Ushauri jamani, nimepewa taarifa binti yangu wa kazi ni mjamzito

Ushauri jamani, nimepewa taarifa binti yangu wa kazi ni mjamzito

Mf
Waungwana wa Jf,

Nimetoka mkoa ninaoishi nikasafiri mkoa mwingine kwa ajili ya mapumziko na kuweka akili sawa. Nyumbani nikimuacha binti wa kazi ambae nimekaa naye kwa muda wa mwaka mmoja sasa, ni binti mchapakazi, na asiye na kiburi na pia ni msafi sana, shida yake kubwa ilikuwa akiwa na mwanaume huyu akiachana nae ndani ya wiki anaye mwingine. Nilimuonya sana lakini ndo hivo, nikapiga simu kwa wazazi wake wakamuonya wala hakusikia.

Basi tukaamua tumuache kama alivyo ilmradi wajibu wake nyumbani anautimiza kwangu haikuwa shida, maisha yanaendelea.

Nikiwa huku ile wiki ya kwanza mwishoni napata simu kutoka kwa jirani 'Bushmamy kwema huko? Nikamjibu Nipo salama, akaendelea kusema kuwa binti yako ni mjamzito na inaonekana ana mimba ya miezi miwili maana alivyokuja hapa kwangu alisema ana kama miezi miwili hajaona siku zake, ndo nikamshauri akanunue kipimo kucheki ni Mimba tayari kinaonyesha"'akamaliza kuongea tukaagana.

Basi bwana mi nikaagiza Kilimanjaro ya baridi nikapiga pafu 4 ndo nikaanza kutafakari nafanyeje kwa sababu niliwaza yafuatayo:

Huyu binti nilimpenda tu vile hakuwa na kiburi.

Pili ni mchapakazi na msafi

Tatu kule kwao wanamtegemea kila mwezi atume hela ya kusaidia wazazi.

Nne ni mvumilivu katika hali zote za kiuchumi ninazopitia, na pia ni muaminifu sana hana tamaa na hela.

Pamoja na mambo mengine mengi tu maana nilipanga kuishi naye kabisa kama mdogo wangu ili baadaye nimpeleke ufundi cherehani au nimtafutie kazi lakini mambo ndo yameshakuwa hivyo maana hata hajui mimba ni ya nani.

Hadi sasa sijamwambia kama najua chochote kuhusu hali yake nasubiri nirudi.

Naombeni ushauri tafadhali maana binti ana miaka 20.
Mficha uchi hazai
 
Najua kuna watu wataandamana lakini usisahau option ya abortion endapo hali yake ya kiuchumi mbeleni haieleweki. Baada ya hapo vijiti vitamhusu ili asibebe mimba tena.
Kwani yeye hana haki ya kuzaa?
 
Kweli mkuuu utam hauna kikomo hakawii kuku ongezea mwingine tena
Kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe rekebisha matendo yako utakua na msingi imara

Japo ni hater una wivu na kila mtu humu JF nimeshangaa maisha halisi una huruma za hivyo.

Fukuza tu akalee kwao utamu hauna kikomo ,akijifungua ataendelea tena na tena.
 
Mkuu utapata tuu kwani huyo ulimptaje? Kwani mfano angehamua kuondoka ungemzuwia asiondoke?
Sawa nimekusoma mkuu ila nikimfukuza nawaza kama nitapata binti wap binti mwingine ambae hata kama sipo nnakuwa na uhakika wa usalama watoto
 
Back
Top Bottom