Ushauri: Ianzishwe Wizara ya Mafuta na Gesi ili kuchochea ukuaji wa sekta ya mafuta na gesi Tanzania na Waziri awe Profesa Muhongo

Ushauri: Ianzishwe Wizara ya Mafuta na Gesi ili kuchochea ukuaji wa sekta ya mafuta na gesi Tanzania na Waziri awe Profesa Muhongo

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Hii wizara iwe responsible kwenye mambo ya utafutaji (exploration), uzalishaji (production), usafishaji (refining), usambazaji (distribution), uuzaji (marketing), kuingizaji kutoka nje ya nchi (import), na utoaji kwenda nje ya nchi (export), pamoja na conservation of petroleum, natural gas, petroleum products, and liquefied natural gas Tanzania.

Maeneo muhimu ambayo ningependa hii wizara ihusike nayo ni haya yafuatayo.

1. Exploration and exploitation of petroleum resources, including natural gas (methane, helium)

2. Production, supply distribution, marketing and pricing of petroleum including natural gas and petroleum products.

3. Oil refineries, including Lube plants and natural gas plants.

4. Natural gas utilization to get valuable products.

5. Additives for petroleum and petroleum products.

6. Lube blending and greases.

7. Planning, development and control of, and assistance to all industries dealt with by the Ministry.

8. Planning, development and regulation of gasfield and oilfield services.

9. Administration of various Central laws relating to Petroleum and Natural Gas.

Ningependa wizara ya nishati ishughurikie mambo ya kuzalisha, kusambaza na kuuza umeme.

Ishughurikie uzalishaji wa umeme kutoka vyanzo mbalimbali mfano maji, gesi, joto ardhi, upepo, jua, mawimbi ya bahari n.k.

Huo ndio ushauri wangu,
Ninahisi ikiwa hivi tutaipunguzia wizara ya nishati mzigo, na tutaongeza ufanisi na ukuaji katika sekta ya mafuta na gesi Tanzania.

Nina imani Prof. Muhongo amejifunza hawezi kufanya ujanja tena. Nimempendekeza yeye kwasababu bwana Muhongo ana passion na mambo ya mafuta na gesi kwa hivyo atafanya kazi kwa bidii ili kuendeleza sekta hii Tanzania.

Karibuni kwa maoni.
 
Professor Mhongo amepewa hipe ya uwazir wa nishati tangu Zama za kikwete mpak Maghufuli , na mara zote ameishia kufukuzwa kazi ..... Prof akili anayo Ila Hana juhudi ya uwajibikaji
 
Professor Mhongo amepewa hipe ya uwazir wa nishati tangu Zama za kikwete mpak Maghufuli , na mara zote ameishia kufukuzwa kazi ..... Prof akili anayo Ila Hana juhudi ya uwajibikaji
Ni vyema ukaorodhesha ni eneo lipi ambalo hajawai kuwajibika mkuu.
 
Tatizo sio idadi ya wizara

Tatizo ni ufanisi

Wazo lako kwamba linatia hasara nchi, ule mtazamo usio na maana wa kudhani Kila changamoto inatakiwa itatuliwe kwa kuongeza mizigo kwenye muundo na mfumo wa serikali
 
Naona sasa mnataka kuiuza nchi jumla jumla
 
Mtoa mada upo sahihi.

Tungekuwa na wizara ya nishati na madini lkn haina ufanisi, mawaziri wakipewa hiyo wizara wao wana fikiria upigaji tu ktk mikataba mibovu...

Uwepo wa wizara ya mafuta na gesi na malengo chanya inaweza kuleta maendeleo na wakapimwa kwa kile wanachofanya....
 
Mtoa mada upo sahihi.

Tungekuwa na wizara ya nishati na madini lkn haina ufanisi, mawaziri wakipewa hiyo wizara wao wana fikiria upigaji tu ktk mikataba mibovu...

Uwepo wa wizara ya mafuta na gesi na malengo chanya inaweza kuleta maendeleo na wakapimwa kwa kile wanachofanya....
Huu ndio ukweli mtupu, hizo sekta za umeme, mafuta na gesi ukizichanganya mawaziri wengi huegemea kwenye umeme na mafuta yanayoagizwa nje ya nchi kwasababu ni kurahisi na kuna hela za wazi kabisa lakini huku kwenye kuendeleza utafutaji wa mafuta na gesi nchini kunakua kunapwaya.
 
Prof. Muhongo hata mwendazake alimlaani. Huku musoma anatumia mamilioni ya Rushwa kupata ubunge. Akifika dodoma kazi ni moja tu,kusinzia bungeni
 
Hatufai, huo profesa wake aende akafundishe vyuoni huko ila siyo kwenye uongozi! Narudia tena haifai kabisa!!

Atauza mali asili zote tubakie watupu!! Kama amekutuma kumpigia debe mwambie hafai kuwa waziri!

Alishapewa hiyo wizara akachemsha!!
 
Muhongo? Seriously?
Unamjua vizuri?

Mtu dalali wa vitalu vya mafuta ..
Aliewekwa mifukoni na wawekezaji matapeli ndo unakuja kushauri hapa??
 
Back
Top Bottom