USHAURI: Jengo la NSSF Water Front linalotazama na Magufuli SGR Station linafaa kuwa Hoteli yenye hadhi ya Nyota Tano

Na lishawahi kuungua moto miaka hiyo kijana ukiwa unaogelea kwenye viuno vya mdingi...
Taja mwaka kwanza halafu tupime uzani tuone inaweza ikawa wewe ndio ulikua unaogelea kwenye viuno vya father
 
Taja mwaka kwanza halafu tupime uzani tuone inaweza ikawa wewe ndio ulikua unaogelea kwenye viuno vya father

Ni miaka mingi mzee wakati huo likiungua lilikiwa mali ya NASACO (most likely late 90's), wanaokumbuka exact date wataweka sawa mwaka...

Hili jengo la sasa ni matokeo ya usanifu na ukarabati mpya wa gofu lilikokuwa la NASACO...
 
Liko salama kwa matumizi hilo jengo? Au walipige baruti na kuanzisha jipya
 
Liko salama kwa matumizi hilo jengo? Au walipige baruti na kuanzisha jipya
Liko salama kwa maana ya structure, nguzo na msingi linahitaji tu refurbishment ya maana unalisahau kbs.
 
Ni miaka mingi mzee wakati huo likiungua lilikiwa mali ya NASACO (most likely late 90's), wanaokumbuka exact date wataweka sawa mwaka...

Hili jengo la sasa ni matokeo ya usanifu na ukarabati mpya wa gofu lilikokuwa la NASACO...

Yaani Jengo la miaka ya 90, NSSF waliacha kulibomoa wakaamua waliboreshe?

Hivi usanifu wa miaka ile, utaendana na Mahitaji ya wakati huu na miaka 50 ijayo?
 
Madhumuni ya ujenzi wa jengo hilo ni kuweka hapo Makao Makuu ya National Shipping Agencies Co. "NASACO".
Ujenzi wake umekamilika mwishoni mwa miaka ya 80.

Mwishoni mwa miaka ya 90 jengo hilo liliungua(Tuliambiwa wakora walipiga kibiriti kufuta ushahidi)
NASACO imeingia kwenye mfumo wa kuuzwa ili kuiondoa serikali kwenye biashara.

Hivyo jengo hilo liliuzwa kwa NSSF likawa kitega uchumi.
Miaka hiyo makao makuu ya IPP yalikuwa hapo.
Lengo lake ilikuwa kwa ajili ya nini?
 

Una mawazo mazuri sana.
Muhimu wasisahau kufanya tathmini ya athari kwenye mazingira, uchumi na jamii.
Kingine jengo likodishwe kwa private hotel management firm ili ijiendeshe kwa faida?
 
Uko sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…