Uzoefu unaonesha kwamba mchakato wenye Tija zaidi nzuri zaidi ni (a) Kwanza Binti mwanafunzi amtambue fika Mhusika i.e. awaambie ni nani mwanaume mhusika, halafu ndo: 1. wasilianeni kwanza na Mwanaume mhusika kama anakubali Mzigo wake, 2. Wasilianeni na Wazazi wa mwanaume mhusika na mkubaliane nini cha kufanya hususan malezi ya mimba hadi mtoto-mtarajiwa akizaliwa salama. 3. Msijaribu/Msikubali kamwe hoja ya kutoa mimba (Mnaua kitoto kisicho na hatia na hakiwezi kujitetea- Ni dhambi kubwa mno).
Aidha katika majadiliano yenu pande zote mbili zingatieni kwamba suala/Hoja ya Uanafunzi, binti anaweza kuahirisha masomo kama ni chuo, kubadilisha shule (Sekondari)baada ya kujifungua au binti anaweza kuhiari kuachana na masomo na kuolewa Rasmi i.e. kuanza maisha ya Ndoa yaani kuwa na Familia.
Mwisho nakushauri kwamba Hoja ya Hatua za Kisheria mara zote hazinaga Tija kwani utapoteza JUMLA (Hakuna maslahi yoyote kwako wala kwa binti wala kwa Kidume-husika) e.g. kwani Kidume mhusika akifungwa miaka 30 ww mzazi utapata nini? Kidume mhusika kama ni mtumishi atafukuzwa kazi mazima na kwenda kutumikia 30yrs na hivyo Hataweza tena kutoa msaada wowote kwa binti wala kwako ila ww utalazimika kulea mimba & mtoto(Mjukuu) hadi hapo baba yake atakapotoka Jela. Kwa kifupi kwenye Sheria, Binti atapoteza masomo kwa kufukuzwa shule, Ww mzazi wa binti utapoteza kwa kuingia gharama kubwa ya kulea, Kidume atapoteza kwa kufungwa 30yrs. Ila kama ww unataka kutoa Adhabu kali, basi nenda kwenye Sheria. Lakini kama nia yako ni njema au ni kuweka njia muafaka kukuza na kudumisha mahusiano kati ya familia za pande mbili - yamalizeni nje ya Mahakama.