USHAURI: Familia ya Hayati Magufuli iende Mahakamani kudai fidia ya picha iliyotumika katika kava kukitangaza kitabu cha 'I Am The State'

Hahaha umepanic?

Maandishi Hayapingwi kwa chuki mzee unapaswa uandike kitabu chako kuyakana au kueleza tofauti na yaliyoelezwa mule. Vinginevyo ni UJUHA wa kulazimisha mambo?

Lakini una huo utamaduni wa kusoma VITABU hata hiki kiwe cha pili?
 
Nchi hii watu wake wanatamani Yale ya Sudani eee mwenyezi Mungu tuhepushe na wazandiki.
 
Ukishakuwa Rais MTU yeyote anaweza kuandika kitabu chochote ilimradi havunji sheria na familia ya Rais isidai chochote kama fidia...
Acha kudanganya watu wewe,ujinga wako peleka huko. Hutakiwi kuandika kitu juu ya yeyote yule bira kubalance, Rais ni Mali ya umma ni nembo ya nchi,ndio taaswira ya Taifa, huwezi kumchafua kiongozi wa nchi bira kuidharirisha na kuibagaza nchi.huwezi kuitwa rais bira taasisi ya urais kuichafua.
 
Hahaha umepanic?
Maandishi Hayapingwi kwa chuki mzee unapaswa uandike kitabu chako kuyakana au kueleza tofauti na yaliyoelezwa mule. Vinginevyo ni UJUHA wa kulazimisha mambo?
Lakini una huo utamaduni wa kusoma VITABU hata hiki kiwe cha pili?
Uandishi una kanuni zake mkuu,na kiongozi mkuu wa nchi ni Mali ya umma,hairuhusiwi tu kila mtu akurupuke kuandika upumbavu wake bira mamlaka kuhariri kazi yake.
 

Unajua maana ya kumchafua MTU?

Kuandika habari au hadithi ya kweli ya Matendo mabaya ya Rais kama alifanya kweli tangu lini ikawa kumchafua Rais?

Kitu MTU kama hajafanya na ukamuelezea Kwa ubaya ambao hajafanya ndio kunaitwa kumchafua, pia ni kosa kisheria kama atakushtaki.

Mtu kumsifia Kwa Jambo ambalo hajalifanya hiyo inaitwa Kumpaka MTU Kwa mgongo WA chupa, pia unaweza kushtakiwa Kwa kuzusha Uongo.
 
Kwa hiyo Membe ka7bisha ubadili jina kutoka mwanaharakati huru kwenda mwanaharakati mwema?
 
Uandishi una kanuni zake mkuu,na kiongozi mkuu wa nchi ni Mali ya umma,hairuhusiwi tu kila mtu akurupuke kuandika upumbavu wake bira mamlaka kuhariri kazi yake.
Bora = bila
Unafikiri nn kibaya pale kilichoandikwa ambacho umma hautakiwi kujua?
Aakija muandishi kesho akiandika kitabu cha kumsifia magufuli utataka hicho kitabu nacho kihaririwe?
 
M
Moyoni mwako.
 
Pole sana ila ni bahati mbaya kwamba ukishakuwa kiongozi unakuwa public property kwa yote unayofanya ukiwa ofisi ya umaa. Picha zote alizopiga akiwa raisi ilmradi sio katika privacy zake ni mali ya umma.
 
Ansbert Ngurumo si anamzungumzia "JIKONO JANDAMA"? Picha inaendana na context.
 
Unapoint hapa. Wakishindwa walinda legacy tutaenda
 
Kama Kuna walioandika mabaya ya mwendazake hawana kosa ni haki yao na uhuru wao, pia na ww upo huru kuandika mazuri yake hamna wa kukuzuia

Mara nyingi kama ulifanya kazi kubwa na inayoonekana hata uandikwe vibaya kiasi gani bado legacy yako itaishi ndani ya nchi mfano mwalimu Nyerere ameacha legacy yake nzuri tu wapo wanaojaribu kupotosha kuhus mwalimu Nyerere mfano mzee Mohamed Said lakini bado mema ya nchi yanaishi
 
Bira= bila?
Ulishafanya research popote pale kwenye maishani mwako???
Usilazimishe yasiyowezekana bhana.kingeandikwa kitabu cha kusifia ungeuliza haya yote?
Uhuru wa habar ni oamoja na kusikia usiyopenda kusikia wewe bwana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…