USHAURI: Binti mwanafunzi wa miaka 18 apata ujauzito, tufanye nini?

Asante sana boss kwa ushauri mzuri. Kijana kakubali mzigo na tunaangalia taratibu nzuri waende zao wasitusumbue tena.
 
Lawama za kumchunga au malezi usizitoe wakati huu. Pengine hujawahi kuwa na watoto katika kizazi hiki.
 
Ndio hapa tungependa kujua kisheria kipi kinahesabika kikubwa kati ya uanafunzi au utu uzima wa miaka 18
Sheria inasema ukimpa mimba mwanafunzi ni miaka 30 ndani.

Swali ni...

Je mkienda mahakaman alafu binti akawageuka? Yaani akasema huyo sio baba!

Je mkimfunga huyo jamaa huoni kama mtoto atalelewa bila baba?

Hali kama hii wanavyo fanya watu ni kichukua mahari na kuwafungisha ndoa.. ila ujue ukifanya hivyo shule ndio imeishia hapo na kama huyo baba mtarajiwa hajielewi mtakua mnasovu kesi kila siku! Kwa kifupi kama huyo jamaa hampendi binti (kuna uwezekano mkubwa ikawa hivi maana tayari kesha mbebesha mimba) mjiandae kwa vimbwanga!
 
Mwanafunzi wa shule ya msingi, sekondari au chuo?.

Kama ni wa msingi au sekondari hizo ni jinai na jinai zinaripotiwa kwa vijana wa IGP N. Sirro

Ila kama ni wa chuo, mkazanieni kuwahi clinic kwanza mengine yataji sort tu baadae.
Huyu ni kidato cha tatu. Hii njia ya kwa Siro sioni kama inakuwa na tija kwa yeyote.
 
Hoja ya kumuozesha ndio inapewa nguvu zaidi na wanafamilia. Kijana amemkubali binti na mwanae mtarajiwa.
 
Mimi sio mwanasheria wala sijui chochote kuhusu sheria labda wanasheria watufafanulie hili swala:

Hivi serikali inapomfunga baba wa mtoto miaka 30, yenyewe (serikali) inachukua jukumu gani au inachangiaje kwenye malezi ya huyo mtoto na mama wa mtoto? Kuna fungu flani labda limetengwa la kulea watoto wa dizaini hiyo au jukumu hilo linarudishwa tena kwa wazazi wa binti aliopewa ujauzito?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] hatareee tupu yaan.
 
kama hajabakwa, itakua ni kiherehere chake.
Kwani hata binti mwenyewe anajua kufanya matusi ni makosa. Na vibinti vya siku izi vinavyojua baikoko kuliko hata makungwi.
Iyo ya kumpa mimba tu tayari ni kosa la kufungwa miaka 30
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…