Ushauri: Iundwe Kamati huru kubaini chanzo cha nyufa JNHP maana kuna harufu ya uhujumu uchumi

Watanzania bana,
Walalamishi sana sisi,
Mradi haujaisha Wala mtu Hana details za hizo cracks ni za aina Gani , tayari tushaanza kupiga kelele
Kama Naibu waziri Mkuu kazinotice na kushauri jinsi ya kukabiliana nazo wewe ni nani ubishane naye?.
Au hujasikia maelekezo yake?.
 
Chato
 
kuna kipindi waziri kalemani alionekana kwenye tv akimlalamikia mkandarasi kwa kujenga chini ya Kiwango kwa kujenga nguzo chache kwenye ukuta wa bwawa tofauti na inavyotakiwa na kuweka wasimamizi wataalamu wachache .
Kwanini hakuchukua hatua kwenye hilo tatizo? Au ni hiyo hatua ya kulalamika kwenye TV?
 

Tuwekee video clips au link ya alipoyasema hayo.

Nje ya hapo itabaki kuwa porojo kama porojo zingine.
 
Toka lini viongozi wetu wakathamini maslahi ya taifa hili?
Wao wanathamini matumbo yao pekee hata hiyo kamati unayoisema haitafanya lolote zaidi ya kuendeleza kula hela tu
Kesi ya tumbili uipeleke kwa nyani yani hapo ni pipa na mfuniko
 
Toka lini viongozi wetu wakathamini maslahi ya taifa hili?
Wao wanathamini matumbo yao pekee hata hiyo kamati unayoisema haitafanya lolote zaidi ya kuendeleza kula hela tu
Kesi ya tumbili uipeleke kwa nyani yani hapo ni pipa na mfuniko
Hivi hili bandiko hapa lina ushahidi upi? Kuna video clip, audio clip? Au bila bila?
 
[emoji24] kipara yukowapi, huyu jamaa hajawahi kuwa mzalendo hata dakika moja
Hujui kitu!! Nyamaza na wanao kutag waache mara moja

Hii ndiyo Ile inaitwa Mchawi mpe mwanao akulelee

Mmezungushwa kwenye draft wajanja wamewaingiza kingi Sasa kingi yenu inaenda kuliwa mchezo unakwisha

Naibu Waziri Mkuu ndiyo hivyo Tena kwishnei anaenda kumuumbua Jiwe!!

Inasikitisha inachekesha

Raisi wa Mawe ni mjanja Sanaa

Huyoooooo kilaini 2025
 

Hii habari tunaishabikia lakini sijaona ushahidi wowote zaidi ya maneno ya mleta mada. Ajabu.
 
Akili una
 
Pamoja na angalizo hilo la UZALENDO ulilotoa hapa, hiyo "Tume Huru" toka Bungeni itaanza kuota yenyewe kama uyoga?

Hata kama ni kuwa na matumaini mkuu 'Rabbon', haya matumaini katika hali hii iliyopo sasa wewe unayatoa wapi?

Yaani kweli kwa moyo wako wa dhati katika hali tuliyomo sasa hivi kuwa na matumaini ya kuwapata watu ambao watafanya kazi kizalendo chini ya mfumo usioruhusu uzalendo?

Mimi sielewi matumaini haya unayatoa wapi hasa!

Haya, kwa namna ya muujiza, hiyo tume kweli iundwe, hayo yatakayoibuliwa na timu ya namna hiyo yatapelekwa wapi kufanyiwa utekelezaji wa mapendekezo ya tume?

Labda nikuulize, kwa miaka hii ya karibuni ni tume ngapi zimeundwa na kuwasilisha mapendekezo yao, ambayo yalitekelezwa kama yalivyotakiwa?
Kuna tume yoyote iliyoundwa ambayo hata matokeo ya tume uliyasikia?

Mimi nikupe tu pongezi ya kupenda taratibu zinazohitajika katika mambo kama haya zifanyike. Lakini kwa bahati mbaya sana kwetu sote, hakuna mazingira yanayoruhusu hayo unayoyapendekeza wewe.

Inaeleweka kwa nini watu bado wanashikilia na kuwa na kumbukumbu za kutenda mambo kwa taratibu zinazoeleweka, lakini ukweli ni kwamba nyakati hizi tulizomo ni tofauti kabisa.
Hatuna serikali inayoweza kufanya hayo unayoyapendekeza wewe kwa ufanisi unaotakiwa.

Ukitaka tume itaundwa, lakini hayo matokeo yake usiwe na matumaini nayo.
 
Team yenyewe ndo wamejazwa kina maarage, mafundi ving'amuz unategemea Nini[emoji848]
 
Watakaofanya uchunguzi ni sehemu ya watakaotoa maamuzi ya hatua za kuchukuliwa. Maamuzi yatafanyika kuendana na taswira ya chama kuelekea uchaguzi wa 2025. Hakuna maamuzi au hatua za maana zitachukuliwa nje ya utashi wa kisiasa.
Duh 🙄 !!!
 
Nawaza tu kama hayo manyufa yameanzia kwenye base? Mmmh!
Wale wakandarasi hiyo project sio ya kwanza kuijenga wanao ujuzi na hawawezi wakafanya vitu vya kijinga namna ile !!
Kama ni kweli !
Narudia kama ni kweli hiyo itakuwa ni hujuma !!
 
Mradi haujaisha, haujakabidhiwa. Kugundua dosari na kuanza kutoa maelekezo ni kutafuta sifa. Hata ukikabidhiwa na dosari zikajitokeza huwa kuna muda wa matazamio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…