Uchaguzi 2020 Ushauri - CHADEMA iongezee Timu ya kampeni na Lissu aende Majimboni

Uchaguzi 2020 Ushauri - CHADEMA iongezee Timu ya kampeni na Lissu aende Majimboni

Too late...halafu hamna vichwa vinavyoeeza kusimama vyenyewe kwenye kampeni
Hivi hapa vichwa.
1. John Heche
2. John Mnyika
3. Halima Ndee
4. Mhe. Msigwa
5. Mhe. Sugu ( Rais wa Mbeya)
6. Lazaro Nyarandu
7. Godbless Lema
8. Prof. J ( Mbunge wa binadamu na wanyama)
9. Ester Bulaya & Ester Matiko
10. Jacob Biniface ( Meya Ubungo)
Kamanda wa anga atacheza popote.
Hawa wanamvuto wa kutosha. Haihitaji lwasanii kujaza uwanja. Nadhani wanasubiri dakika za lala salama wanajiweka sawa kwanza majimboni.
 
Ukiangalia kiundani unaona kwa nini CCM inaweza shinda uchaguzi huu kiurahisi sana.

Ni namna walivyojipanga katika Kampeni zao. Kila Mkoa na Wilaya unaona kuna mtu mwenye Ushawishi ndani ya Chama anasaidia kufanya kampeni za wagombea Ubunge au Udiwani. Nimeona Kinana, Kikwete, Ndugai, n.k. wafanya kampeni.

Chadema hapa wamekosa nguvu fulani. Kampeni na mikutano yote inahodhiwa na Lissu tu. Bila Lissu hakuna watu. Katika Jimbo la Bunda nimeona mwamko zaidi kwa wanachama na wapiga kura wao. Mbeya na Arusha nadhani pameamka.

Nashauri timu ya kitaifa iongezeke. Itawanyike nchi nzima na tuone nguvu ya chama na si mtu.
Nenda kamshauri mgombea wenu aliye bwaga manyanga na sasa yupo kwao amepumzika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom