Ushauri: Jeshi la Polisi liajiri watu wenye angalau Degree 1 yenye GPA ya kuanzia 3.5 na kuendelea

Ushauri: Jeshi la Polisi liajiri watu wenye angalau Degree 1 yenye GPA ya kuanzia 3.5 na kuendelea

Vichekesho

Member
Joined
Jun 20, 2024
Posts
66
Reaction score
3,277
Tunataka jeshi la wasomi wenye GPA kubwa ili wakifanya mambo ya hovyo tuwe na haki zote za kuwanyooshea kidole.

Mtu aliyeishia form 4 na kupata division 4 hawezi kulaumiwa kwani upeo wake hauwezi kuwa wa juu. Muda wote atahitaji kutumia nguvu kuliko akili katika utatuzi wa changamoto mbalimbali.

Natoa wito kwa Mh. Rais ikikupendeza, askari wote wenye sifa chini ya hizi wapewe mafunzo maalumu ya mgambo na watumike kwenye malindo, polisi wabaki wasomi tu.
 
Kazi za Polisi zinaitaji nguvu sana sana kuliko akili
 
Tunataka jeshi la wasomi wenye GPA kubwa ili wakifanya mambo ya hovyo tuwe na haki zote za kuwanyooshea kidole...

GPA ndio kitu gani? Mbona sehemu zote wanazoajiri kutumia GPA imekuwa ni mkutano wa watu wasiojielewa na wasiojua wanafanya nini?

Nashauri, waajiri wa sasa, hasa serikalini, waanze kuajiri watu waliosoma na kuelimika. Wanaoweza kutoa majawabu ya changamoto tunazokabiliana nazo.

Sio kukusanya watu wanaojua kukariri makaratasi mkafikiria wana akili. Wengine wengi wameshakosea
 
Mafwele ni PhD holder lakini ukatili anaotufanyia wtz ni Bora wa standard seven
 
Back
Top Bottom