Ushauri kabla mwaka haujaisha tuwashike mkono wenye shida, Upendo na Maombi mtambuka

Ushauri kabla mwaka haujaisha tuwashike mkono wenye shida, Upendo na Maombi mtambuka

Pang Fung Mi

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2022
Posts
6,653
Reaction score
13,919
Katika hali ya kuishi umungu ndani yetu na kumuishi mungu wetu, Kwa rehema zake tukajae mioyo ya huruma na upendo, tukawashike mkono enye shida mfano wagonjwa hospitalini Kwa chochote kile, iwe pesa, iwe chakula etc.

Sambamba na hilo pia tusiwasahau wajane, yatima na wasiojiweza kama wenye ulemavu hasa walio kwenye vituo maalumu, tupeleke pesa, nguo, sabuni, sukari, Kwa kadri nafsi na uwezo wako ulivo.

Pia tuwaombee inspirational speakers au motivation speakers maana na wao wana mchango mkubwa katika kuhuisha uhai wetu kutuvusha kwenye changamoto zetu.

Tuwaombee wachungaji, mashekhe wanaotujenga kiroho na nafsi zetu.

Tuwaombee Madaktari hospitalini wazidishe upendo na huruma, Kwa maana shida yetu namba moja ni afya Kuyumba, Mungu awatie nguvu nanyi ni malaika katika utumishi wenu.

Tuwaombee viongozi wa kitaifa na ngazi zote sisi wa Mungu mmoja katika utumishi wao wakumbuke dhana jumuishi katika utendaji wao.
Tujiombee ongezeko la kipato na mavuno kwenye utafutaji ili tumudu kustawisha familia zetu katika nyanja zote, tujenge uchumi na taifa imara.

Tumuombe Mungu tuwe na fikra chanya nyakati zote na kuzishinda fikra hasi.

Siwezi kutaja yote Mungu atubariki sote. Katika jina lake Mungu

Amen, nawasilisha.
 
Back
Top Bottom