Ushauri: Anataka kuniharibia penzi langu jipya, nifanyeje?

Ushauri: Anataka kuniharibia penzi langu jipya, nifanyeje?

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Jana usiku katika kusherehekea mambo ya muungano, ikabidi nitoke na bebi wangu tukaenda kiwanja kimoja; tukawa tunapiga maji yetu machungu kama kawaida yetu.

Kutokana na mazingira kuwa na 'vibe' wengi walikuwa wakiingia na kutoka, kwa bahati mbaya kuna mdada mmoja nilikuwa nimemzoea kipindi cha nyuma, ila sina mahusiano naye; ila kwa kilichotokea jana nimegundua ana hisia na mimi.

Baada ya kulewa sana, ikabidi niondoke na mpenzi wangu kurudi nyumbani; tukabiga shoo zetu kabambe kama mnavyojua equation x huwa hazembei kwenye hayo mambo.

Mtoto akawa analia, anasema,'' equation x uwe unanipa kila siku, na usimpe mwingine; nenda spidi hivyo hivyo usimwage bhana''.

Kutokana na maneno hayo, huku akitoa kwa sauti ambayo sijaizoea, nikaona kama vile muumba amenipendelea.

Wakati nipo napumzika (half time) mida ya saa nane na nusu usiku, ujumbe ukaingia kwenye simu yangu kutoka kwa yule dada, ukisema; ''equation x uko wapi kuna tatizo limetokea linakuhusu wewe mwenyewe tu jitahidi unione sasa hivi''

Nikauliza tatizo lipi na linahusu nini?, akanijibu si vizuri kuongelea au kuchat kwenye simu we njoo tu.

Nikamwambia bebi wangu, nimepata ujumbe hapa nashindwa kuuelewa, ebu amka twende tukausikilize; kutokana na bibie kuwa amechoka, akaniambia we nenda tu utanijulisha.

Mi nikawa na wasi wasi, ni kitu gani kimetokea? Ikabidi nimshtue jamaa yangu wa karibu, nikamwambia ebu twende eneo x nimepata ujumbe nina mashaka nao, jamaa akasema poa.

Nikachukua kasalio kidogo, nikaenda sehemu husika; mara namkuta yule mdada yupo peke yake anapata kinywaji; nikamuuliza kulikoni kuniita huo usiku wa manane.

Akasema nimekumis tu na nina hisia na wewe; nilitamani nimzabe vibao, lakini akili nyingine ikaniambia mtu akikuambia hisia zake ni vizuri pia kuzi heshimu; basi nikaagiza maji na juisi yeye akawa anapiga zake pombe.

Muda haujakaa sawa, rafiki wa bebi wangu alikuwa pale akaniona na kunifuata mezani na kuniuliza, ''bebi mama umemuacha wapi?''

Nikamjibu yupo nyumbani amepumzika, amesema hawezi kutoka tena; akaniuliza, ''na hapa unafanya nini?'', nikacheka tu; ikabidi nimnunulie savana 2 akaondoka.

Sasa leo asubuhi imekuwa ni siku ya kusuluhisha migogoro; hapa nilipo sina uhakika kama nitapewa shoo jioni.

Mbaya zaidi, niliwatambia humu, nimepata mpenzi mwenye sifa zilizopitiliza.

Wakuu nipeni ushauri​
 
Basi kama hutojali na unamjali shemeji yetu nipasie namba za huyo msumbufu nami nimsumbue asiharibu penzi lenu la kunywa vitu vikali
Sawa mkuu, nakutumia muda si mrefu; jitahidi umfundishe adabu ki kweli kweli 😀
 
Back
Top Bottom