Ushauri: Je, ajenge nyumba au aweke pesa fixed deposit CRDB kwa riba ya 7%?

Ushauri: Je, ajenge nyumba au aweke pesa fixed deposit CRDB kwa riba ya 7%?

Ukijenga nyumba kila baada ya miaka 5 lazima utumie 20% uliyotumia kuikarabati. Kujenga nyumba ya kupanga ni kujiletea sonona. Ni hayo
Itategemea ulijengaje na hao wapangaji wako ni watu wa namna gani
 
Ajenge nyumba ya kawaida,apangishe,au flem za biashara,chonde chonde,asiingie kwenye biashara ya magsri,mafuso,au bodaboda,mtamzika mapema,
Bi mkubwa wangu,alipata kama ,120M,akanunua fuso,akamuweka kaka yake(anko)asimamie,anko mwenyewe choka mbaya,faida hakuna,kila siku gari bovu,lakini anko halileti nyumbani,mwishowe likauzwa kwa hasara!!
Sasa hv wote ni hoehae,watoto ndio tunabeba mzigo,
 
Mama yangu kastaafu utumishi.kapewa.mafao milioni 100.anataka ushauri ajenge.nyumba yakupangisha au aweke fixed deposit bank ambayo kwa urahisi itampa kama laki saba kila mwezi.

Ushauri please
Kwamba yeye hajakutwa na kikokotoo kipya? Maana kapata mafao manono kiasi
 
UTT vipande ni 12% na kila mwezi anapata cash 1M yake wakati hiyo million 100 ipo intact. Kujenga nyumba ni Upuuzi maana hata siku moja hiyo hela hai rudi. Ukijenga nyumba kila baada ya miaka 5 lazima utumie 20% uliyotumia kuikarabati. Kujenga nyumba ya kupanga ni kujiletea sonona. Ni hayo
nyumba ina faida nyingi kwa sababu thamani yake inaongezeka vizuri.

Nyumba ni safe assets

Kwanza sijawahi waza kulipa kodi au kusumbuana na mwenye nyumba. Na isitoshe nina familia kubwa sana, watoto wa kike na kiume.

kwa sisi wafanyabiashara huwa tunakopa sana kwa kutumia hati za nyumba zetu

akijenga nyumba maeneo mazuri anaweza kula kodi nzuri sana. Ukijenga chanika usitegemee utapata hela sawa na aliyejenga mbezi kwa Kodi

Binafsi nimeona faida kubwa ya kujenga natafuta hela nijenge hata kumi. Mzee kajenga guest mpaka naona wivu kila siku vyumba vinajaa wakati mwanzo nilikuwa namshauri kuwa guest ziko nyingi hazitolipa

strategic thinking itakusaidia sana huko mbeleni. .
 
Ajenge nyumba ya kawaida,apangishe,au flem za biashara,chonde chonde,asiingie kwenye biashara ya magsri,mafuso,au bodaboda,mtamzika mapema,
Bi mkubwa wangu,alipata kama ,120M,akanunua fuso,akamuweka kaka yake(anko)asimamie,anko mwenyewe choka mbaya,faida hakuna,kila siku gari bovu,lakini anko halileti nyumbani,mwishowe likauzwa kwa hasara!!
Sasa hv wote ni hoehae,watoto ndio tunabeba mzigo,
Umenikumbusha jamaa mmoja mjeda alistaafu bado ana nguvu watoto ndio wanaanza sekondari si akanunua fuso mbili. Napoongea hapa hata nyumba ya kuishi kashindwa kumaliza madirisha kaweka maboksi madirishani. Fuso zote aliuza kwa hasara

Sasa hivi watoto wanasoma kwa shida sana na mmoja alimaliza anaendesha bodaboda
 
Ana uzoefu na ujenzi.. ana viwanja kadhaa, ajenge apartments.. piga chumba, sebune, choo jiko.. chumba, choo, n.k.. anakula fedha yake tu.. inawezekana hiyo 100 isiishe na ikabaki chenji ya kufanya mengine..

Tena kama viwanja vipo tayari huenda akatoa, nyumba mbili..
Kama sehemu mnayoishi frem zina thamani nzuri.. ajenge na fremu hapo kwake.

Hana kiwanja, apoint eneo ambalo aparments zina soko.. apate eneo pia frem zinamahitaji.. ashushe mjengo na frem zake kadhaa..

Hapo atakuwa anakula passion ndani ya pension.
 
Mama yangu kastaafu utumishi.kapewa.mafao milioni 100.anataka ushauri ajenge.nyumba yakupangisha au aweke fixed deposit bank ambayo kwa urahisi itampa kama laki saba kila mwezi.

Ushauri please
Ushauri ajenge apangishe.Akifanya tofauti itakuwa shida.Baada ya miaks 5+ atakuwa kafulia hadi shida.Pressure itakuwa mali yake.

Pesa akiwa nayo imejaa kila mmoja miongoni mwa watoto kukopa bila kurudisha mwisho anafulia na kufa maskini.

Narudia kama yupo mkoa anatoa nyumba 4 kiasi kingine kilichobaki ndo afungue biashara na kula.Kumbuka biashara ikifa uhakika wa 1 kwa mwezi nyumba inampa mshahara.Chonde nyie watoto msimkope mama yenu ndio mwanzo wa kushindwa mama kufanya jambo la maana.Ni uzoefu wangu kwa wastafu zaidi ya watatu
 
amunue Govt Bonds BoT, UTT au Share ktk Makampuni....

Km aliwahi kuwa na Biashara tangu yupo Ofisini, anaweza kuipa pesa kuiboresha... asijaribu kuanzisha biashara mpya...

Asijenge Nyumba... wkt wa ujenzi kuna pesa itatumika: kusimamia ujenzi, kuHandle matatizo ya Kijamii, gharama kuongezeka ingali ujenzi unanedelea (bei za building materials, makosa ya mafundi sites nk)
km ni nyumba nashauri iwe ya kununua ...
 
Maisha ya ajira kwel ni utumwa na unyonyaji unafanyaa kazi miaka 40 ufike miaka 60 ndipo upate milion 100.
Wakati watoto wa Kikinga anamiaka 20 anapita airport ana cash milioni 300 anaenda jumua t shirt na jeans China akauze njombe
sio watu wote waloingia ktk Biashara walitoboa... labda hujakutana na waliobuma...
 
Ukisha staafu hata ujitunze viipi mwusho wa siku mali ni kwa ajili ya utakao waacha duniani. Hao wanaomwambia atunze hela ale kidogo kidogo wanamdanganya. Hela haitunziki ili iliwe kidogokidogo. Baada ya miezi 6 tu tutarudi hapa kwenye account zikiwa zimebaki chavhe sana.

Ndugu, wanao, marafiki na matatizo wakijua umetunza hela kila siku wanagonga hodi mlangoni kwako kukushawishi hili na lile na ni ngumu kuwakatalia wote. Unaweza kuwakatalia ndugu ukaangukia kwa wanao. Unawakatalia wanao unaangukia kwenye matatizo

Wote walio jaribu kuweka nenda kavute statement yao uone kama walikaa na hizo hela kwa miaka 2 na zaidi.

Niko hapa
Ndo maana wanamshaufi aweke fixed ili ale taratibu faida huku mpunga ukiwa intact. Akifa vijana wanarithi fwedha.
 
Back
Top Bottom