Ushauri gari nzuri ya familia

Ushauri gari nzuri ya familia

Wakuu michango yenu mizuri sana, naomba tuwe tunatoa ufafanuzi japo kiduchu kuhusiana na magari tunayotaja kwani si wote wanautaalamu wa magari hasa mimi. Asante !
 
Wakuu naomba ushauri juu ya gari zuri la familia linaloweza milikiwa na mtu wa kipato cha chini. Liwe na uwezo wa kubeba watu 5. Gharama yake isizidi milioni 14. Picha zitasaidia zaidi.
Mkuu pamoja na magari yote waliyoshauri wenzangu hapo juu mimi nakushauri chukua Toyota GAIA, ina cc 1990, ina seat 8 hutojuta
 
Bajeti inareflect hata uwezo wa maintenance baada ya umiliki...toyota raum new model itakufaa,fuel economical spare parts easy to get en price za kawaida...ukitaka gari ya juu chukua kilitime
 
Mkuu pamoja na magari yote waliyoshauri wenzangu hapo juu mimi nakushauri chukua Toyota GAIA, ina cc 1990, ina seat 8 hutojuta
Mkuu kwa uzoefu wangu GAIA ina ubovu wa shockup, na body yake huinama mapema. Yaani ikishaanza mapicha kila siku utakuwa garage.
 
Hapa nakuunga mkono
Naitumia kifamilia mwaka wa 3 sasa, ukizingatia wazazi wangu na wakwe zangu wapo vijijini. Hivyo siku nakwenda kuwasalimu nachukuwa watoto wangu 2, mdada wa kazi, kajomba zangu, shem angu na wife. Na mazagazaga machukua full amani
 
Barabara si mbaya sana japo nahitaji gari inayovumilia hali zote.
1200px-Toyota_Probox_Van_DX.jpg

TAFUTA HIYO
INAITWA PRO BOX
 
Nunua Harrier old model hutojutia
Sijui kwanini watu wanaogopaga hizi mashine, wanaishia kununua stress.... for the budget sake, i can understand... otherwise Harrier 2.4 ni gari nzuri saaaanaaaa......
Fuel consumption inatofautiana mtu na mtu kwenye matumizi ya chombo....
 
Back
Top Bottom