Ushauri jamani, nimeshaharibu sinunui tena vitu used

Ushauri jamani, nimeshaharibu sinunui tena vitu used

Zama za kununua simu used zimeisha it's very risk. Pole kwa msala
 
Karipoti kupoteza line story iishie hapo japo wanauwezo wakutrack call history
 
Dah inanikumbusha kuna dogo aliuziwa simu hivi hivi online.Bei chee! Maeneo ya hapo mombasa dsm...
Alafu yeye anakaa kitunda kakaa kama wiki kuna namba ikawa imekosewa ya dada mmoja ivi sisi wanaume bana wepesi kuvutika.yule dada....

Akaanzisha tu mazoea kwenye simu hawajuani wala nini dem akaomba waonane dogo bila kujua aka kubali wakapanga wakutanie mombasa yule dada kumbe ni askari bana na dogo anategwa walipofika eneo la tukio kumbe askari washajiandaa kabisa..
Wamepaki tu gari Lao pembeni na wanapingu kabisa.
Katika maongezi wakaja jamaa wawili wanamuuliza wee ni fulani fulani ndio tunakushikilia kwanzia sasa.

Kwa kutumia Mali ya wizi ambayo ni hiyo simu unayotumia kilichomuokoa yule dogo ni kujulikana yule maeneo walio mkamatia ndugu zake walikuja kumuachia kwa dhamana ya 600k kwa simu ya 150k

Usiamini watu wanao uza hizi simu used wanaweza kukuzunguka wao wenyewe otherwise umenunua refurbished ambazo ni used from dubai,UK,USA,China na kwenye duka kabisa.
 
Wakuu kwema? Mimi kijana wenu mtiifu nimekuja kwenu nikiwa na majanga naomba mnisaidie.

Nilinunua simu mtandaoni kupitia kupatana.com, niliona bei ni nzuri nikamcheki jamaa nikachat nae kwenye hiyo website na akanipa namba.

Nikampigia kwa simu ya kawaida maana namba haikuwa WhatsApp, tukaongea akasema yupo mbezi nije tukutane niione.

Nikakutana nae pale mbezi stendi nikaicheki cheki nikaona ipo fresh niikampa hela nikaondoka na simu.

Baada ya kuitumia kama siku mbili nikagundua ina tatizo la charge ambalo sikuligundua muda ule. Nilipojaribu kumpigia nikashangaa namba zote nilizokuwa nawasiliana naye hazipatikani.

Niliumia lakini nikakubali tu kuishi nayo hivyo hivyo, nikakubali kupigwa. Sasa kimbembe kimekuja leo asubuhi wakati naitumia hii simu nikashangaa tu mara ghafla inawasha camera na kuanza kupiga 112, halafu inapiga milio kama ya ambulance, nikawahi nikaizima.

Nimekaa nimefikiria nimeshagundua itakuwa simu ilikuwa ya wizi na mwenye nayo anaitafuta, au huenda ilikuwa ni njama ya mapolisi kunifanyia hako kamchezo.

Sasa hapa nilichofanya nimeizima, ila bado nawaza nini nifanye sasa? Maana aliyeniuzia hapatikani na hata zile message za kupatana ameshazifuta hata mimi saivi sizioni.

Nilishaona watu wanakamatwa na polisi kwa hizi njama na kulipishwa pesa mingi au kubambikiziwa kesi.

Sasa nifanyeje wakuu?
Simu ya aina gani?
 
Story Yako insschekesha na kufundisha.
Kwanini hukupokea hiyo simu iliyoita Kwa 112?
 
Hata asipoweka laini.
Ikiwa tu hewani kaisha.
labda aizime
wakiingiza IMEI number ya Simu inasoma mahali ulipo hata Kama uvunguni.
Watakuja mpaka hapo.
Yaani kule wanaona kabisa mizunguko yako.
Wasikutishe mkuu
Izo simu zinazoibiwa zinatumika sana na akuna kinachotokea sema haziwekwi line
 
Kuna boya kama wewe kauziwa Samsung s9 plus tume mdaka katulipa laki 2 ya gharama na usumbufu alio tupa..ni simu gani kwanza yaweza kua ni tecno iyo waki kudaka uta toa Ten tu ya mafuta
 
Halafu sasa hivi kuna maduka mengi tu k,koo yanauza simu used kali tu kutoka nje zinauzwa kuanzia 200k na kuendelea mfano samsung s6,7,8 na9 iphone 6,8,9 sony xz1, 2, 3 unapewa risiti na guarantee. Unachofanya unawatafuta online kupitia kupatana zoom au jiji buy online ukiwasiliana nao unaenda dukani mwenyewe usisubiri wakuletee ukiridhika na bidhaa unalipia unasepa, lakini sio kununua kitu kwa mtu mkononi ni risk sana.
 
Kuna vishkwambi hapa vinauzwa bei ya kutupa, havijatumika hata wiki

images - 2022-08-02T212621.281.jpeg
 
Tupa simu na line ukiyoweka kwenye iyo simu
 
Hivi unaanzaje kununua kitu kama simu mkononi kwa mtu wakati maduka yamejaa Kariakoo mpaka vichochoroni?

Assume hiyo simu mtu alidungwa kisu akaporwa,au alibakwa akaporwa kisha simu ukamatwe nayo wewe!!!

Yaani mpaka Mahakama ije ikuone hauna Hatia ya Kuua au Kubaka utakuwa umeshakaa Segerea umejaa ukurutu mpaka makalioni!!acha kabisa kununua vitu vya electronics mkononi,utakuja kubeba msalaba usio wako!!!
Kutafuta kitonga au ganda la ndizi ndiyo tatizo mkuu..
 
Ni kweli vitu used vina changamoto zake lakini kama pesa huna utafanyaje?

Kumbuka wengi tunaishi maisha Used used!

Magari karibu yote unayoyaona hapa nchini ni Used, unafikiri watu hawapendi Mapya? umasikini ni moja ya sababu ya watu kununua vitu Used.
Nunua kitochi cha elfu 25 kipyaaa wakati unajuchanga kuvuta Tecno ya laki moja na nusu... Nani kasema lazima umiliki Samsung??
 
Back
Top Bottom