Umenena......Kuna "kisebule" changu huwa napoa karibu na home baada ya mishe mishe zangu basi bwana mwaka jana mwanzoni wakatuletea kitoto kidogo kutoka huko mbulu, mtoto kanyooka balaaa, kifua kinaita chuchu saa sita, huko nyuma kafungasha hatariii, mtoto nyama nyingiiiii, basi bwana habari zikawafikia wakware, wakawa hawakauki "sebuleni" kwetu mtoto demand ikawa kubwa offer za beer za kutosha binti akatoka kunywa Serengeti lite akaamia kwenye windhoek, Savannah kama huna offer yake ya Savannah tatu, nne basi usijiangaishe, watu wakawa wanapanda dau, akataka macho matatu wakware wakanunua.
Mtoto akazidi kupendeza , sifa na uzuri wake zikavuma mpaka anga za mbali, wadau na wakware maarufu wakahamia sebuleni kwetu na kuweka kambi mpya, sebule yetu ikaanza kuonekana ndogo, hata sisi wenyeji ikabidi tuanze kunywa kwenye seat za gari, pesa ikamwaga mtoto akaanza kumwaga utamu Kama hana akili nzuri, mji ukamchanganya, pesa zikamlevya.
Well to make a story short now ni mwaka mmoja umepita, mtoto wa watu kachuja vibaya Sana, wakware wamemchakaza vibaya Sana, kakosa nuru, nadhani ana udongo mbaya huyu binti maana imekuwa haraka mno, masikini hata kile kifua kizuri Cha mvuto hakipo tena, kachoka masikini, kachunda, habari za hapa sebuleni Ni kuwa binti kaukwaa, wengine wanasema ametoa mimba vibaya, maneno ya binadamu ni mengi hata wale wakware wamemkimbia na kuamia bar nyingine wenyeji tumebaki sebuleni kwetu kwakuwa ndio nyumbani, Sasa hata tunakaa kwa amani, ooh nimesahau mrembo wetu amerudi kwenye Serengeti lite now zile Savannah hakuna tena.