ya mpesa, benki mpaka utoe nauli ya 6k ndio unafika.
Hata angeajiliwa sekta binafsi, huko ndo hatari zaidi... Kuna watu wanalipwa hadi laki na nusu maisha yanasonga freshi tu..

Cha msingi yeye kama msomi atumue maarifa aliyo nayo kuangalia fursa zilizopo hiko Kijiji anacho fanyia kazi... Ajiongeze asitegemee mshara tu... Ila asiache kazi maana anaweza jutia baadae
 
Mbaya zaidi unaweza kujikuta kwenye mahusiano na mtu siyo pigo zako kabisa.

Shem wangu mmoja aliishia kuzaa na dereva wa halmashauri halafu mume wa mtu, mpaka nikajiuliza degree mbili ndio zinakuja kuendup namna hii?
Sasa huko bush watu wamaana ndio hao, walimu, manesi, polisi, mtendaji kata, halmashauri ndo vibosile kabisa 😹😹😹
 
Back
Top Bottom