Ushauri jamani, nimeshaharibu sinunui tena vitu used

Ushauri jamani, nimeshaharibu sinunui tena vitu used

Nunua kitochi cha elfu 25 kipyaaa wakati unajuchanga kuvuta Tecno ya laki moja na nusu... Nani kasema lazima umiliki Samsung??

Kila mtu analazima yake.

Kumbuka wengine kazi na biashara zipo kwenye simu, sasa unanunua kitochi utapataje pesa za kununua Smartphone ilhali Mishe zako ni mtandaoni?

Elewa kuwa Dunia ya sasa kuna maelfu ya Vijana wanafanya kazi wakiwa wamelala NYUMBANI NA wanapata pesa za kutosha kupitia Smartphone.

Imetokea Smartphone imeibiwa, au kuharibika na Hana pesa ya nyingi ya haraka ya kununua simu mpya ndio hapo ananunua Used Kwa muda ili aendeleze biashara zake.

Nokia Tochi ni Kwa mawasiliano, Smartphone ni zaidi ya mawasiliano.
 
Hili ni tatizo, laweza kumpata mtu yeyote na kusababishia usumbufu mkubwa kwake na hata kwa familia yake na kupelekea shida na mateso kwao.
Cha msingi, utengenezwe mfumo wa kununua vifaa used vya aina hii, kwamba mnunuzi na muuzaji wanafika mamlakani kukikagua ubora na historia yake ili mnunuzi anunue akawe na aman nacho.
Hii itapunguza kabs utapeli wa namna hii na usumbufu unaosababishwa nao.
 
Wakuu kwema? Mimi kijana wenu mtiifu nimekuja kwenu nikiwa na majanga naomba mnisaidie.

Nilinunua simu mtandaoni kupitia kupatana.com, niliona bei ni nzuri nikamcheki jamaa nikachat nae kwenye hiyo website na akanipa namba.

Nikampigia kwa simu ya kawaida maana namba haikuwa WhatsApp, tukaongea akasema yupo mbezi nije tukutane niione.

Nikakutana nae pale mbezi stendi nikaicheki cheki nikaona ipo fresh niikampa hela nikaondoka na simu.

Baada ya kuitumia kama siku mbili nikagundua ina tatizo la charge ambalo sikuligundua muda ule. Nilipojaribu kumpigia nikashangaa namba zote nilizokuwa nawasiliana naye hazipatikani.

Niliumia lakini nikakubali tu kuishi nayo hivyo hivyo, nikakubali kupigwa. Sasa kimbembe kimekuja leo asubuhi wakati naitumia hii simu nikashangaa tu mara ghafla inawasha camera na kuanza kupiga 112, halafu inapiga milio kama ya ambulance, nikawahi nikaizima.

Nimekaa nimefikiria nimeshagundua itakuwa simu ilikuwa ya wizi na mwenye nayo anaitafuta, au huenda ilikuwa ni njama ya mapolisi kunifanyia hako kamchezo.

Sasa hapa nilichofanya nimeizima, ila bado nawaza nini nifanye sasa? Maana aliyeniuzia hapatikani na hata zile message za kupatana ameshazifuta hata mimi saivi sizioni.

Nilishaona watu wanakamatwa na polisi kwa hizi njama na kulipishwa pesa mingi au kubambikiziwa kesi.

Sasa nifanyeje wakuu?
Pole sana mkuu.
 
Option mbili.
1. Isalimishe polisi
2. Itelekeze na uanze upya

Na suggest option two. Ila unaweza kuitunza tu home ili siku za mbeleni ukikamatwa ujitetee
Alishaitumia,hapo watatrack simu alizopiga kwa watu then hao watu ndio watakaosema yeye ni nani,hapo ajiandae na wazee wa staki shari,obey au msimbazi ndio wenye michezo hiyo 😀
 
Mengineyo
4. Andikishaneni, iwe polisi au kwa mwenyekiti wa mtaa hata bolazi

5. Muulize muuzaji kama ana kitambulisho cha kupiga kura, NIDA etc akipige kopi kisha akuachie nakala
Binafsi kitu used kabla sijakupa pesa lazima uconfess kwenye video ya wewe flan bin flan unaniuzia kitu flan ambacho ni mali yako halali,risiti ya uliyonunulia iko kitu na mashahidi juu,unaweza kuchukulia simple then ukaja kuingia kwenye ttz bila kutegemea
 
Pole sana, waTanzania wengi kwenye biashara za mitandaoni siyo waaminifu...
 
Nenda ukariport police ,usiogope pengine itakusahidia uko mbele,
Ikiwezekana tafuta police ongeanae kwa siri mpange ,ili kikinuka aje akusahidie
Subiri uje ukamatwe ndio ukione cha moto,
 
Wakuu kwema? Mimi kijana wenu mtiifu nimekuja kwenu nikiwa na majanga naomba mnisaidie.

Nilinunua simu mtandaoni kupitia kupatana.com, niliona bei ni nzuri nikamcheki jamaa nikachat nae kwenye hiyo website na akanipa namba.

Nikampigia kwa simu ya kawaida maana namba haikuwa WhatsApp, tukaongea akasema yupo mbezi nije tukutane niione.

Nikakutana nae pale mbezi stendi nikaicheki cheki nikaona ipo fresh niikampa hela nikaondoka na simu.

Baada ya kuitumia kama siku mbili nikagundua ina tatizo la charge ambalo sikuligundua muda ule. Nilipojaribu kumpigia nikashangaa namba zote nilizokuwa nawasiliana naye hazipatikani.

Niliumia lakini nikakubali tu kuishi nayo hivyo hivyo, nikakubali kupigwa. Sasa kimbembe kimekuja leo asubuhi wakati naitumia hii simu nikashangaa tu mara ghafla inawasha camera na kuanza kupiga 112, halafu inapiga milio kama ya ambulance, nikawahi nikaizima.

Nimekaa nimefikiria nimeshagundua itakuwa simu ilikuwa ya wizi na mwenye nayo anaitafuta, au huenda ilikuwa ni njama ya mapolisi kunifanyia hako kamchezo.

Sasa hapa nilichofanya nimeizima, ila bado nawaza nini nifanye sasa? Maana aliyeniuzia hapatikani na hata zile message za kupatana ameshazifuta hata mimi saivi sizioni.

Nilishaona watu wanakamatwa na polisi kwa hizi njama na kulipishwa pesa mingi au kubambikiziwa kesi.

Sasa nifanyeje wakuu?
Wachana na electronics zilizotumika. Nunua mpya mahala panapoeleweka.
 
Dunia ya sasa bila vielelezo lolote laweza kukupata.

Trust no one.
Kuna watu wanaoña wajinga Walioweka Rekodi kwenye simu.

Au unapoongea na Huduma Kwa Wateja wanapokuambia mazungumzo yatarekodiwaa wanafikiri wanaofanya hivyo ni wajinga.

Hata ukipewa Risiti bado kuna risiti Fake, lakini kurekodi ni muhimu sana

Hakika
 
Back
Top Bottom