Ushauri: hakikisha una mganga mzuri kabla ujaenda oral interview yeyote ya utumishi

Mganga pekee ni Mungu.
Me nimeanza hizi harakati za ajira za serikali mwaka huu.mpaka sasa nishapiga written 3,kati ya hizo nimeingia oral moja ndio nasubiria majibu yake yatoke.
Tumtumainie Mungu pekee
Upo sahihi mkuu. Mungu pekee ndiye anaweza kukuvusha. Pale unapohisi huna tena namna na umekata tamaa ndipo Mungu anakuinua. Kikubwa ni kupambana bila kuchoka. Pia marafiki wema na watu wanaokupa hamasa ya kusonga mbele sio wa kupuuza.
 
Kwa hiyo unataka uwaroge/mzingaombwe wasahili ili wasione na kusikia kutokujua kwako?! Sijaelewa.
 
Ingekuwa hiyo mbinu Ina work out sifikirii Kama kungekuwa na jobless kwa kuanza na familia za hao waganga
 
Ingekuwa hiyo mbinu Ina work out sifikirii Kama kungekuwa na jobless kwa kuanza na familia za hao waganga
Mkuu Umefanya case study ipi nchini ambayo imepitishwa na maprofesa kua nyumba zote wanazoishi waganga vijana wanaotafuta kazi wamepata ama hawajapata..
 
Siyo kuhusu case study tu, inawezekana ni mtoto wa mganga ila wakati wa interview anajiandaa vema na anapita na sio kusikia maneno tupu ya mlezi au mzazi wake ambae ni mganga, kupita interview ni kujiandaa vema
 
Hii inawezekana?
 
Nakuunga mkono mkuu, bila connection niliganikiwa kuingia oral tano, na katika hizo tano, oral interview moja ikaniingiza kwenye utumishi wa umma
Iliotiki ni ya mganga au connection?
 
Anaehitaji mganga mzuri....pm
Sioo kweli kaka ,ila Kila mmoja na Imani yake ,ety bila mganga hutoboi oral utumishi ,mtegemeeni Mungu tu ndioo Kila kitu na wakati wako ukifika unapata kazi vizuri tu ,ushuhuda ni Mimi mwenyewe Sina mtu ninae mjua serikalini Wala kwenda kwa mganga ,ila nilimtumaini Mungu na kusoma vizuri bhasi Mungu atakupa kibali ,na hadi Sasa Mungu kanipa kazi huko huko serikalini . Yote kwa yote Kila mtu na Imani yake .
 
Wewe ndio mganga mwenyewe umekuja kutafuta wateja? Msomi anayeenda kwa mganga kufaulu usaili sidhani hata kama ana uwezo wa kufanya hiyo kazi kwa ufanisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…