Ushauri bure kwa Kesi yoyote ya Madai au Jinai

Ushauri bure kwa Kesi yoyote ya Madai au Jinai

Mimi nataka kujua haki za raia kipindi unatamatwa na polisi,
Na ukifikishwa kituoni kipi kinatakiwa nifanye na nisifanyiwe nini? maana kuna kupigwa siunajua wengine hatujui kunyenyekea na polisi wanapenda tuwaone superior.
 
ndio, hua kuna ukomo katika mirathi, kwa mfano marehem akifa alaf ndugu wa marehemu wakashindwa kufungua mirathi mahakamani ndani ya muda wa miaka mitatu toka kifo cha marehemu, basi mali za marehemu zitachukuliwa na kua chini ya uangalizi wa administrator general, so ukomo ni miaka mitatu toka kifo cha marehemu... njia za kuongeza muda na kurudishwa mali chini ya uangalizi wa wanandugu baada muda wa sheria kupita, ni maombi mapya yanayoweza kufanywa na wanasheria.
Haina ukomo mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haina ukomo mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
ka kwambia nani kua hakuna ukomo? okei iko hivi, haki ya kusimamia mali za marehemu almaarufu kama mirathi ni lazima ithibitishwe na mahakama aidha marehemu awe ameacha wosia au hajaacha,vyote ni mahakama ndio itathibitisha au ita teua kutokana na mapendekezo ya ndugu wa marehemu, hatua hii huitwa application for letter of probate or application for granted probate, sasa kwa mujibu wa sheria za mirathi maombi haya yanapaswa kufanyika ndani ya miaka mitatu toka kifo cha marehemu, na muda huu ukipita basi admistrator general atapaswa kuziweka chini ya uangalizi wake mali hizo mpaka pale ndugu wa marehemu watakapo jitokeza na kuomba wapewa ruhusa na muda kuongezwa wa mahakama.
 
Wakili,hii huduma ingekua kila mwisho wa wiki ingependeza sana, pale juu mwanzo kabisa nilikuuliza nikimuwekea dhamana mtuhumiwa polisi au mahakamani je naweza kufungwa? Au nichukue hatua zipi kukwepa mkono wa sheria?

Sent using Jamii Forums mobile app
ntaangalia kwa kadri ntakavyokua napata nafasi... nimekujibu swali hili angalia hapo juu.
 
Mimi nataka kujua haki za raia kipindi unatamatwa na polisi,

Na ukifikishwa kituoni kipi kinatakiwa nifanye na nisifanyiwe nini? maana kuna kupigwa siunajua wengine hatujui kunyenyekea na polisi wanapenda tuwaone superior.
haki ni nyingi mkuu, siwezi kuziandika hapa zote, lakini muhimu ni kuakikisha unatoa maelezo kwa muda usiozidi masaa manne, kuwekwa ndani muda usiozidi masaa 24, lakini kutoa maelezo kituoni hapo ktk hali huru, chini ya mwanasheria au ndugu yako, kuelezwa kosa ulilokamatiwa nalo, kuakikisha unasaini document zozote zile ambazo unaufahamu nazo na zimetokana na maelezo, endapo watakupiga na kukufosi usaini maelezo waliyo yatoa wao na wakakulazimisha uyasaini basi unaweza kukubali tu kwa kuepuka kuumizwa sanaa na utakuja kuyakana mahakamani kua hayakupatikana kwa ridhaa yako.... muhimu ni kumbuka endapo utaratibu huu utavurugwa na hao polisi basi itakua ni moja ya ticket ya kukuacha huru ata kama kosa ulilifanya kweli, kuna watu kweli waliua ila mahakama iliwaachia huru kutokana na polisi kushindwa kufuata maelekezo ya sheria.
 
Asante sana. Je ukiwa hauna mali za kufidishia kilichobaki?

Sent using Jamii Forums mobile app
hii hua ni mtihani sana, na hapa ndipo wakopeshaji wanapoliaga, kikawaida inashauriwa kumkopa mtu ambae kama atashindwa kulipa deni husika basi awe atleast ata na mali ambayo inaendana na pesa aliyokopa, ndio maana utaona ma bank mengi yanafanya assessment za nyumba kwanza zinazowekwa bond, isije mtu akakopa milion 50 kumbe nyumba ina thamani ya milion 10 tu.
 
Mkuu kama kwa mtumishi wa umma ni kitu gani ama ni kosa gan ama shitaka gan litakalo mpa mamlaka mwajiri wako kukutaka maelezo ndani ya masaa 24?
mkuu watumishi wengi wanakua chini ya sheria ndogo ndogo za almashauri husika, sheria ya umma imeruhusu taasisi za kiserikali kutengeneza sheria ndogo ndogo ambazo zitacontrol mahusiano makazini na nidhamu za wafanyakazi, uenda huyo mwajili wako ametumia sheria moja wapo kati ya hizo, na ingekua vizuri pia kupitia sheria za taasisi husika uliyopo, uenda kuna kifungu kimempa mamlaka hayo uyo afisa utumishi.
 
haki ni nyingi mkuu, siwezi kuziandika hapa zote, lakini muhimu ni kuakikisha unatoa maelezo kwa muda usiozidi masaa manne, kuwekwa ndani muda usiozidi masaa 24, lakini kutoa maelezo kituoni hapo ktk hali huru, chini ya mwanasheria au ndugu yako, kuelezwa kosa ulilokamatiwa nalo, kuakikisha unasaini document zozote zile ambazo unaufahamu nazo na zimetokana na maelezo, endapo watakupiga na kukufosi usaini maelezo waliyo yatoa wao na wakakulazimisha uyasaini basi unaweza kukubali tu kwa kuepuka kuumizwa sanaa na utakuja kuyakana mahakamani kua hayakupatikana kwa ridhaa yako.... muhimu ni kumbuka endapo utaratibu huu utavurugwa na hao polisi basi itakua ni moja ya ticket ya kukuacha huru ata kama kosa ulilifanya kweli, kuna watu kweli waliua ila mahakama iliwaachia huru kutokana na polisi kushindwa kufuata maelekezo ya sheria.
Asante sana mwana sheria mkuu wa JF, napenda kujifunza vitu vingi nilikua naomba huu uzi uwe endelevu siku zisizo zawiki utujibie maswali ya kisheri.
 
Back
Top Bottom