USHAURI: Jengo la NSSF Water Front linalotazama na Magufuli SGR Station linafaa kuwa Hoteli yenye hadhi ya Nyota Tano

Architect wa jengo hilo ni mpolo,aliisha tangulia mbele na jengo alilobuni ni White elephant kwa miaka mingi sana. Sidhani kama linatumika. 🤔
Ndo maana nikafikiri namna hii, bora likaendelezwa kwa kubadilishwa matumizi. SGR imelipa uhai eneo hili tena pale hotel inafaa, maana Airport hapo (cabin crew huwa hawapendi kulala mbali), Treni unavuka barabara, bandari, mjini kati, kariakoo, BRT less than 10 mins, masaki….
 
Limeshakodishwa na wahindi wanafungua hospital
 
Kwa taarifa yako liliwahi kuwa na hotel.
 
Architect wa jengo hilo ni mpolo,aliisha tangulia mbele na jengo alilobuni ni White elephant kwa miaka mingi sana. Sidhani kama linatumika. 🤔
Uongo sio kitu kizuri.

Amandla...
 
Kipindi cha nyuma,wapangaji wote waliondolewa
Maana lilikuwa na kashkash
Matatizo ya umeme nk
Kama wanalifanyia marekebisho basi afadhali
Crdb walikuwa na branch kubwa pale pia

Ova
Ukifika sasa hivi panatia huzuni mno.. Maana ukarabari wenyewe ni wa kuungaunga mno! Inaelekea wanataka kutumia gharama ndogo sana
 
Ukifika sasa hivi panatia huzuni mno.. Maana ukarabari wenyewe ni wa kuungaunga mno! Inaelekea wanataka kutumia gharama ndogo sana
Dah hii inasikitisha sana unampa mtu kumbe na yeye ni dalali aisee
 
Pale kuweka hospitali sijui lile jengo linaoza siku hadi siku
 
Na lishawahi kuungua moto miaka hiyo kijana ukiwa unaogelea kwenye viuno vya mdingi...
Mfumo wa umeme wa jengo hilo jau,si ndomana wapangaji wote walikimbia

Ova
 
Hilo jengo lilikuwa la Nasaco ambalo liliungua. NSSF walilirithi ( sijui kama walilinunua) na wakalifanyia ukarabati na kuongeza ukumbi wa mikutano. Ilitarajiwa kuwa litatumika kama ofisi ya NSSF.
Nahisi kuwa changamoto kubwa waliyokuwa nayo ni mahali iliyopo. Kuligeuza kuwa hospitali au hoteli kutakuwa rahisi maana matumizi yote hayo yanahitaji miundombinu ya kipekee. Hamna airline itakayotaka kuweka wafanyakazi wake sehemu kama ile. Aidha, vifaa vya hospitali ni vizito na vinahitaji mazingira ya kipekee, itakuwa vigumu kukidhi vyote hivyo katika jengo hilo kama lilivyo. mwisho wa siku wataomba walibomoe ili wajenge jengo litakalokidhi wamhitaji ya sasa.

Amandla...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…