Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tumia moyo wako mkuu, maana ndio utaathirika. Achana na moyo wa kupewa. Hizo tofari za matobo na hicho unataka kufanya HAPANA. Bora ingekuwa suala la mirunda tungepeana au kuazimana moyo. Siwezi kukupa au kukuazima moyo wangu halafu udumbukie kwenye choo.Ahsante mkuu kwa kunipa moyo
Acha na sitisha huo mpangoFundi alisema zile ndo nzuri ili maji yapenye yanyonywe na ardhi
Sasa kwa usalama zaidi ili kupunguza athari nifanyeje mkuu
Naufuatilia huu uzi maana ndo nilichofanyaKama heading inavyojieleza, nilinunua kiplot kidogo ivi nikajenga kajumba ka vyumba vitatu mbele kuna kanafasi ka parking ya gari ndogo na nyuma kukabaki nafasi ndogo ambayo nikatumia kuchimba shimo la choo.
Nilivyopata vihela kidogo nikashawishika kuzunguusha fence, sasa baada ya kumaliza fence nikaona ile nafasi ya nyuma ya nyumba ni kubwa kiasi na nnaweza kujenga store na vyoo viwili na jiko la nje la kishkaji nikafanya ivo.
Tukashauriana na fundi kuwa tutumie ukuta wa fensi kuamsha vile vyumba na tufunike shimo la choo kwa zege ili ile sehem ndo tuitumie kujenga vyoo na upande mwingine uwe kwa ajili ya jiko na store na tukafanya ivo.
Sasa hofu yangu ni kuwa lile shimo haliwezi kuleta shida baadae likaporomoka au msuguano wa joto likaripuka na kuleta madhara, je njia sahihi ni ipi au nisiwe na wasiwasi halitaleta shida ushauri wenu wanajenzi.
Umeuliza vizuri sana mkuu mikambaa siijui ila nimetumia mabanzi ya uku kwetu tunayaita mkarambati ni magumu na hayaliwi na waduduPitia vipengele vifuatavyo,viangaliwe.
Hatari zilizopo
1.Kutitia Kwa Ardhi
-maji ya kutoka kwenye matundu ya choo,hufanya ardhi upande mmoja utitie.
-Hii ujitokeza sana kwenye kichanga.
2.Matilio
NONDO
-Kama kwenye zege kuna nondo
-shimo lina maji ya Kinyesi,na mvuke.
-Zege Siku zote hunyonya maji, so maji yatafikia nondo.
-Maji hayo yenye chumvi,yaya sababisha kutu kwa mwendokasi.
MIKAMBAA
-Kama umeweka mikambaa
-Haiathiriwi na maji
-Lakini haina nguvu kuliko nondo.
3.PRESSURE
-Haujaweka bomba la kutolea joto.
-Joto huongeza pressure
-Pessure isipo ruhusiwa, itatafuta sehemu nyepesi kuharibu taratibu.
-pressure litavimbisha kuta na kuweka nyufa.
4.UZITO
-umepiga mahesabu juu ya samani zitakazowekwa ndani ya hivyo vyomba.
-Je,huo mkambaa una uwezo wa kuhimili uzito wa kilo 300 au 600
5.MSINGI
-Msingi umeujengaje,
-Kuna zege lenye nondo, la kuzidisha uimara
TAHADHARI
Watu wasiige huu mfumo, una hatari sana.
Hata nondo pia haziliwi na wadudu...Umeuliza vizuri sana mkuu mikambaa siijui ila nimetumia mabanzi ya uku kwetu tunayaita mkarambati ni magumu na hayaliwi na wadudu
Na kuhusu zege la msingi ni kweli nimeweka kama inch 4 upana na cement iliyokolea
Na kuhusu uzito, sehem ya shimo nimejenga vyoo viwili tu kwingine ndio nimeongezea kujenga jiko na store
Fundi kanishauri niweke chemba za kupumulia na tumefanya ivoHata nondo pia haziliwi na wadudu...
Simenti kukolea siyo factor hapo,
Hayo mazingira ni yanazalisha joto na unyevu wenye chumvi.
-Je,umetumia simenti yenye kuendana na hivyo vitu....?
-Je,kuna additives zozote ulizoweka kwenye simenti kukabiliana na hivyo vitu...?
Mbao/miti na Zege zina viwango tofauti vya kusinyaa na kutanuka, vimetofautiana sana...
-Je,ulishapiga hesabu juu ya hili...?
Hebu muulize fundi kama ana uelewa wa hivyo vitu nilivyo kuuliza.Fundi kanishauri niweke chemba za kupumulia na tumefanya ivo