Ushauri jamani, nimeshaharibu sinunui tena vitu used

Ukiwasiliana na mtu Kwa nini usirekodi?
Ukinunua vitu Mtandaoni Kwa nini usiwe una-screenshot? Na kuhifadhi kwenye kumbukumbu zako hata walau mwaka mzima?

Sio kosa kununua kitu used, lakini hapo ishu itaanzia kuthibitisha kwamba umenunua, hunarisiti, huna kumbukumbu yoyote kuonyesha ni kweli unaushahidi WA kununua hiyo simu.

Mimi nikinunua kitu used huwa nafanya hivi;

1. Narekodi Mawasiliano yangu na huyo muuzaji, tena Kwa kumuuliza maswali mfano,
Simu ni Aina gani, rangi gani, inatumia laini moja au mbili, n.k.

2. Screenshot TANGAZO la bidhaa uliyoiona Mtandaoni ukainunua.

3. Mkikutana mpige picha kisiri. Hii unaenda na mtu mwingine WA ziada ambaye atakuwa anarekodi matukio bila ya muuzaji kujua.

4. Ni vyema kujua majina yake,

Kwa dunia ya sasa huwezi kuepuka kununua vitu Used
Kwa nini usiepuke kununua used ? Hakuna ulazima wowote wa kununua vitu used , vitu used vina madhara mengi , bora uende dukani tu kuepuka matatizo .
 
Mengineyo
4. Andikishaneni, iwe polisi au kwa mwenyekiti wa mtaa hata bolazi

5. Muulize muuzaji kama ana kitambulisho cha kupiga kura, NIDA etc akipige kopi kisha akuachie nakala
 
Wakuu kwema? Mimi kijana wenu mtiifu nimekuja kwenu nikiwa na majanga naomba mnisaidie.

Nilinunua simu mtandaoni kupitia kupatana.com
Niliona bei ni nzuri nikamcheki jamaa nikachat nae kwenye hiyo website na akanipa namba.

Nikampigia kwa simu ya kawaida maana namba haikuwa WhatsApp, tukaongea akasema yupo mbezi nije tukutane niione.

Nikakutana nae pale mbezi stendi nikaicheki cheki nikaona ipo fresh niikampa hela nikaondoka na simu.
Baada ya kuitumia kama siku mbili nikagundua ina tatizo la charge ambalo sikuligundua muda ule, Nilipojariby kumpigia nikashangaa namba zote nilizokuwa nawasiliana naye hazipatikani.

Niliumia lakini nikakubali tu kuishi nayo hivo hivo, nikakubali kupigwa,,,,, Sasa kimbembe kimekuja leo asubuhi wakati naitumia hii simu nikashangaa tu mara ghafla inawasha camera na kuanza kupiga 112..Halafu inapiga milio kama ya ambulance....Nikawahi nikaizima.

Nimekaa nimefikiria nmeshagundua itakuwa simu ilikuwa ya wizi na mwenye nayo anaitafuta, au huenda ilikuwa ni njama ya mapolisi kunifanyia hako kamchezo.

Sasa hapa nilichofanya nimeizima, ila bado nawaza nini nifanye sasa? Maana aliyeniuzia hapatikani na hata zile message za kupatana ameshazifuta hata mimi saivi sizioni.

nilishaona watu wanakamatwa na polisi kwa hizi njama na kulipishwa pesa mingi au kubambikiziwa kesi.
Sasa nifanyeje wakuu?
Usalama wako kaitupe chooni au anza kutafuta wakili msomi
 
WAHUNI WA CCM WAMESHA KUINGIZA CHAKA [emoji1787][emoji1787]
 
Kwa nini usiepuke kununua used ? Hakuna ulazima wowote wa kununua vitu used , vitu used vina madhara mengi , bora uende dukani tu kuepuka matatizo .

Ni kweli vitu used vina changamoto zake lakini kama pesa huna utafanyaje?

Kumbuka wengi tunaishi maisha Used used!

Magari karibu yote unayoyaona hapa nchini ni Used, unafikiri watu hawapendi Mapya? umasikini ni moja ya sababu ya watu kununua vitu Used.
 
Kama utaenda polisi tafadhali tadhali usiende peke yako,tena kama inawezekana chukua vijisenti kidogo mpatie jamaa mmoja mwenye kitambi na kijigari muombe adai ni kaka/dada yako.na huyohuyo ndo akutolee maelezo maana wewe uijieleza lazima utakuwa na panik flani.au basi nenda na wakili kabisa maana hata kwa 50,000/- anaweza kukusindikiza!
 
Ukishatia line kwenye simi tayari tcra wanaijua namba inayotumia simu, Polisi wakienda tcra wanapewa namba inayotumia simu.

Kiufupi washakujua iwapo simu iliibiwa na alieibiwa alienda kuifatilia polisi. hata ukiitupa simu chooni haisaidii, tena itunze simu vizuri lasivyo utadaiwa na pesa ya simu hiyo mpya.

Mpe mtu unaemwamini kama laki 1 hivi, awe mtu mzima kidogo mwenye maneno ya busara akiri kwamba ulinunua simu mtaani bila kujua ni ya wizi na akuombwe msamaha kwa hio laki 1, lasivyo unaenda jela kiutani utani.

Kuwa makini sana unaponunua vitu kama modem na simu ambazo huwa zina imei inayorahisisha kazi kujua namba inayotumia kifaa.
 
Back
Top Bottom