Ushauri: Anataka kuacha kazi Serikalini sababu ya maslahi madogo

Ushauri: Anataka kuacha kazi Serikalini sababu ya maslahi madogo

Wewe hujatembea Tanzania na kama umetembea unaishia mawilayani hufiki vijijini
Dr sehemu ina maduka mawili ya Mpesa, nauli 6k kuifikia benk hiyo ni sehemu ya kusema sijawahi kuona au kufika eneo kama hilo, u r kidding brother,
mimi niliwahi fika mahala huko Mbeya tukampa mzee lift kwenye escudo, baadae tunamshusha anauliza huyu mnamchinja akiwa na ukubwa gani? hapo ni full kinyaki anajua lile gari ni mnyama!
 
Sa usafiri wa huko nini tena ndugu, ni mwendo wa baiskeli....tena wananishawishi namie nijifunze, kimoyomoyo najisemea tu mmh na utu uzima huu nije nivunje kiungo najifunza baiskeli akaaaah!!!!
Walitaka wakuchakaze uwe mwanakijiji kabisaa
 
Ila kuna sehemu ukitupwa ni kama umelaaniwa. Hata ukiwa na pesa cha kutumia hamna.
Kila mtu amekulia mahali pake
Kuna mwamba alipata kazi as auditor wa TRA Lindi mjini aliripoti ila hakuishi kwa amani mpaka alipohama. Manispaa kabisa lakini jamaa alilia je, angepelekwa vijiji vya kuvuka kwa mtumbwi.
 
Dr sehemu ina maduka mawili ya Mpesa, nauli 6k kuifikia benk hiyo ni sehemu ya kusema sijawahi kuona au kufika eneo kama hilo, u r kidding brother,
mimi niliwahi fika mahala huko Mbeya tukampa mzee lift kwenye escudo, baadae tunamshusha anauliza huyu mnamchinja akiwa na ukubwa gani? hapo ni full kinyaki anajua lile gari ni mnyama!
Acha uongo wewe mtu mzima asijue kwamba gari sio mnyama acha kutupiga kamba.
 
Sijaona sababu mahsusi zinazomfanya huyo jamaa aache kazi maana hata Mimi mwalimu niliyeko kazini nimeanzia vijijini ,mimi nakumbuka ajira yangu ya kwanza ilikuwa ni Lindi- liwale vijijini ndani kabisa,ukifika simu unazima unabaki kumulikia tochi tu kuwasiliana na ndugu Hadi uende mjini nauli ni sh 12 kwenda tu, yeye huyo jamaa Yako anaona 6K lakini baadaye nikafanikiwa kusogea mjini.

Sasa kama Hoja yake ya kuacha kazi ni mazingira magumu huyo jamaa kashafeli tayari kwani bado ana nafasi kubwa ya kubadilisha mazingira akarudi kwenye maeneo anayoyataka na akaendelea na ajira yake ya ualimu. Lakini pia kuhusu hoja ya mshahara,mimi nadhani mshahara ni mkubwa kama ni graduate mshahara wake unaanza na laki 7. As basic,na takehome zaidi ya laki 5 hiyo ni pesa kubwa sana.

Lakini siku zote ajira za serikalini mshahara sio kwa ajili ya kufanya maendeleo makubwa hasa Kwa kazi zetu za ualimu,mshahara hutosha kwan mahitaji ya chakula kunywa na kulala. Sasa kama anataka kujiongeza kiuchumi basi atumie mshahara wake Kukopa ,kuna mikopo kwa mwalimu anayeanza na. Mshahara wa wa Hadi 20M sasa,hivyo akope aweze kuitumia kuiwekeza kwenye biashara zingine sio kutegemea ualimu ,atengeneze mwenyewe posho yake asitegemee posho za serikali ,posho Kwa Ajira ya ualimu ni ngumu .

NB.hakuna mkate aongee na afisa elimu wake Kwa herufi kubwa ioi amuhamishie mjini ndani ya wilaya yake,Nb elewa neno herufi kubwa
 
Ila kuna sehemu ukitupwa ni kama umelaaniwa. Hata ukiwa na pesa cha kutumia hamna.
Kila mtu amekulia mahali pake
Kuna mwamba alipata kazi as auditor wa TRA Lindi mjini aliripoti ila hakuishi kwa amani mpaka alipohama. Manispaa kabisa lakini jamaa alilia je, angepelekwa vijiji vya kuvuka kwa mtumbwi.
Huyu amenyeka, hajakutana na mazingira magumu, hapa tunaongelea vijijini, ukitaka kuangalia mpira kibanda umiza au kunywa bia nauli kwa bodaboda 20,000 kwenda na kurudi
 
Msomi ana mind set ya kuajiriwa, ameajiriwa anaona ni tofauti na expectations zake. Sehemu yenye maduka mawili ameshindwa kugeuza challenge kuwa fursa, hatutoacha kulalamika hadi hapo tutakapobadilika mind set!!
Sio rahisi hivyo kuna vijiji ukianzisha kitu ni kama umetangaza vita ya jadi hata usingizi upati tena full vibwanga..
 
Mwanangu kasomea india udaktari wa moyo kafanya intership jakaya kaona wafanyakazi walivyo na roho mbaya humo jakaya na kujipendelea kaangalia mshahara kaona nayenyewe ovyo, kagoma kumalizia intership hataki kabisa anasema bora akafanye biashara yoyote ile tumebembeleza sana kagoma
 
Utete iko wapi?? 😁
HahahahaaHa imagine hio ni Wilaya iko mbele kushoto ya Ikwiriri, unapita daraja la mkapa, unafika eneo kuna junction panaitwa Nyamwage unapinda kulia unaacha njia ya Lindi!

Miaka Ile ilikua ni bus la Kampuni ya Tokyo Takara au uende Hadi Kibiti ukifika unaenda kupanda kivuko Ndio unafika hio Nchi!
 
Mwanangu kasomea india udaktari wa moyo kafanya intership jakaya kaona wafanyakazi walivyo na roho mbaya humo jakaya na kujipendelea kaangalia mshahara kaona nayenyewe ovyo, kagoma kumalizia intership hataki kabisa anasema bora akafanye biashara yoyote ile tumebembeleza sana kagoma
kama namjua vile jina linaanzia na S linaishia K? anapenda sana kucheza Golf now days?
 
Ushauri wa kuacha au kutoacha nashindwa kuutoa ikiwa sijui yuko kijiji gani. Kuna maeneo ni kijijini sana lakini mtu mwenye kamtaji kidogo tu anaweza kufanya mambo mengine mengi na akapiga pesa safi hadi akasahau kurudi mjini. Ni vizuri tukijua yuko mkoa gani, wilaya gani na kijijini gani, inatosha hata asipotaja shule for privacy.

Mara nyingi usiache kazi kama hujapata kazi (kwa maana ya kazi kama kuajiriwa au kujiajiri) na kwamba hiyo kazi nyingine inaweza kukusustain for angalau miezi sita.​
 
Back
Top Bottom