February Makamba
JF-Expert Member
- Jan 31, 2020
- 2,151
- 2,983
Wakuu kwema? Mimi kijana wenu mtiifu nimekuja kwenu nikiwa na majanga naomba mnisaidie.
Nilinunua simu mtandaoni kupitia kupatana.com, niliona bei ni nzuri nikamcheki jamaa nikachat nae kwenye hiyo website na akanipa namba.
Nikampigia kwa simu ya kawaida maana namba haikuwa WhatsApp, tukaongea akasema yupo mbezi nije tukutane niione.
Nikakutana nae pale mbezi stendi nikaicheki cheki nikaona ipo fresh niikampa hela nikaondoka na simu.
Baada ya kuitumia kama siku mbili nikagundua ina tatizo la charge ambalo sikuligundua muda ule. Nilipojaribu kumpigia nikashangaa namba zote nilizokuwa nawasiliana naye hazipatikani.
Niliumia lakini nikakubali tu kuishi nayo hivyo hivyo, nikakubali kupigwa. Sasa kimbembe kimekuja leo asubuhi wakati naitumia hii simu nikashangaa tu mara ghafla inawasha camera na kuanza kupiga 112, halafu inapiga milio kama ya ambulance, nikawahi nikaizima.
Nimekaa nimefikiria nimeshagundua itakuwa simu ilikuwa ya wizi na mwenye nayo anaitafuta, au huenda ilikuwa ni njama ya mapolisi kunifanyia hako kamchezo.
Sasa hapa nilichofanya nimeizima, ila bado nawaza nini nifanye sasa? Maana aliyeniuzia hapatikani na hata zile message za kupatana ameshazifuta hata mimi saivi sizioni.
Nilishaona watu wanakamatwa na polisi kwa hizi njama na kulipishwa pesa mingi au kubambikiziwa kesi.
Sasa nifanyeje wakuu?