Ukiwasiliana na mtu Kwa nini usirekodi?
Ukinunua vitu Mtandaoni Kwa nini usiwe una-screenshot? Na kuhifadhi kwenye kumbukumbu zako hata walau mwaka mzima?
Sio kosa kununua kitu used, lakini hapo ishu itaanzia kuthibitisha kwamba umenunua, hunarisiti, huna kumbukumbu yoyote kuonyesha ni kweli unaushahidi WA kununua hiyo simu.
Mimi nikinunua kitu used huwa nafanya hivi;
1. Narekodi Mawasiliano yangu na huyo muuzaji, tena Kwa kumuuliza maswali mfano,
Simu ni Aina gani, rangi gani, inatumia laini moja au mbili, n.k.
2. Screenshot TANGAZO la bidhaa uliyoiona Mtandaoni ukainunua.
3. Mkikutana mpige picha kisiri. Hii unaenda na mtu mwingine WA ziada ambaye atakuwa anarekodi matukio bila ya muuzaji kujua.
4. Ni vyema kujua majina yake,
Kwa dunia ya sasa huwezi kuepuka kununua vitu Used