Kuwa na utaratibu wa anwani ya makazi ni jambo jema lakini maboresho makubwa yanahitajika. Faida kubwa ya kuwa na anwani ya makazi ni kujulikana kwa sehemu au eneo, mtaa mtu anapoishi ili kufika kwa urahisi bila kuelekezwa na mtu.
Hapa Mwanza katika Wilaya ya Nyamagagana tayari utaratibu huu umekwishafanyika na anwani nyingi zimewekwa karibu kila nyumba bila hata kuwashirikisha wakazi wa mitaa husika.
Mitaa mingi imepewa majina bila kuwashirikisha wanaokaa kwenye mitaa hiyo. Kama inavyofahamika Mwanza ni Jiji lenye milima. Anwani hizi wameziweka sehemu nyingi ambapo hamna barabara na milimani ambapo kama mtu anataka kwenda kwa ndugu yake yenye anwani ya makazi hawezi kufika.
Nashauri kablya kuanza na anwani ya makazi kwanza wakazi wa mitaa washirikishwe kuhusu jina la mtaa kitu ambacho hakikufanyika kwa Wilaya ya Nyamagana na pili wafungue barabara ili mtu afike kwa urahisi kwenye makazi.