Ushauri: Je, nilivyojenga juu ya shimo la choo ni sahihi?

Ushauri: Je, nilivyojenga juu ya shimo la choo ni sahihi?

Unauliza baada ya kujenga? Kama nimelewa vizuri ujenzi wako, shimo la choo linahitaji sehemu ya ''kupumua'' kwani kunakuwa na production ya gas ndani. Uliweka chimney ya kutolea gas?
Ndy mkuu nmeweka na chemba yahivi likijaa tunaweza kufyonza lkn uwezekano wa kujaa ni mdogo kwakuwa chini hatujasakafia
 
Uimara unategemea kuta za hilo shimo la choo na slab umetumia material gani.

Shule za umma miaka ya nyuma vyoo vilikuwa vinakuwa juu ya karo lenyewe hata matundu sita na hakuna shida pamoja na idadi kubwa ya wanafunzi.
Namimi nilifanya kwa mawazo haya nikaona inawezekana
 
Huu uzi ulitakiwa uulete kabla ya kujenga ili upewe ushauri, hicho ulichofanya ni hatari kubwa ni suala la muda tu, je utabomoa? jibu unalo wewe.
 
Ndy mkuu nmeweka na chemba yahivi likijaa tunaweza kufyonza lkn uwezekano wa kujaa ni mdogo kwakuwa chini hatujasakafia
Kama uliweka ndefu na hewa inatoka kwenda juu bila kuathiri ndani ya nyumba sioni tatizo. Cha kuzingatia ni kuwa ujenzi uwe imara ili kusiwepo na weakness zozote. Mafundi wetu nawajua hivyo kama uliwasimamia vizuri it should work. pia uwe unafanya assessment za mara kwa mara
 
Kama heading inavyojieleza, nilinunua kiplot kidogo ivi nikajenga kajumba ka vyumba vitatu mbele kuna kanafasi ka parking ya gari ndogo na nyuma kukabaki nafasi ndogo ambayo nikatumia kuchimba shimo la choo.

Nilivyopata vihela kidogo nikashawishika kuzunguusha fence, sasa baada ya kumaliza fence nikaona ile nafasi ya nyuma ya nyumba ni kubwa kiasi na nnaweza kujenga store na vyoo viwili na jiko la nje la kishkaji nikafanya ivo.

Tukashauriana na fundi kuwa tutumie ukuta wa fensi kuamsha vile vyumba na tufunike shimo la choo kwa zege ili ile sehem ndo tuitumie kujenga vyoo na upande mwingine uwe kwa ajili ya jiko na store na tukafanya ivo.

Sasa hofu yangu ni kuwa lile shimo haliwezi kuleta shida baadae likaporomoka au msuguano wa joto likaripuka na kuleta madhara, je njia sahihi ni ipi au nisiwe na wasiwasi halitaleta shida ushauri wenu wanajenzi.
Zaidi ya 60% humu tumekulia kwenye vyoo vya namna iyo...hakikisha tu ilo zege ni imara na angalia pia nature ya eneo isije kuwa mfinyazi pakatitia
 
Pole sana. Ujenzi unaumiza sana kichwa haswa kama huna plan.

Swali lako linaonyesha kwamba hukujipanga kabla ya kujenga.

Sioni sababu ya kujenga karo wakati kuna mashimo ya kisasa yenye kutumia eneo dogo na hayajai.
 
Hela za kuunga unga mkuu
 
Zaidi ya 60% humu tumekulia kwenye vyoo vya namna iyo...hakikisha tu ilo zege ni imara na angalia pia nature ya eneo isije kuwa mfinyazi pakatitia
Eneo ni sehemu ya kichuguu ardhi yake ngumu sana hata kuchimba tulipata tabu sana
 
Sio mabanzi haya mabaki ya nje ya mbao, ni miti fulani migumu inaitwa mikambaa hiyo ni migumu inadumu hata miaka 100
Upo sahihi mkuu kuna na watu walinieleza ivo tuweke mabanzi kwani yanadumu sana kuliko nondo ndo nikakata shauri niweke lkn pia gharama zilikuwa afadhari kuliko ningetumia nondo zile pana
 
CHANGAMOTO YA MBONGO.
  • boss yeye.
  • designer yeye
  • Qs
  • Vendor yeye
  • Qualitu assuarance yeye
  • injinia yeye
  • badala ya fundi kumshauri, yeye ndio anamshaur fundi

AKIMALIZA ANAKUJA KUOMBA USHAURI.
Hapana mkuu, karibia mawazo yote katoa fundi mm nimepitisha tu hadi nakuja huku naona kama kutakuwa na shida japo fundi(maiko) ananihakikishia hakutakuwa na shida
 
Sawa ila unatakiwa uwe mwangalifu kwa sababu nyumba ukiijenga ndivyo isivyo ni kama kilema kila ukiingalia unakasirika.

Nenda polepole.
Ahsante mkuu nimekuelewa
 
Hapana mkuu, karibia mawazo yote katoa fundi mm nimepitisha tu hadi nakuja huku naona kama kutakuwa na shida japo fundi(maiko) ananihakikishia hakutakuwa na shida
Fundi maiko huyo ni taka taka..sasa kwenye ukajenge juu ya shimo la choo...ule mvule umeweka bomba kwa namna gan.

Unge share picha ingekua rahis zaid
 
Back
Top Bottom