Ushauri: Je, nilivyojenga juu ya shimo la choo ni sahihi?

Mzee umefanya hatari sana, ulitakiwa uulize kabla ya kujenga. Huu uzi hauna faida tena kwako.
 
Mzee umefanya hatari sana, ulitakiwa uulize kabla ya kujenga. Huu uzi hauna faida tena kwako.
Nipe athari niweze kujipanga hiyo ndo itakuwa faida kwangu

Au nipe uzoefu kama hamna shida niwe na amani pia ni faida
 
Ahsante mkuu kwa kunipa moyo
Tumia moyo wako mkuu, maana ndio utaathirika. Achana na moyo wa kupewa. Hizo tofari za matobo na hicho unataka kufanya HAPANA. Bora ingekuwa suala la mirunda tungepeana au kuazimana moyo. Siwezi kukupa au kukuazima moyo wangu halafu udumbukie kwenye choo.
 
Fundi alisema zile ndo nzuri ili maji yapenye yanyonywe na ardhi

Sasa kwa usalama zaidi ili kupunguza athari nifanyeje mkuu
Acha na sitisha huo mpango
 
Naufuatilia huu uzi maana ndo nilichofanya
 
Pitia vipengele vifuatavyo,viangaliwe.
Hatari zilizopo
1.Kutitia Kwa Ardhi
-maji ya kutoka kwenye matundu ya choo,hufanya ardhi upande mmoja utitie.
-Hii ujitokeza sana kwenye kichanga.

2.Matilio
NONDO
-Kama kwenye zege kuna nondo
-shimo lina maji ya Kinyesi,na mvuke.
-Zege Siku zote hunyonya maji, so maji yatafikia nondo.
-Maji hayo yenye chumvi,yaya sababisha kutu kwa mwendokasi.

MIKAMBAA
-Kama umeweka mikambaa
-Haiathiriwi na maji
-Lakini haina nguvu kuliko nondo.

3.PRESSURE
-Haujaweka bomba la kutolea joto.
-Joto huongeza pressure
-Pessure isipo ruhusiwa, itatafuta sehemu nyepesi kuharibu taratibu.
-pressure litavimbisha kuta na kuweka nyufa.

4.UZITO
-umepiga mahesabu juu ya samani zitakazowekwa ndani ya hivyo vyomba.
-Je,huo mkambaa una uwezo wa kuhimili uzito wa kilo 300 au 600

5.MSINGI
-Msingi umeujengaje,
-Kuna zege lenye nondo, la kuzidisha uimara

TAHADHARI
Watu wasiige huu mfumo, una hatari sana.
 
Umeuliza vizuri sana mkuu mikambaa siijui ila nimetumia mabanzi ya uku kwetu tunayaita mkarambati ni magumu na hayaliwi na wadudu

Na kuhusu zege la msingi ni kweli nimeweka kama inch 4 upana na cement iliyokolea

Na kuhusu uzito, sehem ya shimo nimejenga vyoo viwili tu kwingine ndio nimeongezea kujenga jiko na store
 
We ushajenga ushauri wa nini labda tu uweke sehem ya kupumulia ya ilo shimo ndo cha kukushauri
 
Hata nondo pia haziliwi na wadudu...

Simenti kukolea siyo factor hapo,
Hayo mazingira ni yanazalisha joto na unyevu wenye chumvi.
-Je,umetumia simenti yenye kuendana na hivyo vitu....?
-Je,kuna additives zozote ulizoweka kwenye simenti kukabiliana na hivyo vitu...?

Mbao/miti na Zege zina viwango tofauti vya kusinyaa na kutanuka, vimetofautiana sana...
-Je,ulishapiga hesabu juu ya hili...?
 
Fundi kanishauri niweke chemba za kupumulia na tumefanya ivo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…